PDA

View Full Version : Utabiri Wa NdotoAbu-Muslim
04-08-08,
Asalaam alaikum,
Sheikh nimewahi kusikia na kuona kwenye baadhi ya vitabu na internet kuwa kuna utabiri wa ndoto,yaani mtu akiota huenda kwa mtu fulani au kwenye kitabu au internet kuiangalia maana ya ndoto yake.
Suala jee inafaa kufanya hivi?
Na ni kweli utabiri huu au la?
Kama inafaa na ni kweli,basi ni nani mwenye elimu ya kutabiri ndoto,ni mtu yeyote au mtu mwenye elimu gani?

Wabillahi at tawfiq.

Akhuukum,

Abu-Muslim

Uislam
12-08-08,
Assalam Aleykum Warahmatullahi Wabarakatuhu

Ndugu yangu suala la kufasiri ndoto ni moja katika masuala muhimu.

Naam mtu anaweza kuota ndoto katika usingizi wake, na ikawa na maana Fulani ambayo yeye mwenyewe huwenda akafahamu, mithali kuna watu walikua katika maasi ya mwendo mbaya, basi Mwenyezi Mungu akawaotesha ndoto ambayo ikawa ni funzo kwao na njia ya kujisawazisha katika maisha yao.

Ama kuna ndoto nyengine hutakiwa Watu ambao Mwenyezi Mungu kawapa kipaji na neema ya elimu hii ya kufasiri ndoto. Na si kila mtu anaweza kufasiri ndoto.

Ama njia ya internet na vitabuni huwa ni ufasiri wa ndoto kwa ujumla ya maana ya ndoto yenyewe sa lazima mtu aote ndoto kisha maana yake iwe sawa sawa na iliyotajwa katika internet au kitabu.

Wallahu Aalam

webmaster

rashid43
12-08-08,
Assalaamu Alaykum Ndugu Abu-Muslim,

Tunakukaribisha katika mtandao wa Sekenke.com kuna ndoto nyingi sana (540) zimefasiriwa na tofauti labda utapata ndoto ambayo unayoitafuta. Katika ukumbi wa: TAFSIRI ZA NDOTO.