PDA

View Full Version : MishonoBanour
28-09-04,
Aaww
Here By Are Some Designs You Might Like
Regards Banour

Uislam
28-09-04,
Assalam Alaykum Warahmatullah..

ndugu Banour ..asante sana kwa makala zako, na jitihada zako..Lakini tu kuna jambo moja..kuhusu hii mishono jee unahisi itawasitiri wanawake wa kiislam, maana lengo letu kubwa ni kumuonesha mwanamke vazi na heshima pamoja na hijabu. Nadhani iko mishono mingi ambayo unaweza kutusaidia na kutuonesha..

Samahani usifahamu vibaya, lakini tujitahidini sote ili tuoneshe mavazi mema..
shukran sana..

istiqama
29-09-04,
Ndugu Banour
Mishono hiyo unawataka wanake wa Kiislamu kuzivaa? ikiwa jawabu ndiyo basi sasa tunaanza kuipinga amry ya Allah na ikabu yake sio ndogo kama hatukujiwahi haraka sana kwa kutubu.
Tunakuomba ndugu Banour uwaoneshe wenzako mishoni ya sitara ili Allah awe radhi na wewe kwani kuipinga amri yake kama alivoileta katika Quraan basi itakuwa khatari kubwa sana.
Samahani lakini wajibu wetu kukubushana.

Banour
02-10-04,
AAWW
Their is nothing wrong with the mishono
if you knwo how to stich them, you should make
long hands cover the chest, long dress, and ofcause
hijab, you only take the good part and leave the bad.

This is how we atain knowledge also, when we travel to
a foreign country we try and acquire the good and
leave the evil and bad. By me posting these designs
does not mean that i want you ladies to dress like this,
common lets use our brains, even when you go to the
tailor you look at the mishono books then you select
what you want to stich right :) so those books are even worst
how come no complains in the tailoring shop.

Regards Banour

Abu-Muslim
05-10-04,
Asalaam alaykum
Ndugu yangu Banoor nakushauri ikiwa nimekosea nambie.Kwa fikra zangu mimi hii mishono (design)ndio inayopelekea mwanamke wa kiislamu kujivua mabuibui na majilbabu yake kwasababu ya kutaka kuonesha jinsi gani kapendeza.Amini usiamini hio ni 100% ni kweli kabisa.Maumbile ya mwanamke ni mtu anayependa kusifiwa na kuonekana mzuri wakati wote.Kwa hio anapoona mishono mbali mbali hutaka kushona ili aonekane mzuri na kusifiwa.Sasa hii kusifiwa huanzia nyumbani kwake baadae huona haitoshi na fulani aone,na fulani na fulani,mpaka inafika hadi huwa hataki tena kuvaa buibui wala jilbabu ili watu wote kwa ujumla wapate kuona na sifa kuwa nyingi kwamba fulani mzuri na kavaa uzuri.Mimi nakwambia ukitaka usitake hii mishono ni fitna tena kubwa sana dhidi Muislamu na waislamu kwa ujumla.Hapo zamani wake za Mtume (s.a.w) na wanawake wema wa wakati huo walikuwa hawana mishono wala nini.Kulikuwa hakuna fitna hizi kabisa wanawake wakijisitiri sawa sawa leo hii yamekuja mambo haya bala tupu,kila mwanamke anataka kubadili nguo kama siku zinavyobadilika.
Ikiwa mwanamke atajistiri kwa mabuibui na majilbabu sawa sawa basi amini usiamini hutosikia tena mshono huu wala mshono ule.

Wabillahi tawfiq.

Akhuukum,

Abu-Muslim.

Banour
05-10-04,
AAWW
WE are living in a world full of fitna,and alot of examinations.
We all want to show of what we wear, what big house we have
what job one has and many more. WE should tell eachother that
no matter what we have Allah will account our intentions, did we
share, did we take care of the poor, bla bla and much more.

Now, we should encourage eachother in this forum, for woman
to dress in those mishono but in a proper manner which does not
show her aura, and her intention should be pure for herself not
to show off, and also she should wear these cloths for her husband
not a must in weddings, parties whatsover. These issues are
strongly encouraged, we should not avoid them in the right places, and right manner.

I can tell you alot of ladies dont wear their gold, beutiful dresses, makeup, eyeshadows unless they go for weddings to show of, so why dont we transform ourselves to do these things at home, as we can dress no matter
how we want infront of out husbands no limitations.

So when i uploaded these designs it is up to you where you are going to
wear it, my intention was clean, to dress for yourself in the right way.

regards hajer

Uislam
05-10-04,
Jamani kiswahile weee.... hatufahamu kizungu mwatuwacha kwenye mataa, tunataka kuelimika lakini sio kwa ki china...aaa nakusudia kizungu..

au mutufasirie kwa kiswahili...

