View Single Post
  #2 (permalink)  
Old 08-02-10,
Abukhalil's Avatar
Abukhalil Abukhalil is offline
Msimamizi wa Masuala ya Dini
 
Join Date: 07-09-04
Posts: 1,202
Default

Waalaykum Salaam warahmatu-LLahi wabarakaatuh

Jawabu:

Kwa mujibu wa wenye ilmu, utumiaji wa maji ya kisima kilichomo/kilichochimbwa katika shamba lilonyan'ganywa si haramu kwa asiyechukua/asiyenyan'ganya ardhi hiyo; kwani maji ya kisima hayamilikiwi na mtu; bali mwenye kisima anamiliki shimo lenyewe tu likiwa katika ardhi yake.

Dalili ya hayo ni kauli ya Mtume -rehma za Allah na amani zimshukie- "Waislamu ni washirika katika matatu: maji, nyasi, na moto"; imepokewa na Abu Daud, Ahmad, Ibnu Majah na wengine. Wa'LLahu A'lam.

Abukhalil.
Reply With Quote