ukumbi  

Go Back   ukumbi > ukumbi Main Category > UKUMBI WA MASUALA ya DINI

Reply

 

LinkBack Thread Tools
  #1 (permalink)  
Old 01-02-10,
New Member
 
Join Date: 15-05-08
Posts: 25
Default Hajji na sala ya eid

Assalamu alaykum warahmatullah wabarakaatuh

Nini hekima ya mwenye kutekeleza ibada ya hija kutokufunga sunna ya "ashuraa" na kutokusali sala ya eid

Wabillah ttawfiq
Reply With Quote
  #2 (permalink)  
Old 08-02-10,
Abukhalil's Avatar
Msimamizi wa Masuala ya Dini
 
Join Date: 07-09-04
Posts: 1,202
Default

Waalaykum Salaam warahmatu-LLahi wabarakaatuh

Jawabu:

Nadhani unakusudia saumu ya "Siku ya Arafa", ambapo mahujaji huwa katika kisimamo cha Arafa. Imethibiti kuwa Mtume wa Allah -rehma za Allah na amani zimshukie- hakufunga siku hiyo alipohiji. Kwa ajili hiyo, imefahamika kuwa himizo lake -rehma za Allah na amani zimshukie- la kuifunga siku hiyo ni kwa wale wasiokuwa katika hijja.

Wenye ilmu wamesema kuwa hikma ya kuto kufunga siku hiyo kwa mwenye kuhiji ni kumfanya awe na nguvu na hamasa ya kumdhukuru Allah kwa wingi na kumuomba tangu adhuhuri hadi magharibi bila ya kudhoofika.

Halikadhalika sala ya eid haikusuniwa kwa mahujaji kwasababu wakati wa sala hiyo wao huwa wameshughulika na kupiga jamra la 'Aqaba, na wakimaliza hufanya ibada nyenginezo za hijja kama kuchinja, kunyoa na kutufu tawafu ya ifadha.
Wa'LLahu A'lam.

Abukhalil.
Reply With Quote
  #3 (permalink)  
Old 11-02-10,
New Member
 
Join Date: 15-05-08
Posts: 25
Default

Mtu ambaye anafanyiwa hija na mtu mwngine na yeye (mwenyekufanyiwa hija) akabakia katika nchi yake kipi kilichobora kwake kuhusuina na utekelelezaji wa ibada ya funga ya arafat na sala ya ied?
Reply With Quote
  #4 (permalink)  
Old 21-02-10,
Abukhalil's Avatar
Msimamizi wa Masuala ya Dini
 
Join Date: 07-09-04
Posts: 1,202
Default

Jawabu:

Madamu yeye hayumo mwenyewe katika hija, bila shaka ni bora kwake akiweza kufunga siku ya arafa na kuhudhuria sala ya Eid. Wa'LLahu A'lam.

Abukhalil.
Reply With Quote
Reply

Bookmarks


Currently Active Users Viewing This Thread: 1 (0 members and 1 guests)

 
Thread Tools

Posting Rules
You may not post new threads
You may not post replies
You may not post attachments
You may not edit your posts

BB code is On
Smilies are On
[IMG] code is On
HTML code is Off
Trackbacks are On
Pingbacks are On
Refbacks are On



All times are GMT +5. The time now is .


Powered by vBulletin Version 3.8.3
Copyright ©2000 - 2010, Jelsoft Enterprises Ltd - Upgraded by SurCity.net.