|
Jee! Uislamu ni
Dini ya haki?
Ndugu zangu Wasomaji madhumuni ya makala au maelezo haya sio kupinga dini
yoyote, wala kumhujumu aliyekuwa si Muislamu, au kumshambulia Muislamu
aliyekuwa hafuati Uislamu kama anavyotakiwa. Lakini madhumuni ya
maelezo haya ni kuwasaidia wale ambao wanataka kujisaidia nafsi zao,
ambao wanataka kujua na kuufahamu ukweli wa dini hii na umuhimu wa
kuifuata na kutekeleza maamrisho ya Mungu mmoja wa haki kwa ajili ya
maslaha, mafanikio na faida ya pamoja ya duniani na akhera.
Kwanza itabidi tukubaliane kuwa katika ulimwengu huu tunaoishi hakuna
maneno yaliokuwa hai, ya ukweli, yenye maana, yenye uwongofu yaliokuwa
madhubuti kama maneno ya Mwenyeezi Mungu. Hili jambo halina wasi wasi wala
shaka hata kidogo. Kwa hivyo maneno yaliotajwa na Mola wetu katika kitabu
cha mwisho cha viumbe wote ambacho ni Qur’ani, kilicholetwa miaka elfu
kumi na nne nyuma. Kitabu hicho bado kipo hai na yataendelea maneno yake
kuwa hai, kudumu na kudhihiri ukweli wake na kufahamika zaidi, kwa sababu
Mwenyeezi Mungu kachukuwa ahadi ya kukilinda kitabu hicho. (Qur’ani)
Qur’ani ni maneno ya Mwenyeezi Mungu ambayo wajibu wa kila mwenye akili,
fahamu, ujuzi na busara kwa Binaadamu na Majini kukiamini na kukifuata
kitabu hicho na kuyazingatia na kuyapekecha maamrisho hayo ikiwa tunataka
uwongofu, amani, salama ya nafsi zetu na himaya ya maisha yetu kutoka kwa
Mola wetu kwa maslaha ya hapa duniani na Akhera.
Mungu huyo mmoja (wa kweli na wa haki) ni yule yule aliyemteremshia
uwongofu Mtume Nuhu, Mtume Ibrahim, Mtume daudi, Mtume Musa, Mtume Issa,
Mtume Muhammad na Watume wengineo wote wa mwanzo waliopita. Kwa yoyote
asiyewaamini watume hao waliotajwa na Mola wetu basi hajawa Muislamu wa
kweli, kwani anapinga maneno ya Mola wake.
Aya ifuatayo au maneno haya ni kutoka kwenye kitabu kitukufu cha
Mwenyeezi Mungu, ambaye anatubainishia kwa kutufahamisha na kutuilimisha
waja wake. Kwa hivyo ndugu msomaji nakuusia yasome zaidi ya mara moja na
jaribu kuyafahamu na kuyazingatia ili upate faida zaidi.
ÔóÑóÚó áóßõã ãøöäó ÇáÏøöíäö ãóÇ æóÕøóì Èöåö äõæÍðÇ
æóÇáøóÐöí ÃóæúÍóíúäóÇ Åöáóíúßó æóãóÇ æóÕøóíúäóÇ Èöåö ÅöÈúÑóÇåöíãó æóãõæÓóì
æóÚöíÓóì Ãóäú ÃóÞöíãõæÇ ÇáÏøöíäó æóáóÇ ÊóÊóÝóÑøóÞõæÇ Ýöíåö
Amekuamrisheni (sharia ya) dini ile ile aliyomuusia Nuhu na
tuliokufunulia wewe (Muhammad), na tuliowausia Ibrahim, na Musa na
Issa, kwamba shikeni dini wala msifarikiane kwa hayo.
Ash-shuura-13
Watume wote walioteremshwa na huyo Mungu mmoja (jina lake Allah)
wameteremshwa kwa ajili ya maelekezo yale yale waliokuja nayo Watume
waliopita. Na kusisitizwa kuwa hakuna Mungu wa kuabudiwa isipokuwa
Mungu mmoja tu. Na ujumbe ni ule ule wa kuwatetea viumbe na kila
mabaya na kuwaongoza waliopotea ili washikamane na uwongofu unaotoka kwa
Mola wao kwa madhumuni ya kuwa wawe viumbe bora, waweze kuishi maisha
mazuri duniani na kupata ujira wa kuishi maisha mazuri Akhera.
Kwa kuwa Mungu alioteremsha Watume na vitabu vilivyopita ni yule yule
‘Allah’ kwa hivyo hapa inabidi tukubaliane kuwa ‘Allah’ alikuwa kishapanga
kuwa atamleta Mtume mwengine baada ya Mtume Musa na Issa, na kuamua kuwa
huyo ndiye atakaekuwa Mtume wa mwisho, ambaye jina lake litakuwa Muhammad
(Ahmad), alikuwa kishaweka wapi amweke na lini amkabidhi jukumu la Utume.
Aya zifuatazo zinathibitisha hayo.
Kutabiriwa Mtume
Muhammad (SAW) katika Taurat na Injiil
ÇáøóÐöíäó íóÊøóÈöÚõæäó ÇáÑøóÓõæáó ÇáäøóÈöíøó ÇáÃõãøöíøó
ÇáøóÐöí íóÌöÏõæäóåõ ãóßúÊõæÈðÇ ÚöäÏóåõãú Ýöí ÇáÊøóæúÑóÇÉö æóÇáÅöäúÌöíáö
íóÃúãõÑõåõã ÈöÇáúãóÚúÑõæÝö æóíóäúåóÇåõãú Úóäö ÇáúãõäßóÑö æóíõÍöáøõ áóåõãõ
ÇáØøóíøöÈóÇÊö æóíõÍóÑøöãõ Úóáóíúåöãõ ÇáúÎóÈóÂÆöËó æóíóÖóÚõ Úóäúåõãú
ÅöÕúÑóåõãú æóÇáÃóÛúáÇóáó ÇáøóÊöí ßóÇäóÊú Úóáóíúåöãú ÝóÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇú
Èöåö æóÚóÒøóÑõæåõ æóäóÕóÑõæåõ æóÇÊøóÈóÚõæÇú ÇáäøõæÑó ÇáøóÐöíó ÃõäÒöáó
ãóÚóåõ ÃõæúáóÜÆößó åõãõ ÇáúãõÝúáöÍõæäó
Ambao kwamba wanamfuata huyo Mjumbe, Mtume, asiyesoma wala kuandika,
wanayemkuta kaandikwa kwao katika Taurat na Injiil, anayewaamrisha
mema na anayewakataza mabaya (maovu), na anawahalalishia vizuri, na
anawaharamishia viovu, na anawaondolea mizigo yao, na minyororo iliyokuwa
juu yao. Basi wale waliomuamini yeye, na wakamhishimu, na wakamsaidia, na
wakafuata nuru iliyoteremshwa pamoja naye, hao ndiyo wenye kufanikiwa.
Al A’raaf-157
Maelezo zaidi
Maneno haya ya Mwenyeezi Mungu yanatuonesha dalili zilizo wazi kuwa
Mayahudi na Manasara walikuwa wanajua kuwa atakuja Mtume mwengine na
utakuja uwongofu wa kitabu changine kwa sababu washaambiwa na Mola wao.
Na sababu ya kuambiwa huko ni kuwa wasimpinge na wamkubali na wafuate
uwongofu mpya huo utakapofika (Qur’ani).
