ASALAM ALAYKUM,

MAHITAJI
nyama kilo 1 na nusu ya kusaga
mayai 18
siagi robo kilo
unga wa ngano robo kilo
carrots nusu kilo
pilipili boga robo kilo
uzile,mdalasini,pilipili manga za unga kidogo.
b/powder 2tsp
ndimu 1
kitunguu thomu na tangawizi kidogo.

NAMNA YA KUPIKA

1)chukua nyama itie viungo vyake vyote ndimu,thomu,tangawizi,uzile mdalasini,pilipili manga, ichanganye vizuri halafu iteleke iwache iwive na uhakikishe imekauka maji yote.
2)saga siagi na mayai 6 mpaka iwe cream na nyeupe kama ya keki ukisha tia unga na p/powder endelea kusaga mpaka iwe laini.
3)chukua treya ya kupikia ipake siagi kidogo au samli.
4)umimine huo mchanganyiko wa keki ktk treya yako ueneze vizuri kwa mwiko.
5)chukua mayai 6 yablend vizuri halafu yamimine ktk ile nyama na uchanganye vizurii sana mayai yakolee yote halafu mimina juu ya ule mchanganyiko wa keki itandaze vizuri hiyo nyama keki isionekane.
6)grate carrot ziwe kama chips za muhogo halafu zitie juu ya nyama zitandaze vizuri ukiziweka fanya kama unanyunyiza kwa mkono.kata pilipili boga ziwe slice kokwa toa,weka juu pia kama kerrots.
7)chukua mayai 6 yaliobakia yatie ktk blendar ya pige sanaa mpaka yatoke mapovu mengii sana halafu yamimine yaenee kote usiache nafasi bila ya kuweka mayai.
8)washa oven 180c pre- heated temp.halafu bake juu na chini,mpaka iwive na kukauka.
9)ikiwiva itoe iwache ipoe ikipoa kata vipande viwe square na uandaee.
10)tayari kwa kuliwa.