ukumbi  

Go Back   ukumbi > ukumbi Main Category > UKUMBI WA MASUALA ya DINI > Ndoa na Talaka

 

 

LinkBack Thread Tools
  #1 (permalink)  
Old 26-02-08,
Moderator
 
Join Date: 10-09-04
Location: Mawaleh-Shamaliya,Oman
Posts: 225
Send a message via MSN to Abu-Muslim Send a message via Yahoo to Abu-Muslim
Default Kuoa mke wa pili

Sheikh,
Asalaam alaykum.
Kuna kijana anauliza hivi,yeye ameamua kuoa mke wa pili na akaamua kumueleza mkewe kusudio lake hilo.Lakini kwa bahati mbaya mkewe hakuwafiki suala hilo,ni hataki hata kusikia neno moja.Aya na hadithi zote alizompa kuhusu wajibu huo hazikufaa kitu.Kila anapotaja suala hilo basi mkewe hupanda pressure na kutaka kuzimia.
Suala analouliza kijana ni nini cha kufanya ikiwa mkewe hataki mumewe aoe mke mwengine na akimpa nasaha njema ili arudi kwa Allah hasikii bali zinamfanya kuwa mgonjwa.

Namuombea majibu kijana wetu inshaallah.

Wabillahi at tawfiq.

Akhuukum,

Abu-Muslim
  #2 (permalink)  
Old 30-06-08,
uislamu.net webmaster
 
Join Date: 17-07-04
Location: muscat
Posts: 822
Default

Waleykum Salam Warahmatullahi Wabarakatuhu

Ndugu yangu Abu-Muslim asante kwa suala lako..
Kidesturi nadhani hakuna mke ambae anakamatana mkono na mumewe ili akamposee mke wa pili. Takriban wanawake wote hawakubali kukaa uke wenza, hata kama watakuwapo basi ni wachache. Tatizo si kumfahamisha sasa havi wakati hajaowa, yeye sio kama hafahamu, bali anafahamu kuwa hii ni sheria na hakuna awezae kupinga..Tatizo ni kuleta uadilifu baada ya ndoa. Na ukiwauliza waliokuwa na wake wawili au zaidi, basi watakwambia kwamba siku ya kwenda kuowa wa pili, wa mwanzo alikua hajui..Ila tu baada ya ndoa atapata habari na huwenda kama ulivyosema akazimia au hata kupata homa kali. Lakini wajibu wa mume kama kweni alikuwa anashida ya kuongeza mke wapi na hali inamruhusu na kuweza kuleta uadilifu. Basi hapo ndo pana kazi ya kumpoza mke wa mwanzo na kumuonesha kwamba shauri ya kuowa wa pili haikuwa ni kosa maana tutasikiliza kama mwanzo bali zaidi.
Lakini akifanya kinyume ya hayo ndo atajitia katika matatizo.

Natumai kesi kama hizi kila mtu awe tabibu wa nafsi yake maana kila mmoja ndie ajuae nyumba yake zaidi na amjua mkewe zaidi kuliko wengine. Kama kuna njiya ya kumnasihi au kumfahamisha akafahamu basi mume ndie aijua zaidi kwani wanaishi pamoja miaka.

Tunamuombea masikilizano mema na tawfeeq daima.
Wallahu Aalam

uislamu.net webmaster
__________________

uislamu.net webmaster
uislamu@hotmail.com
 

Bookmarks


Currently Active Users Viewing This Thread: 1 (0 members and 1 guests)

 
Thread Tools

Posting Rules
You may not post new threads
You may not post replies
You may not post attachments
You may not edit your posts

BB code is On
Smilies are On
[IMG] code is On
HTML code is Off
Trackbacks are On
Pingbacks are On
Refbacks are On



All times are GMT +5. The time now is .


Powered by vBulletin Version 3.8.3
Copyright ©2000 - 2010, Jelsoft Enterprises Ltd - Upgraded by SurCity.net.