Lakini yalipodhihiri hayo wengine hawakukubali, na moja ya sababu ya
kutokubali ni kuwa Mtume huyo hakutokana katika wao. Wakubwa hao na
wafuasi wao wakaona wakikubali basi itabidi vyeo vyao na mamlaka ya
wafuasi wao vitatoweka. Kwa hivyo wakafanya kila njia kupinga na kukataa
kufuata na kutii amri ya Mola wao na Mitume wao.
Sifa hizi za Mtume huyu (Muhammad) asiyejua kusoma wala kuandika,
zimetajwa katika aya nyangine vile vile. Na sababu kubwa ni kuonesha
dalili kuwa haya yaliokuja hayatoki kwa Muhammad, yeye hana ilimu, si
msomi wala muandishi, huu ni ujumbe unaotoka kwa ‘Allah’ kwa hivyo
atakayepinga huwa hampingi Muhammad, bali anampinga mwenyeezi Mungu. Ewe
Muumbwa! Una uwezo wewe wa kumpinga Muumbaji?
æóãóÇ íóäØöÞõ Úóäö Çáúåóæóì Åöäú åõæó ÅöáøóÇ æóÍúíñ íõæÍóì
Úóáøóãóåõ ÔóÏöíÏõ ÇáúÞõæóì
Na wala hatamki kwa matamanio (yake Muhammad). Hayakuwa haya ila
ufunuo uliofunuliwa. Amemfundisha aliye mwingi wa nguvu (Mwenyeezi
Mungu).
Annajm-3, 4, 5
Kwa
hivyo aliyokuwa akiyaleta na kuyafundisha Mtume Muhammad (SAW) ni
maamrisho kutoka kwa Mwenyeezi Mungu, sio maamrisho kutoka kwake Muhammad,
yeye hakuwa na ilmu ya darja kubwa kama hii, yeye hakuwa mjuzi wala msomi,
kwa hivyo ukweli uko wazi, na wapinzani huwa wanampinga Mola.
Kwa hakika kuja kwa Mtume mpya (Muhammad) na kitabu kipya (Qur’ani)
ilikuwa ni rehma kubwa kwa Mayahudi (wafuasi wa Taurat), Manasara (wafuasi
wa injiil) na wengineo, kwani upotofu wa viongozi wao uliwafanya viumbe
hawa kuwa wamejitwika mizigo mikubwa na wamejifunga na minyororo ya shida
na dhiki. Kwani walikuwa wamejiharamishia mambo wenyewe, wamejiwekea
vikwazo vya kimaisha vya kila aina kwa kufuata mila zao, wafuasi wao na
kufuata nyao za mababu zao.
Ama wale waliomuamini aliyokuja nayo Mtume Muhammad (SAW), na
wakamuhishimu, na wakamsaidia, na wakafuata nuru iliyoteremshwa kutoka kwa
Mola wao, hao ndiyo waliofanikiwa duniani na Akhera. Kwani wameitikia wito
wa Mola wao na wametii amri na kufuata uwongofu mpya uliowajia wa Qur’ani.
Kutabiriwa Mtume Muhammad (SAW) na Mtume Issa (as)
æóÅöÐú ÞóÇáó ÚöíÓóì ÇÈúäõ ãóÑúíóãó íóÇ Èóäöí ÅöÓúÑóÇÆöíáó
Åöäøöí ÑóÓõæáõ Çááøóåö Åöáóíúßõã ãøõÕóÏøöÞðÇ áøöãóÇ Èóíúäó íóÏóíøó ãöäó
ÇáÊøóæúÑóÇÉö æóãõÈóÔøöÑðÇ ÈöÑóÓõæáò íóÃúÊöí ãöä ÈóÚúÏöí ÇÓúãõåõ ÃóÍúãóÏõ
ÝóáóãøóÇ ÌóÇÁåõã ÈöÇáúÈóíøöäóÇÊö ÞóÇáõæÇ åóÐóÇ ÓöÍúÑñ ãøõÈöíäñ
Na Issa mtoto wa Maryam aliposema: Enyi wana wa Israili! Hakika mimi ni
Mtume wa Mwenyeezi Mungu kwenu, ninathibitisha yaliyokuwa kabla yangu
katika Taurat, na mwenye kubashiria kuja Mtume atakaye kuja baada yangu,
jina lake ni Ahmad. Lakini alipo waletea hoja zilizowazi walisema: Huu
ni uchawi ulio dhahiri.
Ass’af-6
Maelezo zaidi
Hapa kuna mambo mawili yanakwenda sambamba, kwanza Mtume Issa anawaambia
Mayahudi ambao walikuwa wakifuata Taurat, kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyeezi
Mungu, na anayathibitisha na kuyakubali yaliokuja katika Taurat, yaani
aliyokuja nayo Mtume Musa. Kwa hivyo wamkubali na wafuate kitabu kipya cha
Injiil alichoteremshiwa yeye Mtume Issa.
Jambo la pili (Mtume Issa) anawabashiria (kwa amri ya Mwenyeezi Mungu)
kuwa vile vile kutakuja Mtume mwengine baada yake jina lake Ahmad, kwa
hivyo ina maana kwa wakati ule alikuwa akiwalingania wafuate uwongofu mpya
wa Injiil, na waache Taurat, na kuwabashiria kuwa ukifika uwongofu mpya
baada ya Injiil, wote wafuate uwongofu huo atakayekuja nao huyo Mtume
ambaye jina lake Ahmad (Muhammad).
Mtume alipozaliwa, baba yake alikuwa kisha kufa, mama yake alimpa jina la
Ahmad, na baada ya kufa mama yake akachukuliwa kulelewa na Babu yake
ambaye akamwita Muhammad, na inasemekana kuwa Ahmad na Muhammad ni jina
moja.
Sasa tukirudi tena kwa Mtume Issa,
wakati alipo waletea hoja zilizowazi kabisa, wakaona hawana njia ya
kuyakimbia isipokuwa walisema: “Huu ni uchawi ulio dhahiri” ili waendelea
na mambo waliokuwa wanakwenda nayo, lakini ukweli wanaujua na wanayafahamu
uzuri.
Kwa hivyo nawausia ndugu zangu waliokuwa
bado hawajaamua kujisalimisha kwa Mungu wa haki, Mungu wa mitume wote
waliopita kuwa wasikubali kupotezwa kwa kumuasi Mola wao na Mitume yao.
Kwani wamepewa akili na fahamu nzuri ya kuyazingatia haya. Kwa hivyo ni
wajibu kuutumia uwezo huo wa fahamu kwa kutafuta njia ya uwongofu ili
isifike wakati wakafa na wao bado hawajaamua kujisalimisha kwa Mola wao.
Kwani mtu akifa na bado hajarejea kwa Mola wake, basi malipo yake ni moto
mkali sana wa milele wenye maumivu makubwa sana.
Kubashiriwa kuja Mtume Muhammad (SAW) katika Taurat
Þõáú ÃóÑóÃóíúÊõãú Åöä ßóÇäó ãöäú ÚöäÏö Çááøóåö æóßóÝóÑúÊõã
Èöåö æóÔóåöÏó ÔóÇåöÏñ ãøöä Èóäöí ÅöÓúÑóÇÆöíáó Úóáóì ãöËúáöåö ÝóÂãóäó
æóÇÓúÊóßúÈóÑúÊõãú Åöäøó Çááøóåó áÇó íóåúÏöí ÇáúÞóæúãó ÇáÙøóÇáöãöíäó
Sema: Mwaonaje yakiwa haya ni kweli yanatoka kwa Mwenyeezi Mungu, nanyi
mmeyakataa, na akashuhudia shahidi miongoni mwa wana wa Israili juu ya
mfano wa haya, na akaamini na nyinyi mnafanya kiburi? Hakika Mwenyeezi
Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.
