|
Alhamdulilah Rabil Aalamin.
Baada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu na kumtakia rehma Bwana Mtume Muhammad
S.A.W na kuwatakia radhi wasahaba zake wote.
Amma Baad: Ndugu zangu
Waislamu inampasa kila muislam azingatie jambo moja kubwa, nalo ni hizi
neema nyingi zisizokuwa na mfano alizotuoa Mwenyezi Mungu. Binaadamu tokea
anaamka asubuhi mpaka anakuja kuweka ubavu kulala, basi yumo anakula
neema za Mola wake. Wala hawezi kiumbe yeyote yule kukosa neema moja
katika neema hizo. Na hakuna anayeweza kuzikanusha wala kuzikataa.
Baada yote hayo, tukawekewa
duaa za kumfanya Binaadamu wakati wake wote umo katika ibada, wala usipe
wakati akaghafilika, yaane awe kila wakati anazikumbuka neema hizo na kuhu
akimshukuru Mola wake. Ndio Mtume wetu S.A.W akatufundisha duaa nyingi
sana zinazomfanya Muislamu asimsahau Mola wake katika kila wakati
anaoutumia. Ndio maana unapoamka tu! jambo la kwanza ni kumshukuru Allah
kwa kukuhaisha na kukuamsha tena baada ya kuwa umekufa kifo kidogo. Pamoja
na madua mengi mtakayoyaona humu. Uislam.net inajitahidi daima kumuwekea
Msomaji kila lilokuwa na faida katika maisha yake. Tafadhalini pitieni
milango ya madua na ajaribu kila muislamu kuyasoma kama yalivyopangwa,
basi hata atahisi moyo wake unapata utulivu, na Allah humuepusha na
matatizo mengi kwa uwezo wake Subhana Wataala.
|