AINA ZA SUMU

  Vifungu vya Saumu:

Saumu imegawika vifungu vinne:

1-Saumu iliyo wajibu (faradhi).

2-Saumu iliyo haramu.

3-Saumu iliyo himizwa.

4-Saumu iliyo makruhu.

 Saumu iliyo wajibu ni:

Saumu ya Mwezi wa Ramadhani, Saumu ya nadhiri, Saumu ya kaffara; kaffara ya kuuwa, kaffara ya “Dhihar” (mume kumwambia mkewe: wewe kwangu ni kama mgongo wa mama yangu basi anaharimika kwake mpaka atoe kaffara), Kaffara ya “Ilaau” yaani mwanamme kuapa kuwa hatamwingilia mkewe basi hatoweza kumuingilia mpaka atoe kaffara, kaffara ya kwenda kinyume na kiapo chake na Saumu ya Attamatuu kwa yule asieweza kumiliki kuchinja na kirefu cha haya kitapatikana katika vitabu vya Fiqhi.

  Saumu iliyo Haramu:

Kufunga katika Idi mbili (Al-Fitri na Al-Adh-haa) na kufunga kwa aliye katika hedhi na ujusi (kwa mwanamke) na kufunga siku ya shaka nayo ni tarehe 30 thelathini shaabani haifungiwi siku hii ili isiongezeke siku katika Ramadhani kutoka mwezi mwengine. Kama ilivyosemwa kutokana na Ikrima R.A. na Ammar R.A. wamesema: Aliyefunga siku inayotiliwa shaka basi amemuasi Aba Al-Qasim bali inavyopendelewa kuwa atiye niya ya kufunga siku ile iwe mwezi mosi Ramadhani halafu ajizuie mpaka katikati ya mchana ikaja habari ya kuonekana mwezi aendelee na funga yake lakini juu ya hivyo hapana budi kuilipa siku ile kwa sababu hakuiamkia siku ile naye ana hakika kamili kuwa ni Ramadhani na katika sharti ya Saumu kuwa atiye niya ya uhakika tokea siku.

  Saumu iliyohimizwa:

Saumu ya Ashuraa (siku ya kumi ya Muharram) na aongeze kufunga siku moja kabla yake au siku baada yake ili kuwahalifu (kwenda kinyume) mayahudi na manasara kwa sababu wao waitukuza siku hii kwa kuifunga, vile vile inahimizwa kufunga siku ya Arafa kwa mujibu wa kauli ya Mtume (Salallahu Alayhi Wasalam) :

(صوم يوم عرفة يكفر سنتين ماضية , و مستقبلة و صوم عاشوراء يكفر سنة ماضية )

“Saumu katika siku ya Arafa hufuta (madhambi ya) miaka miwili uliopita na unaokuja, na Saumu katika siku ya Aashuraa hufuta madhambi ya mwaka uliopita.”

Inapendelewa vile vile kufunga siku tatu, “Ayyaam Beiydh” nazo ni tarehe 13, 14 na 15 katika kila mwezi wa Hijri (mwezi wa Kiislamu) isipokuwa tarehe 13 katika mwezi Dhul Al-Hijja kwa sababu ni katika siku za “Attashriq”. Amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam

( من صام في كل شهر ثلاثة أيام فكأنه صام الدهر كله )

Anaefunga katika kila mwezi siku tatu basi kama aliyefunga zama zote (milele). Na pia inapendelewa kufunga siku sita katika Shawwaal kwa mujibu wa kauli yake Mtume Salallahu Alayhi Wasalam:-

 ( من صام رمضان ثم أتبعه بستة أيام من شوال فكأنه صام الدهر كله )

“Anaefunga Ramadhani kisha akaifuatilia (kwa kufunga) na siku sita katika Shawwaal basi kama kwamba amefunga milele”.

Inahimizwa kufanya Iitikaaf mwisho wa Ramadhani na ifanywavyo ni kuingia msikiti unaosaliwa jamaa kabla ya kutuwa jua usiku wa tarehe 21 Ramadhani afanya hivyo kwa ajili ya radhi ya Mwenyezi Mungu Subhanahu Wa Taalah na kutarajia malipo yake bila ya kuwa na kusudio lingine na kuwa ajifungie nafsi yake katika msikiti huo kwa kufanya ibada na asitoke humo isipokuwa kwa kwenda kusali Sala ya Idi. Hivi ndivyo ilivyokuwa Sunna. Anaetaka kufanya Iitikaaf chini ya muda huo na atiye niya kabla kwa mujibu wa siku anazotaka kukaa Iitikaaf na haitakiwi kubadilisha niya hiyo wakati yuko msikitini katika Iitikaaf wala asijishughulishe na mambo ya kiDunia isipokuwa kwa mambo ya dharura kama kwenda kukidhi haja au kwenda kula ikiwa hawezi kula msikitini.

Na akifanya Iitikaaf katika wakati usiokuwa Ramadhani basi ni shuruti afunge. Na kufanya Iitikaaf katika Ramadhani na hasa katika kumi la mwisho kuna mambo ya kheri Mwenyezi Mungu huyaleta katika wakati huu na asa akafanikiwa kuipata Laiylatul Al-Qadri. Mtume Salallahu Alayhi Wasalam alifanya Iitikaaf katika mwanzo wa mwezi wa Ramadhani na katikati yake na mwisho wake na hii ndio ilikuwa amali yake ya mwisho Salallahu Alayhi Wasalam. Na Masahaba walikuwa wakichukuwa kwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam vitendo vyake vya mwisho mwisho (hawachukuwi) vya zamani lakini wachukuwa vipya). Na alikuwa Mtume Salallahu Alayhi Wasalam akifunga zaidi katika mwezi wa Shaabani (kuacha mwezi wa Ramadhani) lakini ni lazima afungue siku mbili za mwisho wa Shaabani asiziunganishe na Ramadhani kwa mujibu wa kukataza kwake Salallahu Alayhi Wasalam kuiunganisha Ramadhani na mwengine.