Ah’qaaf-10
Maelezo zaidi
Aya hiyo ya juu inaeleza kuhusu mmoja miongoni mwa Mayahudi jina lake *Abdallah
bin Salaam, ambaye alisilimu, na alipoulizwa kwa nini amesilimu, akasema
kwa kuwa Mtume Muhammad (SAW) ametajwa katika Taurat. Lakini wengine
wakatakabar na kukataa kuamini. *(Kutoka katika tafsiri ya Attabriy-
sababu za kuteremshwa Qur’an)
Tumeona maelezo na mafahamisho ya aya hizo tulizozipitia, ambazo ni
maneno yaliotoka kwa ‘Allah’ (Mwenyeezi Mungu) sio maneno ya Muhammad wala
si maneno ya Waislamu. Maneno hayo yanatupa ukweli kuwa Mungu wa Watume
wote ni mmoja. Sasa kwa nini tunamkubali Mungu mmoja na hatumkubali
Muhammad. Ikiwa imefika hadi Muhammad kutajwa katika Injiil na Taurat,
maana yake tumkubali na kumfuata kwa yale yalioteremshwa na Mola wetu.
Na ikiwa hatufanyi hivyo, basi inamaanisha kuwa hata hivyo vitabu
tuliokuwa navyo hatuvifuati na tunavipinga au hatukubaliani na
yalioandikwa, na khatari zaidi kuwa tunampinga Mungu wa Watume wote hao
tunaowaamini. Kwa hivyo inamaanisha kuwa hatufuati, Taurat, wala Injiil
wala Qur’ani. Sasa tunafuata dini gani na Mungu yupi tunayemuamini?
Ndugu yangu ikiwa hujaamua au kutia nia kujisalimisha kwa Mungu wa
haki ‘Allah’ na kufuata kitabu chake cha mwisho Qur’ani, siwezi kusema
kuwa umepotea, lakini nakuomba ujionee huruma nafsi yako, viumbe sote
tunakosa, lakini makosa ya kumpinga Mwenyeezi Mungu ni makubwa mno na yana
hatari kubwa duniani, na majuto makubwa yatakuwa siku unayokufa na
ukaondoka duniani umedhalilika na adhabu kali ya moto wa Akhera
inakungojea.
Inahitaji ndugu zangu tufikiri, tuzingatie nafsi zetu, na tuamue kufuata
njia ya uwongofu, na tusifuate upotofu. Tusiwe wakaidi na wabaya wa nafsi
zetu, kwani tumepewa akili kwa hivyo inatuwajibikia kuitumia kwa kuchukuwa
uamuzi wa kheri na wa kweli. Hapa hakuna kuvungana kila kitu kipo wazi
kabisa. Ikiwa ndugu yangu bado hujaridhika na yote yaliokuzunguka, basi
kuwa mstahamilivu na jitahidi kusoma yanayofuatia ili upate maelekezo
zaidi.
Ãóãú ÊóÞõæáõæäó Åöäøó ÅöÈúÑóÇåöíãó æóÅöÓúãóÇÚöíáó
æóÅöÓúÍóÜÞó æóíóÚúÞõæÈó æóÇáÃÓúÈóÇØó ßóÇäõæÇú åõæÏðÇ Ãóæú äóÕóÇÑóì Þõáú
ÃóÃóäÊõãú ÃóÚúáóãõ Ãóãö Çááøåõ æóãóäú ÃóÙúáóãõ ãöãøóä ßóÊóãó ÔóåóÇÏóÉð
ÚöäÏóåõ ãöäó Çááøåö æóãóÇ Çááøåõ ÈöÛóÇÝöáò ÚóãøóÇ ÊóÚúãóáõæäó
Au mnasema (nyinyi Mayahudi na Manasara) kuwa Ibrahim na Ismail
na Is’hak na Yaakub na wajukuu zao waliokuwa Mayahudi au Wakristo? (kama
nyinyi) Sema: Je nyinyi mnajua zaidi au Mwenyeezi Mungu? Na ni
nani mwenye kudhulumu zaidi kuliko yule aliyeficha ushahidi alionao utokao
kwa Mwenyeezi Mungu? Na Mwenyeezi Mungu sio mwenye kughafilika kwa hayo
mnayoyafanya.
Al Baqara-140
Maelezo zaidi
Mayahudi na Manasara (Wakristo) hawakupendekezewa kuona kaja Mtume sio
katika jamii yao. Ijapokuwa ametabiriwa katika hivyo vitabu wanaosema kuwa
ndivyo wanavyovitegemea, kwa hivyo hawakukubali kufuata maelekezo hayo, na
mpaka leo wanaendelea na ushindani wao wa kutomkubali Mtume Muhammad (SAW)
na kutoikubali Qur’ani inayotoka kwa Mola wao huyo huyo aliyewateremshia
Taurat na Injiil.
Na baada ya kutokubali ukweli wakawa wanapindukia mipaka na kuipinga na
kujadiliana, hata kufika hadi kusema kuwa Mitume fulani na fulani
wametokana na katika sisi, yaani wanamtowa makosa Mwenyeezi Mungu kwa
nini basi asilete Mtume kutokana na wao, kenda kuleta Mtume kutokana na
jamii ya Warabu, kwa hivyo wao hawamkubali.
Hapa Mwenyeezi Mungu
anawauliza kutokana na maneno yao kuwa “Je nyinyi mnajua zaidi au
Mwenyeezi Mungu ndiye mjuzi”? Na wakati huo huo Mwenyeezi Mungu katoa onyo
kwa kusema ni nani mwenye kudhulumu zaidi kuliko yule aliyeficha ushahidi
alionao utokao kwa Mwenyeezi Mungu? Na Mwenyeezi Mungu sio mwenye
kughafilika kwa hayo wanayoyafanya. Yeye anajua kila kitu, na atawalipa
wanaompinga na kumuasi, kwani yeye haghafiliki wala hasau yanaotendeka.
ÇáøóÐöíäó ÂÊóíúäóÇåõãõ ÇáúßöÊóÇÈó íóÚúÑöÝõæäóåõ ßóãóÇ
íóÚúÑöÝõæäó ÃóÈúäóÇÁåõãú æóÅöäøó ÝóÑöíÞÇð ãøöäúåõãú áóíóßúÊõãõæäó ÇáúÍóÞøó
æóåõãú íóÚúáóãõæäó
Wale tuliowapa
kitabu wanayajua haya kama wanavyowajua watoto wao, na kuna kikundi katika
wao huificha haki na hali wanajua.
Al Baqara-146
Maelezo zaidi
Hapa inaonesha wazi
kabisa kuwa yote yaliokuja ya haki wanayajua uzuri Mayahudi na Manasara,
wanamjua Mungu wa haki, wanajua Qur’ani ni kitabu cha haki, wanajua
Muhammad (SAW) ni Mtume wa haki, na wanajua kibla wanachoelekea
Waislamu (Al Kaaba) kumuabudu Mola wako ni cha haki, ni moja katika
vilivyotajwa katika vitabu vyao.
