|
Muislamu anapotaka kuzungumza kwanza kulipima
neno lake, lisije likawakera wenzake. Kwani ni haramu Muislamu kumkera
Muislamu mwenzake hata kwa maneno. Basi anapokuwa nalo la kusema husema na
anapokuwa hana hunyamaza kimya na ndio bora kwake. Na binaadamu neema kubwa
kapewa na Mola wake kuweza kuzungumza na kufahamiana na wenzake. Ndio
akasema Mwenyezi Mungu katika Surati Rrahmaan Aya ya (1 mpaka 4):
( ÇáÑøóÍúãóÇäõ*Úóáøóãó ÇáúÞõÑúÂäó*ÎóáóÞó
ÇáúÅöäÓóÇäó*Úóáøóãóåõ ÇáúÈóíóÇäó)
Maana yake:
“Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema* Amefundisha Qur’aani* Amemuumba binadamu*
Akamfundisha kunena”.
Na Uislamu ukabainisha wazi wazi vipi
kuitumia neema hii katika kumdhukuru Mwenyezi Mungu kila wakati bila ya
kupoteza muda katika mchezo na maneno yasiyokuwa na maana. Na Uislamu
ukapendezea zaidi kunyamaza. Kwani ndio kusalimika na makosa mengi. Ndio
Mtume (S.A.W) alisema katika Hadithi iliyotolewa na Imam Ahmad kwa njia ya
Abi Dhar Al ghafariy:
( Úáíßó ÈöØõæáö ÇáÕøóãúÊ ¡ ÝÅäøóåõ ãóØúÑóÏÉ
ááÔøíúØóÇä ¡ æóÚóæúä áóß óÚóáì ÃóãúÑö Ïöíúäößó )
Maana yake:
“Jilazimishe sana kukaa kimya.
Kwani huko ni kumfukuza shetani, na hukusaidia katika kutekeleza mambo ya
Dini yako.”
Sadakta ya Sayidi ya Rasula Llaah. Kwani
binaadamu kila akijishughulisha na maneno mengi akawa kila kitu hutaka
kujuwa ndio huwa hana hata wakati wa ibada. Na tabia hii imekatazwa katika
Uislamu. Kasema Mtume (S.A.W) katika Hadithi iliyotolewa na Imam Tirmidhiy:
( ãöäú ÍõÓúäö ÅöÓúáóÇãö ÇáúãóÑúÁö ÊóÑúßõåõ
ãóÇ áóÇ íóÚúäöíåö )
Maana yake:
“Katika dalili bora ya Uislamu wa
mtu. Ni kuacha yaliyokuwa hayamukhusu.”
Jambo madhali halikuhusu basi usilifuatie
ukaja ukafedheheka. Mambo ya watu yaache kwa wenyewe. Ila ikiwa katika njia
ya kupanisha watu. Lakini sio kila kinachotokea katika nyumba ya jirani yako
nawe ukijuwe. Ndio huo umbea! Kutaka kuishibisha roho yako kwa vitu vya watu!
Namna hiyo moyo wa Muislamu kabisa utakuwa bado hauko sawa, tena unahitajia
matibabu ya hali ya juu kabisa. Ndio Mtume (S.A.W) kasema katika Hadithi
iliyotolewa na Imam Ahmad:
(
áóÇ íóÓúÊóÞöíãõ ÅöíãóÇäõ ÚóÈúÏò ÍóÊøóì íóÓúÊóÞöíãó ÞóáúÈõåõ ¡ æóáóÇ
íóÓúÊóÞöíãõ ÞóáúÈõåõ ÍóÊøóì íóÓúÊóÞöíãó áöÓóÇäõåõ ¡ æóáóÇ íóÏúÎõáõ ÑóÌõáñ
ÇáúÌóäøóÉó áóÇ íóÃúãóäõ ÌóÇÑõåõ ÈóæóÇÆöÞóå )õ
Maana yake:
“Haitokuwa madhubuti Imani ya mja
mpaka unyooke moyo wake. Na haotunyooka moyo wake mpaka unyooke ulimi wake.
Na wala hatoingia Peponi yule mtu ambaye hampi uaminifu jirani yake. Kwa
yale mabaya anayomtendea.”
Wallahi ingelikuwa ulimwenguni yanatazamwa
yale wanayoyasema watu, basi yangelikutikana mengi ni maneno ya upuuzi. Wala
hayana faida katika maisha yao. Laiti vikao kama hivi vikawa vya kutafuta
elimu na kupeana nasaha. Ndio maana shetani akawa na nguvu za kutosha
katika kuwapoteza watu. Kwani vingalikuwa vikao vya Waislamu katika kumtaja
Allah, basi shetani maluuni asingelipata wafuasi wengi, ila wale wale tu
waliopotoka. Mwenyezi Mungu alaeleza hayo katika Suratil Israa Aya ya
(63-64):
( æóÇÓúÊóÝúÒöÒú ãóäú ÇÓúÊóØóÚúÊó ãöäúåõãú
ÈöÕóæúÊößó æóÃóÌúáöÈú Úóáóíúåöãú ÈöÎóíúáößó æóÑóÌöáößó æóÔóÇÑößúåõãú Ýöí
ÇáúÃóãúæóÇáö æóÇáúÃóæáóÇÏö æóÚöÏúåõãú æóãóÇ íóÚöÏõåõãú ÇáÔøóíúØóÇäõ ÅöáøóÇ
ÛõÑõæÑðÇ*Åöäøó ÚöÈóÇÏöí áóíúÓó áóßó Úóáóíúåöãú ÓõáúØóÇäñ æóßóÝóì ÈöÑóÈøößó
æóßöíáðÇ)
Maana yake:
“Na
wavute uwawezao miongoni mwao kwa sauti yako, na uwakusanyie (jeshi lako la)
wapandao farasi na waendao kwa miguu. Na shirikiana nao katika mali yao na
watoto wao, na wa’ahidi ahadi za uwongo. Lakini shetani hawapi wa’adi ila wa
udanganyifu”.
Na Mtume (S.A.W) kasema katika Hadithi
iliyotolewa na Imam Al Bukhari:
( Åöäøó Çááøóåó ßóÑöåó áóßõãú ËóáóÇËðÇ Þöíáó
æóÞóÇáó æóÅöÖóÇÚóÉó ÇáúãóÇáö æóßóËúÑóÉó ÇáÓøõÄóÇáö)
Maana yake:
“Kwa hakika Mwenyezi Mungu
anachukizwa kwenu na mambo matatu. Kuzungumza sana, na kupoteza mali (kwa
kufanya israfu) na kuuliza uliza sana mambo ya watu.”
Kwa hivyo Muislamu anapotaka kuzungumza
na wenzake, awe mpole sio kuropokwa bila ya faida. Tena kwa adadu nzuri bila
kuhamaki na kukunja uso. Ikawa ghadhabu haimwishi katika uso wake.
|