Bismillahi Rahmani Rahiim.
Baada ya Kumshukuru
Mwenyezi Mungu na Kumtakia Rehma Bwana Mtume Muhammad S.A.W. Mlango huu wa
Quraan ni katika milango muhimu, Kwani kukifahamu kitabu cha Allah ni
jambo la mwanzo analopaswa kila Muislamu kujielimisha. Si hoja kusikiliza
sauti nzuri tukafurahika nazo, bali kuzingatia yanayosomwa na kisha
kuyatekeleza. Na alhamdulilah Mwenyezi Mungu kawapa baadhi ya waja wake
sauti nzuri wakazitumia katika kukisoma kitabu cha Allah Subhanahu Wataala.
Na hii ni neema huwenda vile vile ikaleta athari nzuri katika masikio ya
wasikizaji. Na Quraan inaposomwa anatakiwa mwenye kusikiliza atulie na awe
makini masikio yake ili apate kuzingatia yake yanayosomwa.

Tunakuomba Allah utujaalie katika wale waja wanayoyasikia
mema kisha wakayafuata. Amin
|