Baada ya Mtume
Muhammad (SAW) kuteremshiwa ujumbe wa kuelekea Al Kaaba wakati wa kusali,
badala ya kuelekea Baitul Muqaddas, Mayahudi na Manasara walikasirika na
kupendelea Waislamu waelekee huko wanakoelekea wao. Ijapokuwa wanajua na
imetajwa katika vitabu vyao kuwa wataelekea Kibla cha Maka, lakini
walijifanya kama hawafahamu, na ndio hapo Mwenyeezi Mungu anawafedhehesha
kwa kusema kuwa wanayajua hayo yote kama wanavyowajua watoto wao.
Þõáú íóÇ ÃóíøõåóÇ ÇáäøóÇÓõ Åöäøöí ÑóÓõæáõ Çááøåö Åöáóíúßõãú
ÌóãöíÚðÇ ÇáøóÐöí áóåõ ãõáúßõ ÇáÓøóãóÇæóÇÊö æóÇáÃóÑúÖö áÇ ÅöáóÜåó ÅöáÇøó
åõæó íõÍúíöÜí æóíõãöíÊõ ÝóÂãöäõæÇú ÈöÇááøåö æóÑóÓõæáöåö ÇáäøóÈöíøö
ÇáÃõãøöíøö ÇáøóÐöí íõÄúãöäõ ÈöÇááøåö æóßóáöãóÇÊöåö æóÇÊøóÈöÚõæåõ
áóÚóáøóßõãú ÊóåúÊóÏõæäó
Sema: Enyi watu!
Hakika mimi ni Mtume kwenu nyinyi nyote, niliyetumwa na Mwenyeezi Mungu,
Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi. Hapana Mungu ila yeye anayehuisha na
anayefisha. Basi muaminini Mwenyeezi Mungu na Mtume wake asiyejua kusoma
na kuandika, ambaye anamuamini Mwenyeezi Mungu na meneno yake. Na mfuateni
yeye ili mpate kuongoka.
Al A’raaf-158
Maelezo zaidi
Hapa kwanza
mwenyeezi Mungu anamuamrisha Mtume Muhammad (SAW) kuwa awaambie na
kuwafahamisha watu kuwa yeye ni Mtume wa wote, yaani Mtume wa Waarabu,
Mayahudi, Manasara na wengineo wote, ni Mtume wa ulimwengu wote. Yaani
inamaanisha kuwa hakuna kufuata kitabu cha uwongofu isipokuwa Qur’ani tu,
na kumfuata Mtume wa mwisho tu.
Mtume huyo na kitabu
hicho kimeteremshwa na Mfalme wa mbingu na ardhi, mwenye kuhuisha viumbe
na mwenye kufisha. Basi tunatakiwa tumuamini yeye Mwenyeezi Mungu na Mtume
wake asiyejua kusoma wala kuandika, ambaye yeye anamuamini Mwenyeezi Mungu
na maneno yake (Qur’an) Vipi leo watu wamesoma wanaandika na wanayafahamu
yote hayo na hawataki kufuata haki? Mola wetu anatuamrisha tumfuate yeye
Muhammad ili tupate kuongoka, kufaidika na kufanikiwa duniani na Akhera.
Matatizo ya kutoufahamu Uislamu
Baadhi ya watu hasa wale wasiokuwa Waislamu ambao hawaufahamu Uislamu, kwa
hivyo wanachukulia kuwa hii ni dini ya vikwazo vinavyowazuilia watu uhuru
wa maisha yao, au ni dini ya watu waliokuwa hawajaendelea kimaisha, au ni
maadui wanaotaka kuangusha dini nyangine na kuifanya dini ya Kiislamu kuwa
ndio bora kuliko dini nyengine zote.
Ni kweli kabisa dini hii ni bora na ndio inayotakiwa kufuatwa na wote. Na
inajuulikana wazi kabisa kuwa dini zilizopita mikono ya viumbe imekwisha
badilisha maneno ya Allah kwa kuyapunguza na kwa kuyaengeza, na ndio
sababu ya kuja kitabu kipya na Mtume mpya. Ndugu zangu tukipenda au
tukichukia ndivyo hivyo hivyo hakuna jengine jipya. Ikiwa watu hawataki
kuongoka na kukubali ukweli, basi wajuwe kuwa watu wanasonga mbele kufuata
nuru ya uwongofu na wapinzani wanabakia kizani kufuata njia zao za
upotofu.
Upotofu unatokana na mambo mawili, kwanza ni kutoufahamu nini Uislamu na
wengine kutotaka kuufahamu Uislamu. Jambo la pili ni kuwa wapo vile vile
wanaoufahamu Uislamu nje na ndani, lakini wanafanya vitimbi vyao. Kwa
hivyo wanafanya mambo ya maslaha ya kidunia ambayo matokeo yake ni kujenga
ukuta wa chuki na upotofu, na madhara makubwa ni kuwa viumbe wanajipotowa
na wanawapoteza wenzao.
Na kwa wale waliokuwa si Waislamu ambao hawakupata fursa ya mafahamisho
ya kweli na kuufahamu ukweli huu wa dini hii ya huyo huyo Mungu mmoja
anayeabudiwa na wote, basi inakuwa ni vigumu kwao kuujua ukweli na
wanatishwa na maadui wa Uislamu na kutiwa chuki hata kufikia hadi kuhisi
kusalimiana na ndugu zao, jirani zao waliokuwa Waislamu inakuwa kwao ni
jambo zito lisilokuwa na budi.
Kwa hivyo madhumuni ni kujaribu kuelezana mambo kwa mpango maalumu ili
wale waliokuwa si Waislamu waweze kuujua na kuufahamu Uislamu kwa hoja na
majadiliano ya kiakili kwa kusoma yaliokuwa muhimu kuyajua na kuyazingatia
ili waweze kuyapima na kuyakubali kwa imani yao, na kwa uhuru wa nafsi zao.
Katika Uislamu hakuna kulazimishwa mtu kujisalimisha nafsi yake kwa Mola
wake, bali ni hiyari ya nafsi ya kujitoa kwenye kiza cha upotofu na
kujiingiza kwenye nuru ya uwongofu.
Kwa hivyo iwapo kutakuwa na mafahamisho ya busara, na maelekezo yenye
msingi madhubuti, wengi waliokuwa si Waislamu wanaojihurumia nafsi zao kwa
kutaka kufuata haki na kujiepusha na matatizo ya duniani na Akhera,
utawakuta wanajisalimisha kwa Mola wao, kwa sababu wamekwishaona nuru ya
ukweli na utamu wa uwongofu wa kufuata haki.
Na wapo wale Waislamu ambao hawaufahamu udani wa Uislamu, ambao vile vile
wakipata maelekezo mazuri hubadilika na kuwa wenye kutimiza walioamrishwa
na kuwacha waliokatazwa, na kujitoa katika ghadhabu za Mwenyeezi Mungu na
kujiweka katika kundi la vipenzi vya Mola wao.
Na wapo Waislamu wenye maradhi ya kutoufuata Uislamu kama unavyotakiwa,
baadhi yao utawaona kuwa wanachaguwa yenye maslaha ya kidunia kuyafuata na
kuyatilia mkazo, na yenye kuzuia raha na matamanio ya kimaisha hupingwa na
kutofuatwa. Na matokeo yake ni imani hutoweka, maasi huzidi, na upotofu
unapata nguvu na umma unaagamia.
