![]() |
|
|||
|
Assalam Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuhu.
Ndugu zangu wasomaji wa ukumbi huu, kwanza tunatoa shukurani za thati kwa juhudi zenu tofauti. Alhamdulilahi daraja tuliyofika ni ya kuridhisha, khasa katika masuala muhimu yanayoulizwa humu. na makala mengineyo Ama mwaka huu tutapenda kujua rai za wasomaji juu ya ukumbi huu, tusaidiane fikra, nini la kuengezwa, au sehemu gani inahitajika kuwekwa sawa, maana tukipata mashauriano itakuwa ni vyema kuupeleka mbele ukumbi huu. Kwa hivyo kila mwenye rai anakaribishwa kuandika rai yake hapa, nini la kufanya katika mwaka huu. Tunataraji kuona rai na ushauri wenu inshaallah. shukran. uislamu.net webmaster |
|
|||
|
Quote:
mimi kwanza ningeliomba uwekwe ukimbi wa maoni kama itawezekana shukran
__________________
km1185@hotmail.co.uk |
|
|||
|
Assalam alaykum Warahmatullahi Wabarakatuhu.
Asante sana ndugu yangu mk1185 kwa juhudi zako na kuitikia kwako wito kwa haraka, hii ikionesha hima yako. Ama ukumbi wa maoni ni vyema kutupa fikra zaidi nini yatakuwa madhumuni yake, na makala gani yataandikwa na jee faida gani tutaweza kunufaika, kwani ni bora tuyadurusu mambo haya, na kutarajia wengine kuunga mkono jambo hili, na tukikubaliana basi ni kazi ya dakika tano tu inshallah. shukran. uislamu.net webmaster |
|
|||
|
Quote:
Maoni yangu juu ya umuhimu wa kuwepo UKUMBI WA MAONI Huo ukimbi wa maoni utakuwa unatumika kama unavyotumika ukumbi wa dini na sharia kwenye mas-ala ya maoni,ushauri na matangazo yanayohusu website au wanakumbi hizi. kwa hiyo tukiuweka ukumbi wa maoni, ukumbi wa dini na sharia utabaki purely dini na sharia. Maoni hayo yatakuwa mara nyingi yanahusu maendeleo ya website au matatizo yake, au hata masuala kuhusu website hii kama vile mfano mtu hawezi kuingia kwenye link fulani, na huenda akauliza mbona sipati kuingia kwenye link fulani? akapata jawabu na sababu juu ya link hiyo iliyokuwemo katika website hii na huwenda ikasaidia vilevile baadhi ya wakati, kwani mawebmaster wanakuwa hawajui kama kuna tatizo fulani sehemu fulani katika website zao, kwa hiyo hii itakuwa ni kama tanbih inshaallah. inaweza kutumika kwa namna mbali mbali za faida. shukran
__________________
km1185@hotmail.co.uk |
|
|||
|
Assalam Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuhu.
Asante sana ndugu yangu, fikra nzuri, basi tuwasubiri na wenzetu wengine waliunge mkono jambo hili. tunawasubiri wanaukumbi wengine..... shukran
uislamu.net |
|
|||
|
Assalam alaykum Warahmatullahi Wabarakatuhu.
Ndugu yangu mk1185 inaonesha mimi na wewe tu, ndio tunataka ukumbi wa maoni, maana bado hata mmoja hajatupa ushauri wake... shukran uislamu.net |
|
|||
|
Quote:
JAMANI USHAURI ULITOKA KUHUSU KUWEPO KWA UKUMBI WA MAONI. JE UKUWEPO AU USIKUWEPO. TUANDIKIE JAPO NENO MOJA: -UWEPO -USIWEPO SHUKRAN W/SALAAM
__________________
km1185@hotmail.co.uk |
|
|||
|
Assalam Alaeykum Warahmatullahi Wabarakatuhu.
Na Kwa Maoni Yangu Mimi Hivi Sasa Tunawaomba Wale Maulamaa Wa Kislamu Wote Duniani Uwepo Ummoja Wa Kimataifa Wa Uislamu Duniani Kote Ambao Utakuwa Unaokwenda Sambamba Na Mvumo Wa Quraan Tukufu Kufuata Yote Yale Ambayo Mwenyewe Allah Ametuamrisha Kupitia Katika Quraan Tukufu. Na Huu Umoja Wa Kimataifa Uwepo Makka Mukkarama .Au Munasemaje Waislamu?
__________________
لا إلهَ إلاّ اللّهُ ?????? ????? ?????????? ??????????? HAYA NI MAELEZO YALIYO WAZI KWA WATU (WOTE) NA OWONGOZI NA MAUIDHA KWA WAMCHAO (MWENYEZI MUNGU). Mkumbushe Kwa Qurani Anayeogopa Onyo Langu. Jitihada Kwetu Tumshinde Iblisi Dua Nakuombeeni. Furaha Kuwa Kivuli Chetu, Afya Njema Kuwa Mavazi Yetu, Amali Njema Kuwa Pambo Letu Pepo Kuwa Maskani Yetu Ya Milele Aamin Na Sipati Kuwezeshwa Haya Ila Na Mwenyezi Mungu. Kwake Yeye Ninategemea, Na Kwake Yeye Naelekea .
Last edited by WALAD MUHAMMAD; 30-01-06 at . |
|
|||
|
Assalam Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuhu.
ASANTE SANA ndugu yangu Abunooh..Wewe ni mtu wa tato miongoni mwa member 407 tuliokuwa nao, sisi hatukuomba pesa wala dhahabu, ila tu ushauri. Jazakallahu kila kheri, na ombi litaangaliwa na uislamu.net lakini bado haitoshi rai ya watu watano tu. shukran sana uislamu.net webmaster |
![]() |
| Bookmarks |
Currently Active Users Viewing This Thread: 1 (0 members and 1 guests) |
|
| Thread Tools | |
|
|