|
Hitimisho
La kushangaza baada ya yote hayo Waislamu tumelinyamazia kimya suala la
UKIMWI katika jamii yetu. Tukiangalia miongoni mwa taasisi na mashirika
ya Kiislamu hakuna juhudi za kweli na maksudi kukabiliana na UKIMWI ima
kwa kuandaa mipango au miradi au kutoa huduma za kimaisha au kiroho kwa
waliokumbwa na janga la UKIMWI.
Suala jengine la kujiuliza uko wapi machango wa wanawake wa Kiislamu ?
Na vikundi vingapi vya wanawake wa kiislamu vinajishughulisha na
taathira za UKIMWI?
Kwa jumla Waislamu bado hatujaanza kulizungumzia suala la UKIMWI na
jinsi ya kujinusuru nao. Imekuwa rahisi kujihami na " la takrabu zinaa
yaani musikaribie zinaa bila ya KUCHUKUA HATUA ZA VITENDO ZA UJUMBE WA
AYA TUKUFU na kuzingatia kwa upande mwengine mazingira na desturi
zinopelekea kushamIri kwa mienendo na hulka zinostawisha kuenea kwa
UKIMWI Inafaa kwa wakati huu, wa kujitakasa nafsi mtafakari kwa undani
zaidi jinsi kunavyokabiliana na janga hili, gonjwa lisilo na dawa wala
kinga thabiti.
TAMATI |