Ikiwa kupinga amri za viumbe wenzetu ni makosa na tunaogopa, vipi leo
tunampinga yule ambaye ametuumba, ametuleta duniani na kuturuzuku kwa
neema na rehma za kila namna, na ambaye anatulea na mwishowe marejeo yetu
yatakuwa kwake na tutahisabiwa kwa yote tuliyoyafanya, ikiwa mazuri au
mabaya. Kwa hivyo tutasema nini tutakapo simamishwa mbele ya haki?
Tutasema hatujui, hatukufundishwa au tumeghafilika? Sababu zote hizo
hazikubaliki.
Jukumu la kuamrishana mema na kukatazana mabaya.
Waliojisalimisha nafsi zao kwa Mwenyeezi Mungu (Waumini) huongozana na
huamrisha mema an hukataza maovu. Huu ni wajibu na ni jukumu la kila mmoja
wetu kutumia njia zozote zile zinazoweza kutumika ili kuweza kuufikisha
ujumbe na kufikia lengo la kuunyanyuwa Uislamu kwa kuilimishana na
kukataza maovu, na kujiadilisha katika kutii amri za Mola wetu.
Kwani Mwenyeezi Mungu kishatuahidi na keshaandaa Pepo nzuri zenye
mabustani yenye kupita mito ndani yake kwa wale waja wake wema, waliofuata
aliyowaamrisha na wakaacha waliokatazwa.
æóÇáúãõÄúãöäõæäó æóÇáúãõÄúãöäóÇÊõ ÈóÚúÖõåõãú ÃóæúáöíóÇÁ
ÈóÚúÖò íóÃúãõÑõæäó ÈöÇáúãóÚúÑõæÝö æóíóäúåóæúäó Úóäö ÇáúãõäßóÑö
æóíõÞöíãõæäó ÇáÕøóáÇóÉó æóíõÄúÊõæäó ÇáÒøóßóÇÉó æóíõØöíÚõæäó Çááøåó
æóÑóÓõæáóåõ ÃõæúáóÜÆößó ÓóíóÑúÍóãõåõãõ Çááøåõ Åöäøó Çááøåó ÚóÒöíÒñ Íóßöíãñ
æóÚóÏó Çááøåõ ÇáúãõÄúãöäöíäó æóÇáúãõÄúãöäóÇÊö ÌóäøóÇÊò ÊóÌúÑöí ãöä
ÊóÍúÊöåóÇ ÇáÃóäúåóÇÑõ ÎóÇáöÏöíäó ÝöíåóÇ æóãóÓóÇßöäó ØóíøöÈóÉð Ýöí ÌóäøóÇÊö
ÚóÏúäò æóÑöÖúæóÇäñ ãøöäó Çááøåö ÃóßúÈóÑõ Ðóáößó åõæó ÇáúÝóæúÒõ ÇáúÚóÙöíãõ
Na
Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi.
Huamrisha mema na hukataza maovu, na hushika salaa na hutoa zakaa, na
kumtii Mwenyeezi Mungu na Mtume wake. Hao Mwenyeezi Mungu atawarehemu.
Mwenyeezi Mungu amewaahidi Waumini wanaume na Waumini wanawake Bustani
zipitazo mito, wadume humo. Na makaazi mema katika bustani za kudumu, na
radhi za Mwenyeezi Mungu ndio kubwa kuliko yote. Huko ndiko kufuzu kukubwa.
At Tawba-71-72
Maelezo zaidi
Aya mbili za juu zinatuelezea kuhusu
tabia nzuri za waumini wanavyo katazana mabaya na kuamrishana mema, ambao
vile vile wanasimamisha Salaa na kutoa Zakaa, na wanamtii Mwenyeezi Mungu
na Mjumbe wake.
Mwenyeezi Mungu amechukua ahadi kwa
viumbe vyake kuwalipa rehma na kuwapa Pepo yenye mabustani mema, na
makaazi mazuri ya kudumu, yenye kila aina ya raha na furaha.
Tukizingatia kuhusu nguzo tano za
Uislamu, tutaona kuwa Salaa na Zakaa ndizo mguzo zilizotajwa zaidi katika
Qur’ani kwa mifano na mafahamisho, na vile vile Wajumbe na Mitume
waliopita waliamrishwa ibada hizi kuzisimamisha na kuzitimiliza.
Hapa tunapata dalili ya umuhimu wa
nguzo hizi, kwa wingi wa thawabu zake na kuwa ni sababu kubwa ya uwongofu
mzuri kwa Waislamu na utengezaji wa imani zao na hali ya maisha yao, iwapo
nguzo hizi zitatimizwa kwa ukweli, kwa ikhlasi na kwa unyenyekevu.
Tukiangalia njia kubwa ya kuchuma
thawabu ni Salaa, kwani kila siku tunasimamisha salaa tano za faridha (zilizotulazimu),
mbali salaa za sunna (nyengeza au ziada). Kwa hivyo hii ndio njia kubwa ya
kujipatia thawabu kwa kumtakasa na kumuomba Mola wetu katika kila siku.
Zakaa ndio njia ya pekee ya kuunyanyua
umma wa Kiislamu, na ndio njia ya kujipatia thawabu za kuendelea kwa
kutukuza wito wa Mola wetu na kuleta mapenzi na mahusiano mema kwa viumbe
waliojisalimisha nafsi zao kwa Mola wao mtukufu ‘Allah’.
Nini maana ya Uislamu?.
Uislamu ni masalimisho ya nafsi kwa kumkubali Mungu mmoja tu wa haki (Mwenyeezi
Mungu) na kufuata kanuni, nidhamu na sharia zake zilizokamilika na
zisizokuwa na shaka wala zisizohitajia kubadilishwa kwa kuongezwa au
kupunguzwa katika zama zote.
Sharia hizo tumeletewa sisi viumbe zituongoze na kutuelekeza katika njia
ya uwongofu, ili tupate amani kamili ya kiwiliwili na akili kwa
kujisalimisha nafsi zetu kwa Muumbaji mmoja tu wa kweli ‘Allah’ kwa
madhumuni ya kupata amani na raha za duniani na Akhera.
Kwani mafanikio mema hayo ya uwongofu ya duaniani ndio yatakaotupelekea
na kutuongoza katika njia ya kupata kulipwa na Mola wetu Pepo, Mabustani
yenye kila aina ya raha za maisha, huko kila tutakachokitamani tutakipata,
hakuna kuumwa wala kufa, hakuna shida wala taabu, ni raha za kudumu za
kuendelea moja kwa moja.
Sharia hizo zitokazo kwa Mwenyeezi Mungu zimetufikia kwa kupitia kwa
wajumbe wake. Kazileta kwa ajili ya kuwatoa viumbe vyake kutoka katika
upotovu na giza la ujinga na kuwaonesha mwangaza wa njia ya uwongofu.
Mwenyeezi Mungu hawezi kuleta Sharia zake kwetu moja kwa moja, bali
hutumia wajumbe wake (Malaika) kama Jibril ambaye huufikisha ujumbe huo
kwa Mtume wake, naye huwafikishia viumbe ujumbe huo na kuufahamisha na
kuuelekeza ili uweze kufahamika na kufuatwa.
