ANUANI ZA KHUTBA

  Quraan na Sunna

  Kukinai ni Khazina

  Adhabu ya Kaburi

  Talaka

  Mayatima

  Huruma

     Uzushi

 

 
 
 
 
 
 
 
 

Khutba za Ijumaa

 SALA YA IJUMAA

Ndugu zangu Waislamu.. Katika neema kubwa za Mwenyezi Mungu ni kuwafanyia waja wake wema siku moja takita wiki ili wapate kukusanyika na kuzungumza yale ambayo huwenda yakawafaa katika maendeleo ya maisha yao. Ndio ikafaridhishwa Sala ya Ijumaa, ambayo huja faridha badala ya Adhuhuri.

Vipi Husaliwa: Sala ya Ijumaa ni Rakaa mbili. Kwanza huanza Imamu kutoka Khutba, kisha baada ya khutba ndio muadhini anaqimu Salaa ya Ijumaa. Imamu husalisha na kusoma kwa sauti katika zote rakaa mbili, ni sunna kusoma katika Rakaa ya kwanza Suraul (Sabihisma rabika.. na rakaa ya pili Hal Ataka Hadithul Ghashiyah). Na katika hukumu zake haifai kuzungumza wakati Imamu anatoa Khutba, wala kumwambia mwenzako (nyamaza).

Kasema Mwenyezi Mungu katika Suratil Jumaa Aya ya (9 - 11):

(Enyi mlioamini! Ikiadhiniwa Sala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara. Hayo ni bora kwenu, lau kama mnajua.) *  (Na itakapo kwisha Sala, tawanyikeni katika nchi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi ili mpate kufanikiwa.) * (Na wanapo iona biashara au pumbao wanayakimbilia hayo na wakakuacha umesimama. Sema: Yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora kuliko pumbao na biashara. Na Mwenyezi Mungu ni Mbora wa watoa riziki).

Baadhi ya Adabu za Ijumaa:

Ni vizuri kwa kila Muislam siku ya Ijumaa kukoga, kama anavyogoka janaba, bali maulamaa wengine wakasema kuwa ni wajib kwa kila mtu. Kisha vile vile kuelekea mapema msikitini katika saa ya mwazo ya siku hii ya Ijumaa, kwani kila ukitangulia ndio fadhila huwa zaidi kama alivyosema Bwana Mtume (S.A.W). Kisha kuvaa nguo safi na iliyo nzuri ni katika suna za Siku ya Ijumaa.

Kusikiliza Khutba:

Khutba ya Ijumaa ni huhisabiwa miongoni mwa hiyo Sala yenyewe, yaani Sala ya Ijumaa huanzia kwa Khutba, ndio maana ikakatazwa kuzungumza katika ya Khutba, na atakaezungumza na Imam anatowa khutba basi hana Ijumaa. Haifai hata kumwambia mwenzako (nyamaza). Wajibu ni kusikiliza mawaidha kwa makini na kuyazingatia yanayosemwa. Na kuhtba inatakiwa iwe na anuani muhimu katika yake yanayowakhusu Waislamu pamoja na kuwafahamisha maendeleo na maisha yao. Na khutba huwa ni mbili hukaa Imam muda mfupi baina yao.

Ijumaa kwa Wanawake:

Wanawake wa Kiislamu wanaweza kuhudhuria Sala ya Ijumaa katika Jamaa Msikitini, sharti wawe mbali na wanaume kusiwe kuna mchanganyiko. Bila ya kurefusha sauti zao na wakae nyuma ya safu za wanaume au pembeni pamoja na kuwepo pazia au sitara.

 

 

 

Copyright ©2004-2005  www.uislam.net