Kuna msemo unaobainisha ya kuwa watu hawapimwi kwa rangi au mali au kabila zao nao ni huo ufatao :-

" "
( Si kila kinachongaa ni dhahabu)
Si uzuri wa sura tu. Sio kila kingaacho ni dhahabu. Na shaba hungaa isije kukughilibu.
Sasa nitakuleteeni baadhi ya hizo Hadithi nyingi za Mtume (S.A.W.) alizotusisitiza kuchagua mchumba mwenye sifa za kidini na sio mwenye sifa za pambo na uzuri wa kidunia kama anavyotaka bilisi.
Hadithi ya kwanza ni hii:
" : ( ) "
Imepokelewa kutokana na Abdullah bin Amru bin Al-Aas (R.A.A.) kuwa Mtume (S.A.W.) kasema Dunia ni pahala pa srarehe ndogo tu, na bora za starehe zake ni mke mwema (yaani mwenye kushika dini). Ameitoa Muslim.

Hadithi ya pili ni hii:
" : ) .
Na imepokelewa kutoka kwa Ibnu Abbas (R.A.A.) ya kuwa Mtume (S.A.W.) alimuambia Omar (R.A.A.) (Nikuambie jambo bora ambalo mtu analienzi ni: Mke mwema, ukimtazama anakufurahisha na ukimuamrisha jambo anakutii na ukiondoka anakulindia.) (kila chako na sharaf yako)Ameitoa Abu Dawuud.

Hadithi ya tatu ni hii:
: ( - - 0000)

Imepokelewa kutoka kwa Saad bin Abi Waqaas (R.A.A) alisema kuwa kasema Mtume (S.A.W) (Mambo manne ni katika mambo ya raha kati ya hayo ni mke mwema..)
Hadithi ya nne ni:
: : -

Imepokelewa kutokana na Anas bin Maalik (R.A.A.) kuwa Mtume (S.A.W.) kasema: (Mwenye kuruzuqiwa na ALLAAH subhaanahu wa taala ,mke mwema, basi huwa amesha saidiwa nusu ya dini yake, basi na amche Mwenyezi Mungu katika nusu ya pili.).
Na ziko Hadithi nyingi nyenginezo ambazo Mtume ( S.A.W.) ametuusia juu ya mke mwema.
Sasa tumeshaona kuwa bilisi anatuvutia tutafute mke mwenye uzuri wa kidunia na Mtume (S.A.W.) anatunasihi tena na tena tutafute mke mwema, mwenye uzuri wa Dunia na Akhera, jee sasa tutamfuata Mtume (S.A.W.) au tutamfuata bilisi (Laana za ALLAAH subhaanahu wa taala zimshukie)?
Wataalamu wengi wameona kuwa malezi ya mtoto mengi yanatokana na mama na ndio wataalamu wa leo wakasema:
(If you educate a woman you educate a family but if you educate a man you educate an individual).
Ukimsomesha mwanamke umesomesha ukoo mzima lakini ukimsomesha mwanamme umesomesha mtu mmoja tu. Wataalamu hao wanasema kuwa mara nyingi mtoto anachukuwa khulqa na tabia zinazotokea umamani kwake (yaani kutoka kwa mama mwenyewe na kutoka katika aila ya mama). Hayo wataalamu hao wameiga tu kusema hivyo. Kwani Mtume wetu (S.A.W.) katuambia katika tokea karne kumi na tano nyuma. Hadithi ifuatayo:
###########################################
" ( ) ( 0 )"
"Imepokewa na Ibnu Aadi na Ibnu Asaakir kutokana na Bibi Aisha (R.A.A) (Chagueni pakueka kizazi chenu, kwani wanawake huzaa watoto wanao shabihi upande wao, na upande wa ndugu zao wa kiume na kike) Na Hadithi nyengine inasema chagueni pakuweka kizazi chenu kwani kikitokea kizazi cha kiume huenda kikafuata kwa wajomba."
Kwa hivyo chagueni wale ambao watoto wenu wakifanana nao mutaridhika. Na hii ni kweli kabisa mukizingatia mutayaona umuhimu wake. Na kinyume chake mtu mzuri ataoa mtu wa namna isiyokuwa yake au asi au mbaya wa tabia, akipata watoto wakiwa wakubwa wakamkuta mama yao na wajomba wamo katika hali hizo watoto hawatakuwa radhi kwa mama uliyewachagulia. Na ndio wanapoingia makosani ya kuanza kumtolea mama maneno, hasa nasaha zikiwa hazina tena kikao.
Ni kweli nguvu nyingi zime-elekezwa kwenye mchumba wa kike awe na sifa njema, nzuri za kidini zilizokwisha tajwa hapo nyuma. Lakini hiyo haina maana kuwa mwana mume yeye na-awe vyovyote vile. Laa.Hilo pia Mtume wetu (S.A.W.) hakuliacha, kalisemea. Tazama Hadithi hii ifuatayo:

" : ( ) "

Imepokelewa kutokana na Abi Hureira (R.A.A.) kuwa Mtume (S.A.W.) kasema: ( Akikujieni kuposa kwenu mtaeridhika na dini yake, na khuluka zake, (yaani mwenye kushika dini na mwenye khulqa nzuri) basi muozeni na kama hamukumuoza itakuwa fitina na fasada kubwa).
Kutokana na Hadithi hiyo, Mtume wetu ( S.A.W.) kitu cha kwanza alichotutaka turidhike nacho upande wa huyo mwanamme ni dini. Yaani dini kaiweka mbele kwa mwanamke na mwanamme na baadae ndio akataja khulqa nzuri. Kwani mwenye kushika dini inatarajiwa sana kuwa na khulqa yake itakuwa nzuri na ndio maana sifa mbili hizo zikatajwa pamoja. Hebu sasa natujiulize, kwa nini Mtume (S.A.W.) akatuambia kuwa mukikataa kumuoza binti yenu mwanamme mwenye sifa hizo itakuwa fitna na fasada kubwa? Sababu ni kuwa Uislamu umetufahamisha kuwa yeyote ataeishika dini hii ya Kiislamu, ambayo ndio dini aliyo ikiri mwenyewe ALLAAH subhaanahu wa taala kama alivyosema katika Quran, Sura ya Aali Imran (3) Ayyah ya 19 yakuwa:-
{ }
Hakika ya dini (ya haki) kwa ALLAAH ni Uislamu)
basi mtu huyo atakuwa na nyendo zenye maongozo mazuri ya kupigiwa mfano. Sasa tukimkataa mtu huyo mwenye sifa nzuri hizo, jee tutakuwa tunamgojea nani tena? Kinyume cha huyo, atakuwa ni yule mwenye sifa mbaya mwenye kufuata uongozi wa bilisi, yaani asieshika dini. Basi kusudio la Mtume (S.A.W) kusema itakuwa fitina na fasada kubwa, ni kuwa tukimgojea huyo asoshika dini ndio tukamuoza au tukamuweka binti yetu tu, bila ya kumuoza mume yeyote ndio hayo alotutahadharisha Mtume wetu (S.A.W). Hapo itakuwa litalotokea kwa binti yetu huyo, hatutokuwa na wa kumlaumu, isipokuwa kulaumu nafsi zetu zilizo tekwa na bilisi, nasi tukakubaliana nae.
Hayo yakiwa ni maelezo ya nasaha kwa ufupi ili tujue njia za kupita katika kutafuta mchumba mwenye kufuata maongozo ya dini ya Kiislamu , makusudio yake ni kumuomba ALLAAH atupe vizazi vyema vitavyo ishi kwa raha, utulivu wa moyo na kujionea fakhari kwa wazazi wao. Watoto hao wendapo wakiwa wakubwa wasije kuona haya mbele ya watoto wenziwao kama wale ambao mama zao hua ni wale walio okotwa ulevini au katika madanguro au katika mirambazo mirambazo ya ujana, na mengineyo yasiyokubalika katika misingi ya dini.
Ni haki ya mtoto kuchaguliwa mama/baba kabla ya kuzaliwa.

Tunamuomba ALLAAH Atujaalie Tuwe Mababa Na Mamama Wale Ambao ALLAAH Anawapenda Aamin
.

Waislamu Maelezo Haya Tumeyachukuwa Katika Kitabu Malezi Mema.

Na InshaALLAAHU Karibu Itatoka Chapa Ya Pili Itapatikana Katika Maduka Ya Vitabu AaminEwe Mola Wangu Nakuomba Kutokana na Majina Yako Matukufu Uwasamehe Wazazi Wangu Kama Walivyo Nilea Nilipokuwa Mdogo, Ewe Mola Wangu Wasamehe Na Uwarehemu Na Uwafutie Makosa Yao Uwaongezee Ujira Wao Na Uifanye Hisabu Yao Kuwa Nyepesi, Ewe Mola Wangu Tukutanishe Sisi Na Wao Katika Pepo Tukufu Ya (Firdausi) Pamoja Na Manabii Na Masidiki Na Mashahidi Na Watu Wema Na Uzuri Ulioje Kwa Watu Hao Kuwa Rafiki
( Zake) Na Sala Na Salamu Zimshukie Mtume Wetu Mpenzi Muhammad (SALLA ALLAAHU ALAYHI WA SALLAM) Pamoja Na Ali Zake Na Masahaba Zake Wote. Aamin.