Kanuni na sharia hizo hazikuletwa mara moja, yaani Qur’ani haikuteremshwa
yote mara mmoja, bali imeteremshwa kidogo kidogo kwa mujibu wa wakati wake
na sababu zake mpaka ikakamilika kwa muda wa miaka 23. Halafu akatuachia
viumbe vyake tuzifuate sharia hizo na kutuelekeza na kutupa mifano mbali
mbali kwa kutueleza nini raha za peponi kwa watakaofuata sharia zake, na
nini adhabu za motoni alizoziweka kwa waje wake watakaomuasi katika amri
zake.
Sasa tukizifuata hizi kanuni na sharia alizotuletea Mola wetu
tutafanikiwa hapa duniani, na mafanikio makubwa zaidi ya milele (ya kudumu)
yatakuwa huko akhera. Sasa tukimuasi Mola wetu kwa kutozifuata hizo kanuni
alizotuletea; basi huenda tukaanza kuadhibishwa hapa hapa duniani, na
adhabu kali zaidi zisizoweza kupigiwa mfano zitawakuta wapotofu siku ya
Akhera kwa wale waliokataa kufuata dini ya Mwenyeezi Mungu.
Jina la Uislamu ni tafauti kabisa na majina yanaotumika kwa kutaja dini
nyangine zilizopita ambazo majina yake yamebadilishwa na wafuasi wake na
kutumika kwa jina au muasisi wake au kabila au nchi wanayoishi kama vile
mfano Ukristo unatokana na Christ (Yesu), Buddism unatokana Budda.
Hinduism inatokana nchi au ardhi wanayoishi hao wafuasi, na Judaism
inatokana na jina la kabila judi. Lakini jina la Uislamu linatokana na
amani na salama kwa kujisalimisha kwa Mungu mmoja wa haki.
Ijapokuwa wamejaribu kuita Uislamu kwa jina la Muhammadanism, ili
waulinganishe na Christianity au Buddism, lakini hawakufaulu kwani
Muhammad ni Mjumbe tu, sio yeye muasisi wa Uislamu. Uislamu ni dini ya
Mwenyeezi Mungu na ni makosa kutumia jina hilo kwa kuita Uislamu au
wafuasi wa dini ya Uislamu.
Jee! Uislamu una mfumo wa pekee?
Bila shaka Uislamu una mfumo na nidhamu tafauti na nidhamu nyangine zote
za kidunia zikiwa za kidini, kisirikali, za kisiasa za kisayansi, za
kihistoria au za kibiashara. Na tafauti ya kwanza ni kuwa nidhamu za
Kiislamu zimepeya na ziko hai, na wala hazihitaji kubadilishwa cho chote
si herufu, si aya wala si sura. Kila zama zikipita nuru yake inachomoza
zaidi na kukubalika na kufahamika kwa uwazi zaidi.
Kitu cha pili kuwa nidhamu ya Uislamu inatumia katika Qur’ani mifano ya
maelekezo ya waliopita au vitendo vilivyopita, au matokeo na malipo ya
wafanyao mazuri (Pepo) na malipo ya wafanyao mabaya (moto) na kumfanya mtu
afikiri na kutumia akili yake kwa kuyakubali kwa uhuru wa nafsi yake,
kutokana na imani yake bila ya kushawishiwa au kulazimishwa kuamini kuwepo
kwa Mungu mmoja tu ‘Allah’
Jambo la tatu ni kuwa Uislamu unaridhisha akili ya viumbe kwa
kuwafundisha na kuwasomesha na kuwashajiisha kutafuta elimu ziada kwa
kuwapa au kutaja mifano katika Qur’ani ya mambo ya ilimu ya sayansi, ilimu
ya anga, ilimu ya maubile ya vitu na mengineyo. Uislamu haukuweka
vizingiti kwa kusema ukichunguwa mambo ya anga au bahari utakufuru au
kumshirikisha Mwenyeezi Mungu, bali watu wanashajiishwa kutafuta ilimu ili
wazidi kujua kuwepo kwa Muumbaji.
Jambo la nne ni kuwa Uislamu hautuzuilii au kutuwekea vikwazo katika
mambo ya kidunia, kama idadi ya kuowa, uwezo wa kumiliki mali, kuwa na
nyumba nzuri, kula chakula kizuri, bali imetuwekea mipaka, ulinzi na
nidhamu kwa ajili ya maslaha ya nafsi pamoja na jamii yote.
Jambo la tano ni Uislamu haumuongozi mtu au jamii peke yake, bali
uwongozi wake ni wa ulimwengu wote kwa jumla. Hautufundishi
kujishughulikia nafsi zetu tu bali unatuongoza kuwa wasaidizi na wema kwa
watu wote na kuwapa haki zao wote waliotuzunguka, wazee, ndugu, watoto,
mke, mume, jirani na hata mpita njia.
Nini maana ya Muislamu?.
Muislamu ni yule kiyumbe aliyejisalimisha nafsi yake kwa Mwenyeezi Mungu (Muumba
wa ulimwengu na vilivyokuwemo ndani yake) kwa kufuata aliyoamrishwa na
kuwacha aliyokatazwa.
Kujisalimisha ni kuwa cho chote unachokitenda basi unakitenda kwa ajili
ya Mola wako, yaani unakifanya kwa kutarajia thawabu. Na jambo lolote
linalokukabili katika mitihani ya kidunia, ama likiwa zuri basi wajibu
wako ushukuru, na ikiwa unalifikiria kuwa baya basi wajibu wako ustahamili
na Mungu wako umdhukuru. (umkumbuke) Mwenyeezi Mungu anajua kila kitu mja
wake anachokifanya, kikiwa cha siri au cha dhahiri. Kwa hivyo kila kiumbe
ana hisabu yake ya mazuri na mabaya anayoyafanya.
Utukufu wa kiumbe huyo aliyejisalimisha nafsi yake kwa Mola wake,
unatokana na uchamungu wake, hautokani na rangi yake, kabila yake,
uwananchi wake, utajiri wake, uzuri wake au cheo chake.
Åöäøó ÃóßúÑóãóßõãú ÚöäÏó Çááøóåö ÃóÊúÞóÇßõãú Åöäøó Çááøóåó Úóáöíãñ ÎóÈöíÑñ
Mwenyeezi Mungu anasema: “Hakika aliyemtukufu (bora) kati yenu
kwa Mwenyeezi Mungu ni huyo aliye mcha mungu zaidi katika nyinyi. Hakika
Mwenyeezi Mungu ni mwenye kujua (kila kitu), mwenye (ujuzi)
khabari ”.
Al Hujuraat-13
Kiumbe
yupi aliye bora?
Nini maana ya kafiri?.
Kafiri ni yule kiumbe aliyejitoa katika himaya ya Mwenyeezi Mungu, au
akakataa kuamini na kufuata sharia na kanuni za Mola wake. Akapinga
aliyoamrishwa, na akafanya aliyokatazwa na akawacha alioamrishwa.
Mwenyeezi Mungu ni Mungu wa viumbe vyote.
Tumeeleza mwanzo kuwa Mwenyeezi Mungu ndiye aliyeteremsha Mitume (Wajumbe)
na ndiye aliyeleta vitabu vya kufuatwa na viumbe vyake kwa madhumuni ya
kuwaongowa katika njia ya haki. Bila ya kuwa na sharia ya Mwenyeezi Mungu
na kuifuata, basi viumbe tutakuwa tunaishi maisha ya kinyama, yenye kila
aina ya mazonge na dhiki za kimaisha.