shukuran

arfy_ahmed
05-10-04,
Ndugu Waislamu,
AAWW.
Mimi napenda kuchangia kuhusu mada hii kuhusu MISHONO. Hakika mimi sioni kuwa mwanamke aliyekwisha olewa akishona nguo ambayo ina mishono mbali mbali haifai. Hapa huenda kuwa sisi tumemfahamu vibaya Banour alipotia picha hizo katika ukumbi huu, huenda kuwa yeye anamategemeo kuwa ukumbi huu hawaingii ispokuwa w/wake na hamna mwanamume anaweza kuingia katika ukumbi huu. Mimi ushauri wangu ni kuwa ikiwa tunataka kuonyesha wanawake wenzetu mishono basi ni bora tutafute picha zenye sitara ili tuepushe wanaume kutizama yaliokuwa haramu kuyatizama. Ama kusema kuwa mwanamke akivaa nguo za mishono atakuwa anajionesha mbele za watu mavazi hayo, hii ni tabia mbovu za wanawake hao ama mwanamke mwenye heshima yake atavaa kivazi hicho mbele ya mumewe tu na kuonyesha maringo yake mbele ya mume huyo. Mimi nakataa kabisa kusema kuwa hii mishono ni sababu ya waislamu kuharibika. Hakika waislamu wameharibika baada ya waislamu khasa wanaume kuacha kamba waliopewa na ALLAH waikamate, hapa tukaanza kuhalalisha haramu na kuharamisha halali. Hakika ukisoma histori utaona kuwa wanawake wa zamani walikuwa wakijuwa kujipamba mbele ya waume zao, mpaka mmoja katika masahaba akasema hakika mimi napenda nimpambie mke wangu kama mimi ninavyo penda yeye anipambie.
Kwa ufupi tusiharamishe vitu ambavyo ni halali kwa ajili labda njia ya kuweka picha hizo katika kumbi hii ilikuwa si kwa kukusudia vibaya.

Wito huu nautoa kwa wanawake wakiislamu, ni wajibu kwenu kujipamba mbele za waume zenu na ni haramu kwenu kuonyesha mapambo yenu mbele ya wanaume wageni juu yenu, kwani siku hizi utasikia wanaume wanasema usiowe mwanamke aliyekamata dini kwani hawajui kujipamba na kujitizama. Hakika fikra hii ni potovu kwani inatakikana wanawake waliokamata dini wawe msitari wa mbele katika kujipamba mbel za waume zao na si kunuka harufu za vitunguu na kuvaa maguo mapana majumbani kisha mume huyo akitoka nnje anadanganyika akiona mwanamke amevaa nguo inayobana mwili.
WALLAHU AALAM.

Sheikh wangu nimekufahamu vema kabisa.Niliposema kusifiwa mwanamke huanzia nyumbani nilikusudia hivo kwamba mapambo yanavaliwa ndani, sikatai hilo lakini baadae hutaka kuoneshwa na wengine pia,kwani hujui shetani anavyotembea ndani ya mwili wa binadamu? jambo la halali atafanya kila njia kuligeuza kuwa la haramu.Shaitani akitaka kukuingia hakujii direct anakujia indirect bila kukushtua ukitahamaki wapii......kisha kuvaa.Kuna nguo za kuvaa chumbani,ukumbini na jikoni.Hapa lazima paeleweke.Inaposemwa kwamba mke umuoneshe mume mapambo na uzuri wake ieleweke kwamba ni nguo gani za kuvaa na pahala gani,sio nguo ya jikoni kuvaliwa chumbani na ya chumbani kuvakiwa ukumbini.Kwa mfano mdogo tu,hiyo mishono inayosemwa mishono inaingia akili mtu kuvaa mbele ya baba,ndugu,watoto na wazee wake?
Hapa watu wanakipengele kimoja kwamba madamu nguo inafunika mwili wote basi ndio sitara,kasema nani.Hicho ni kisingizo tu cha kuhalalisha yao.Hio mishono mingi ni ile ambayo ya kubana mwili na kuonesha figure yote ya m/mke.Kama ikiwa si ya kubana mwili hakuna atayepinga kwa hilo.Kwa mtu mwenye heshima zake hawezi kuvaa nguo kama hizo hata mbele ya mwanawe.Kama kuvaa hivo basi avae chumbani na mumewe sio pahala popote.

Wabillahi tawfiq.

Akhuukum,

Abu-Muslim.

abunooh
11-10-04,
Ndugu waislam,

Tufahamu kitu kimoja kuwa maovu katika maisha yetu ni mengi,hayahesabiki. Lakini kusema kuwa tuchukuwe mazuri na tuache maovu,sifikirii kuwa tunaweza.
Lakufanywa ni kukumbuka kuwa ALLAAH ametunabihisha kutoka hapo kale kuwa mayahudi na manasara hawatoridhika na sisi hadi tufate mila zao.
Mwanamme aliemsifu ALLAAH katika Qur-aan sie yule apendae ashonewe pasua nijabe wala popo bawa, bali ni yule anaejua pahala pa mwanamke katika uislam na haki zake.
Pelelezeni aghlabia ya wanaume wakitaka kuchakuwa mchumba huwa wanatafuta wale wanavaa kiheshima na hata wakisha kuoa pia huwaamrisha wake zao kuwa vazi lao liwe jilbaab.
Na kueleza mapenzi yangu mimi, nikivaliwa jilbaab na mama watoto basi huwa na hisia nzuri sana moyoni mwangu na husema moyoni mwangu Alhamdu Lillahi alieniruzuku mke, sio balaa.
Dada Banour, mwanamke anapovaa mishono ya kisasa (aliofundishwa na adui wa uislam) basi ikiwa ni kigori,ameolewa au hata kizee, basi njiani huwa ni balaa tu.Hapo huwa mtihani mkubwa kwetu sisi wanaume(nas alu LLAAHA l-afu wal-aafia) na tunapomuona alievaa lile vazi la kiislaam basi nafikiri mwanamme atakaye shangiria katika mada hii baada yangu ataelezea zaidi vipi sisi huwa tunamueka katika kundi la waheshimiwa mwanamke huyo.

Nikiendelea kuandika nitachokesha wasomaji lakini kwa ufupi hayo makatalogi ni mbinu za maadui kututoa katika mila za kiisilamu.

Wassalaam Khitaam,

Abu Nooh.