Anaetaka Misahafu na Juzuu
Assalamu Alaikum WarahmatuLLahi wa Barakatuh
Ndugu zangu wa Islamu,Huko Afrika watoto wa Kiislamu wengi mno na pia Miskiti wanapata shidda kubwa sana kupata misahafu na juzuu.Kwa hivyo hakuna budi illa kukuombeni muwasaidie kuwanunulia na kuzipeleka huko na Thawabu zake mnazijua hakuna haja ya kukufahmisheni.
Hapa Omani ndugu zetu wamejitolea kuuza Misahafu na juzuu kwa bei ndogo kabisa kama ifuatayo:
1.Msahafu mzuri riali moja.
2.Juzuu moja ni bazi 150 tu.Juzuu sokoni inauzwa mpaka baza 800 na hawa jamaa hawakuzidisha baiza 150.
Ndugu hao ni:
Sk.Hilal Alharthy 99459120.
Sk.Said Al Mufarji 99425598.
Hii ni fursa ya kuitafuta pepo khususan katika mwezi mfadhili wa Ramadhan.
|