ÞõæáõæÇú
ÂãóäøóÇ ÈöÇááøåö æóãóÂ ÃõäÒöáó ÅöáóíúäóÇ æóãóÇ ÃõäÒöáó Åöáóì ÅöÈúÑóÇåöíãó
æóÅöÓúãóÇÚöíáó æóÅöÓúÍóÞó æóíóÚúÞõæÈó æóÇáÃÓúÈóÇØö æóãóÇ ÃõæÊöíó ãõæÓóì
æóÚöíÓóì æóãóÇ ÃõæÊöíó ÇáäøóÈöíøõæäó ãöä ÑøóÈøöåöãú áÇó äõÝóÑøöÞõ Èóíúäó
ÃóÍóÏò ãøöäúåõãú æóäóÍúäõ áóåõ ãõÓúáöãõæäó
Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyeezi Mungu na yale tulioteremshiwa sisi,
na yalioteremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is’hak na Yaakub na wajukuu
zake, na waliyopewa Musa na Isa, na pia waliyopewa Watume wengine kutoka
kwa Mola wao, hatutafautishi baina ya yoyote katika hao, na sisi
tumesilimu kwake.
Al Baqara-136
Maelezo zaidi
Hapa wanaambiwa waliojisalimisha kwa Mola wao (Waislamu) kuwa waambie wale
Mayahudi na manasara wanaokataa kumfuata Muhammad kwa alioletewa, kuwa
sisi tunamuamini Mwenyeezi Mungu na yale tulioteremshiwa kwa watume
waliopita. Na wala hatutafautishi yoyote kati ya Mitume hao, na sisi
tumemkubali Muhammad na tumesilimu.
Vitabu vya Mwenyeezi Mungu alivyoviteremsha.
Jumla ya vitabu vyote vilivyoteremshwa na Mwenyeezi Mungu kwa ajili ya
uwongofu wa waja wake kupitia kwa Wajumbe wake ni Mia moja na nne (104)
kama hivi ifuatavyo:
Vitabu 50 kwa Mtume Shaith (as)
Vitabu 30 kwa Mtume Idriis (as)
Vitabu 10 kwa Mtume Ibrahim (as) (Vitabu-Suhuf)
Vitabu 10 kwa Mtume Musa (as) (Suhuf kabla ya Taurat)
Kitabu 1 kwa Mtume Musa (as) Taurat
Kitabu 1 kwa Mtume Daud (as) Zabur
Kitabu 1 kwa Mtume Issa (as) Injiil
Kitabu 1 kwa Mtume Muhammad (SAW) Qur’ani
Watume waliotajwa katika Qur’ani (ishirini na tano)
1-Adam 2-Idris 3-Nuuh 4-Huud 5-Saleh
6-Ibrahim 7-Luut 8-Ismail 9-Is’haak 10-Yaakub
11-Yusuf 12-Shuayb 13-Ayyub 14-Dhul-kifl 15-Mussa
16-Harun 17-Daud 18-Suleiman 19-Ilyas 20-Ilyasaa
21-Yunus 22-Zakaria 23-Yahya 24-Issa 25-Muhammad
Kwanini kukawa na Mitume na vitabu zaidi ya kimoja?
Mwenyeezi Mungu kateremsha ujumbe katika zama mbali mbali na katika miji
mbali mbali, na uteremshaji uliendelea mpaka kufikia Mitume hii ya
mwishoni kama Mtume Musa, Mtume Issa na Mtume Muhammad.
Sababu kubwa ya kuteremshwa Mitume baada ya Mitume ni kuwa baada ya
kupita miaka mingi na kufa hii Mitume, yale yalioteremshwa yanakuwa
hayafuatwi tena na viumbe. Na kila miaka ikipita upotofu unakuwa unazidi
kupata nguvu. Kwa hivyo Mwenyeezi Mungu huleta Mjumbe mpya, na Ujumbe
mwengine kwa ajili ya kuwaokowa na kuwaongoza viumbe ili wafuate njia ya
haki.
Sasa tukitazama alipokuja Mtume Issa, ilikuwa viumbe wote waikubali na
kuifuata dini hii mpya, yaani mpaka Mayahudi waache kufuata Taurati na
wafuate Injiil, kwani kwa wakati ule ndio dini iliofuatia na imekuja na
maamrisho mapya. Na vile vile ilivyokuja Qur’ani ilikuwa wajibu dini za
nyuma ziwachwe na dini hii ya Uislamu ifuatwe na viumbe wote. Kwa kuwa
Mungu aliyeteremsha Zabur, Taurati, Injili na Qur’ani ni yule yule.
Kama tulivyoeleza mwanzo, kutokana na maslaha ya kidunia ya viongozi wa
dini hizo, huyakataa haya na kuhakikisha wafuasi wao wapo pamoja nao, ili
vyeo vyao na mapato yao yaweze kuendelea. Hata kufikia hadi kubadilisha
maelekezo ya Mola wao, na kuandika wanavyotaka wao, na kufuata mila na
utamaduni wao, badala ya kufuata maelekezo na maamrisho walioletewa na
Mola wao.
Huu ni upotofu mkubwa, na haya ni makosa makubwa ya kupinga maamrisho ya
haki, na kufuata matamanio ya nafsi. Tunamuomba Mola wetu awazidue na
kuwaongoza waliopotea uwajie muangaza na kuweza kuona nuru ya njia ya haki
waifuate na kuwa katika himaya ya Mwenyeezi Mungu duniani na Akhera, Amiin.
Viumbe tumepewa uhuru wa kufikiri na kuzingatia, kwa hivyo tuitumie hiyo
akili kwa kujiuliza nafsi zetu kuwa ikiwa mfano kuna mtungaji wa kitabu
anayesifika sana, ambaye kitabu chake hicho huwa anakisawazisha kila baada
ya miaka fulani na kuchapisha chapa mpya. Sasa ikiwa mtu anataka kununua
kitabu hicho, jee! Atanunua chapa za zamani au atanunua kitabu kilicho
chapishwa karibuni? Sote tutanunua chapa mpya kwa sababu itakuwa bora
kuliko chapa za zamani.
Sasa tukirejea tena Mungu anayeabudiwa ni yule yule mmoja kwa wote, na
vitabu alivyoviteremsha kwa waja wake ni yeye ndiye aliyevileta kwa
madhumini ya kuwaongowa viumbe vyake, kwa hivyo kitabu cha kufuatwa na
viumbe vyote ni kitabu cha mwisho (Qur’ani) ambacho kimechukuwa
yaliokuwamo katika vitabu vyote vilivyopita.
Tunajua kuwa Qur’ani ni kitabu cha mwisho, na wala hakuna kuja kwa Mtume
mwengine mpya, wala kuja kwa kitabu kipya. Lakini lau kama tumeletewa na
Mola wetu Mjumbe (Mtume) mpya na uwongozi mpya, basi ingelikuwa tuwache
vitabu vya Mungu vyote vilivyopita pamoja na Qur’ani na tufuate kitabu
chenye maamrisho mapya.
Hili ni jambo liko wazi, na linaingia akilini na kukubalika kwa kila
aliyekuwa anataka haki na ukweli, na anayeipenda nafsi yake kwa kuamini
kuwepo kwa Mungu mmoja, kwa hoja zote zilizowazi kabisa.