  Saumu iliyo makruhu:

Ni Saumu ya siku za “Attashriq” nazo ni siku tatu zinazofuatia Idi Al-adh-ha (Idi kubwa) kwa sababu hizo ni siku ambazo Mwenyezi Mungu Subhanahu Wa Taalah anawafanyia “dhiyafa” (anawakaribisha na kuwakirimu) waja wake kwa hiyo haifai kuikataa dhiyafa yake na sababu ya kuitwa ayyam “attashriiq” kwa sababu huanikwa nyama katika jua siku hizo. Na vile vile ni makruhu kufunga siku moja au mbili kabla ya Ramadhani ili zisiungane nao, na pia kufunga siku ya Ijumaa peke yake isipokuwa kama ikitanguliwa na siku au ikifuatiliwa na siku kwa sababu wamesema kuwa Ijumaa ni Idi na haifai kufunga siku ya Idi.

Amesema Shekhe wetu Noor Diin Mwenyezi Mungu Amrehemu kuwa tofauti iliopo baina ya Idi na siku ya Ijumaa kuwa imekubaliwa kwa ujumla kwamba ni haramu kufunga siku ya Idi hata ikatanguliwa kufungwa siku moja au ikafatiliwa na siku moja ambayo ni kingume ya siku ya Ijumaa kwani imekubaliwa kwa ujumla kwamba inaruhusiwa kufunga siku ya Ijumaa ikiwa itatanguliwa au ikafatiliwa na kufunga siku moja. Vile vile katika Saumu iliyo makruhu kufunga milele.

Amesema Mtume Salallahu Alayhi Wasalam:

لا صام من صام الأبد

“Hajafunga mwenye kufunga milele”

na kauli yake aliemwambia Abdullah bin Omar:

صم صيام داود : كان يصوم يوما ويفـطر يوماً ولا يفـر إذا لاقي

“Funga Saumu ya Dawood alikuwa afunga siku na afungua siku na hakuwa akikimbia akutanapo (na adui) na aliambiwa hivyo wakati aliposhikilia ombi lake la kutaka kufunga milele akamnasihi Salallahu Alayhi Wasalam asifanye hivyo na akamwambia:

( صم و افطر و قم و نم , فإن لعينيك عليك حقا و إن لنفسك و أهلك عليك حقا )

“Funga na ufungue, usimame (kwa kufanya Ibada) na ulale kwani jicho lako lina haki juu yako na nafsi yako na watu wako (mke na watoto wako) wana haki juu yako” na katika hadithi nyingine “wana hadhi juu yako”.

Vile vile katika Saumu iliyo makruhu ni Saumu ya msafiri akiwa amedhoofika hata akawa hawezi kufanya yale yaliyomuwajibikia kuyafanya kama alivyofanya Mtume Salallahu Alayhi Wasallam katika baadhi ya vita vyake alipoona uchofu umedhihiri kwa masahaba zake kutokana na kufunga basi akawaamrisha wafungue kwa kuwaonea huruma kwa hiyo msafiri amepewa ruhusa ya kufungua na hiyo ni Rehema ya Mwenyezi Mungu Subhanahu Wa Taalah juu ya waja wake.

Saumu kwa ujumla ni kheri na ina fadhila kubwa isipokuwa kwa zile siku zilizokatazwa kufunga kwa mujibu wa kauli yake Salallahu Alayhi Wasalam:

لكل شيء  زكاة  وزكاة الجسد الصوم

Kila kitu kina Zaka na Zaka ya kiwiliwili ni Saumu.

Na katika kauli yake Salallahu Alayhi Wasalam:

( من صام يوماً ابتغاء وجه الله أبعده الله من جهنم كبعد غراب طائر و هو فرخ حتى مات هرما )

“Anaefunga siku moja kwa kutaka kumridhisha Mwenyezi Mungu (tu peke yake) basi Mola humuweka mbali na Jahannam kama umbali wa kunguru anaeanza kupuruka yu hali ni kinda mpaka anapokufa naye amekonga”.

Hadithi mbili hizi zimetolewa na Abu Huraira. Na katika hadithi:

( لكل شيء  زكاة  وزكاة الجسد الصوم)

 

Kila kitu kina Zaka na Zaka ya kiwiliwili ni Saumu.

Na katika kauli yake Salallahu Alayhi Wasalam:

( من صام يوماً ابتغاء وجه الله أبعده الله من جهنم كبعد غراب طائر و هو فرخ حتى مات هرما )

“Anaefunga siku moja kwa kutaka kumridhisha Mwenyezi Mungu (tu peke yake) basi Mola humuweka mbali na Jahannam kama umbali wa kunguru anaeanza kupuruka yu hali ni kinda mpaka anapokufa naye amekonga”.

Hadithi mbili hizi zimetolewa na Abu Huraira. Na katika hadithi:

(الشتاء ربيع المؤمن طال ليله فقام وقصر نهاره فصام)

Siku za baridi ni faida kwa mwenye kuamini usiku wakni mrefu kwa hiyo hupata kusimama (usiku kufanya ibada) na mchana wake ni mfupi na hufunga.