Ndugu msomaji, ikiwa wewe bado hujajisalimisha kwa Mola wako, basi
sikwambii silimu, lakini nakuomba usome zaidi na ujaribu kuuliza watu
wenye kufahamu dini uzuri zaidi, ili upate maelekezo mazuri na ya kweli
mpaka ukinai nafsi yako, na ujuwe cho chote unachokifanya, unakifanya kwa
sababu gani. Asikwambie mtu fuata tu, kwani kila ukijua sababu ndio
utafahamu zaidi na utayatekeleza kwa imani ya kweli.
Uislamu hakuna kuvungana kwa maneno, yote yanayofuatwa yana maelekezo na
yana sababu na misingi maalumu kwa nini yanafanywa. Na akikwambia mtu
fanya tu kama wanavyofanya wengine, basi jua yeye huyo haifahamu dini yake
uzuri, na tafuta mtu mwenye kufahamu akupe maelekezo zaidi.
Kiumbe akizaliwa na kuja duniani, anakuja katika hali ya kuwa yuko huru,
lakini akifika duniani anakumbana na mazonge ya kila namna ambayo
yanampelekea kupotea ikiwa hakupata maelekezo mema. Na upotofu huo
unatokana na mazingira aliyoinukia au anayoishi nayo.
Kutokana na maendeleo ya kidunia ambayo yanatumika vibaya kwa kukusudia
katika vyombo vya habari na mafundisho ya elimu na mambo mbali mbali ya
kimaisha, mara nyingi tunajikuta tumetekwa kiakili, kimawazo na kimaisha
na kuelekezwa katika njia ya upotofu na kuambiwa kuwa haya ndio maendeleo
na ndio njia ya pekee ya raha na mafanikio ya maisha.
Njia pekee ya uwongofu katika maisha ya kiumbe ni kushikamana na
maamrisho ya dini ya haki, yanayotokana na Mungu wa haki anayestahiki peke
yake kuabudiwa na kutegemewa na viumbe vyake vyote. Na kwa lolote jengine
tunalolifanya la kimaisha tunatakiwa tuliambatanishe na kulilinganisha na
maelekezo kutoka kwa Mwenyeezi Mungu.
Kwa nini wakaumbwa Malaika, Binaadamu na Majini?
Mwenyeezi Mungu kaumba malaika ambao si katika jinsi ya Binaadamu wala
Majini. Viumbe hawa hawamuasi Mola wao kwa wanayoamrishwa, wao hawali wala
hawanywi, wala hawana sifa za uke (usichana)wala sifa za uume (uvulana).
Wameumbwa kwa ajili ya kuabudu na kutekeleza amri za Mola wao.
Binaadaamu na majini wameumbwa vile vile kwa ajili ya kumuabudu Mwenyeezi
Mungu mmoja, hatukuletwa duniani kwa ajili ya kuja kutafuta mali, utawala
na raha za kidunia. Mambo ya kidunia yote unaruhusiwa kuwa nayo na
kumiliki kila unachoweza kuwanacho katika sharia na mipaka yake. Lakini
ibada ndio msingi na madhumuni ya kuletwa duniani.
Kwa hivyo kiakili ikiwa tumeumbwa na kuletwa duniani ili kwa ajili ya
kumuabudu Mwenyeezi Mungu, basi tunavyotakiwa katika masaa 24 ya kila siku
inatuwajibikia kuyatumia zaidi ya nusu ya masaa hayo katika kufanya ibada.
Ndio maana Mola wetu alituamrisha kwanza kusali salaa 50 katika kila siku
moja, halafu tukapunguziwa na kupunguziwa mpaka zikafika salaa 5 tu.
Lakini malipo ya salaa hizo tano tunalipwa sawa na salaa 50 kwa rehma na
kwa mapenzi ya Mola wetu. Hii ndio dalili ya kuwa Mola wetu katuumba na
kutuleta duani ili tuje kumuabudu. Na ibada sio salaa tu, kuna kufunga,
kuna kuhiji, kuna kutowa zakaa na mengineyo.
Sasa hebu tufikirini kama ndio ingekuwa tumeachiwa na zile salaa 50
kuzisali kila siku, basi kwa uchache tungelikuwa tunasali salaa 2 katika
kila saa mmoja si usiku si mchana. Sasa kungelikuwa na uwezo wa kuendelea
kulala masaa 8 mfululizo na kufanya kazi masaa 8, na kupumzika masaa 8
katika siku mmoja ya masaa 24? Wengi wetu tungeshindwa kuyatimiza kama
yanavyotakiwa. Tumeamrishwa salaa 5 na bado kuna watu wanashindwa
kuzitimiza, ewe kiumbe unataka nini zaidi ufanyiwe?
Kwa hivyo ibada hapa inakusanya mambo yote ya kheri ikiwa kusali,
kutafuta rizki ya halali, kufunga, kuhiji, kutoa zaka, kumdhukuru (kumtaja)
Mola wako, kusomesha na kuelimisha wenzio, kuupigania Uislamu kwa hali na
mali na mengineyo yote ya kheri basi ni ibada.
æóãóÇ ÎóáóÞúÊõ ÇáúÌöäøó æóÇáúÅöäÓó ÅöáøóÇ áöíóÚúÈõÏõæäö
ãóÇ
ÃõÑöíÏõ ãöäúåõã ãøöä ÑøöÒúÞò æóãóÇ ÃõÑöíÏõ Ãóä íõØúÚöãõæäö
Åöäøó
Çááøóåó åõæó ÇáÑøóÒøóÇÞõ Ðõæ ÇáúÞõæøóÉö ÇáúãóÊöíäõ
Nami sikuwaumba Majini na Watu ila (isipokuwa) waniabudu mimi.
Na sitaki kwao rizki, wala sitaki wanilishe. Hakika Mwenyeezi Mungu ndiye
mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu madhubuti.
Adh-dhaariyaat-56-58
Maelezo zaidi
Hapa tukizingatia tutaona kuwa Mwenyeezi Mungu hakutuumba ila kwa ajili ya
kumuabudu. Na tukimuabudu basi yeye hanufaiki na kitu, tunamuabudu ili
sisi tupate faida na manufaa kutoka kwake kwa kutulipa aliyotuahidi viumbe
vyake.
Kwa hivyo Mwenyeezi Mungu hataki kitu cho chote kwetu wala si muhitaji wa
jambo lo lote, bali anataka tumuabudu kwa kuwa yeye ndiye mwenye kutulisha,
kuturuzuku, kutuhami na kutuongoza. Na anataka tuchume thawabu wenyewe
kutokana na mambo ya kheri aliyotuamrisha ili atupe Pepo aliyotuahidi
viumbe vyake.
Sasa kama tunavyojua kuwa Binaadamu na
Majini wameumbwa kwa ajili ya kumuabudu Mwenyeezi Mungu. Na hilo ndio
lengo la Mola wetu, kwa hivyo jee! ndugu zangu tunalitimiza lengo hilo?
Na ikiwa hatukulitimiza na kulikamilisha, basi tujuwe kuwa kuna moto mkali
wa jahannam unatungojea. Ni wajibu kufikiri kwa makadirio ya moto wa
duniani (tunaoutumia) ukitupata kidogo tunaruka na kupaparika, roho mbichi
inataka kututoka. Jee! Moto huo ambao umefanywa khasa kwa ajili ya
kuwatesa waasi, ukali wake utakuwa hali gani?
Muandishi:
Ali S. Al Harrassy © asharasy@omantel.net.om
|