![]() |
|
|||
|
Pepo imetengenezwa kwa mabustani mazuri mazuri na mito aina tofauti inayopita mbele yake. Mwenyezi Mungu S.W.T. katuelezea katika Suratil Baqarah aya ya 25, “
]æóÈóÔøöÑú ÇáøóÐöíäó ÂãóäõæÇ æóÚóãöáõæÇ ÇáÕøóÇáöÍóÇÊö Ãóäøó áóåõãú ÌóäøóÇÊò ÊóÌúÑöí ãöäú ÊóÍúÊöåóÇ ÇáÃäúåóÇÑõ[ Maana yake, “Na wabashirie walioamini na kufanya vitendo vizuri, kwamba watapata mabustani yapitayo mito mbele yake.” Mtume S.A.W. alipokuwa katika safari yake ya usiku wa Israa alioneshwa mito hiyo ya Peponi naye akasema. Katika Hadithi iliyopokelewa na Anas bin Maalik R.A.A. kasema, “ ‘‘ÑõÝöÚóÊú áöí ÇáÓöÏúÑóÉõ ¡ ÝÅÐÇ ÃÑÈÚÉ ÃäåÇÑ : äóåúÑóÇäö ÙóÇåöÑóÇäö ¡ æóäóåúÑóÇäö ÈóÇØöäóÇäö ¡ ÝÃãÇ ÇáÙøóÇåöÑóÇäö ÝóÇáäøöíáõ æóÇáúÝõÑóÇÊõ ¡ æóÃóãøóÇ ÇáúÈóÇØöäóÇäö : Ýöí ÇáúÌóäøóÉö (ÓóíúÍóÇäõ æóÌóíúÍóÇäõ) Maana yake, “Nikapandishiwa juu (mti wa) Mkunazi (katika mbingu ya saba), tahamaki (nikaona) mito minne: mito miwili iliyo dhahiri, na mito miwili iliyofichika. Ama ile iliyo dhahiri ni (mto) Nile na Euphrates. Na ama ile iliyofichika ni mito miwili katika Pepo (Saihaan na Jaihaan).” Mto mmoja wa Peponi unaitwa Kawthar na ambao Mwenyezi Mungu S.W.T. amemuahidi kumpa Mtume wetu S.A.W. kwa ajili ya kumliwaza baada ya kufiliwa na mtoto wake. Maadui zake walifurahia sana kitendo hiki cha kufiwa mwanawe kwani wao walikuwa wakiona hapana kheri kubwa katika dunia hii kama kuwa na mali na watoto wanaume. Lakini neema za Mwenyezi Mungu hazina kikomo na anampa amtakae. Mwenyezi Mungu S.W.T. kasema katika Surat Kawthar aya ya 1, “ ]ÅöäøóÇ ÃóÚúØóíúäóÇßó ÇáúßóæúËóÑó[ Maana yake, “Hakika tumekupa kheri nyingi.” Mtume wetu S.A.W. kwa kuwafahamisha Masahaba zake aliwauliza kwa njia ya maswali kuhusu mto Kawthar katika Hadithi iliyopokelewa na Anas bin Maalik R.A.A. na kutolewa na Muslim, kasema, “ ‘‘ÃÊóÏúÑõæäó ãóÇ ÇáúßóæúËóÑõ ¿ ÞóÇáõæÇ : Çááøóåõ æóÑóÓõæáõåõ ÃóÚúáóãõ ! ÞóÇáó : åõæó äóåúÑñ æóÚóÏóäöíåö Çááå ÚóÒøó æóÌóáøó ¡ Úóáóíúåö ÎóíúÑñ ßóËöíÑñ’’ Maana yake, “Mnajua nini Kawthar?” Wakasema: “Mwenyezi Mungu na Mtume Wake ndio wajuao!” Akasema (Mtume S.A.W.): “Huo ni mto alioniahidi Mwenyezi Mungu Mtukufu (kunipa) una kheri nyingi.” Mito ya Peponi si mito ya maji peke yake bali pia kuna mito ya vinywaji aina nyingine mbalimbali kama vile: Mito ya maziwa, mito ya ulevi wenye ladha kwa wanywao, na si kama ule ulevi wa duniani wa kutoa akili na kuumiza kichwa. Na pia kuna mito ya asali iliyosafishwa yenye ladha nzuri kabisa kwa wanywao. Kama alivyotufahamisha Mwenyezi Mungu S.W.T. ndani ya Qur`aani, kasema katika Surat Muhammad aya ya 15, “ ]ãóËóáõ ÇáúÌóäøóÉö ÇáøóÊöí æõÚöÏó ÇáúãõÊøóÞõæäó ÝöíåóÇ ÃóäúåóÇÑñ ãöäú ãóÇÁò ÛóíúÑö ÂÓöäò æóÃóäúåóÇÑñ ãöäú áóÈóäò áóãú íóÊóÛóíøóÑú ØóÚúãõåõ æóÃóäúåóÇÑñ ãöäú ÎóãúÑò áóÐøóÉò áöáÔøóÇÑöÈöíäó æóÃóäúåóÇÑñ ãöäú ÚóÓóáò ãõÕóÝøðì…[ Maana yake, “Mfano wa Pepo walioahidiwa wacha Mungu ina mito ya maji yasiyovunda, na mito ya maziwa isiyoharibika ladha yake, na mito ya ulevi yenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyosafishwa…” Katika Pepo kuna mto mwingine unaoitwa Baariq ambao uko katika mlango wa Pepo, mto huu ni makhsusi kwa ajili ya watu waliokufa mashahidi na ambao walioko bado katika Barzakh (maisha baada ya kufa), roho zao zitakuwa kwenye mto ule. Kama ilivyoelezewa katika Hadithi iliyopokelewa na Ibn Abbas R.A.A. na iliyotolewa na Ahmad, Tabarani na Haakim, “ ‘‘ÇáÔøõåóÏóÇÁõ Úóáóì ÈóÇÑöÞö äóåóÑò ÈöÈóÇÈö ÇáúÌóäøóÉö ¡ Ýöí ÞõÈøóÉò ÎóÖúÑóÇÁó ¡ íóÎúÑõÌõ Úóáóíúåöãú ÑöÒúÞõåõãú ãöäó ÇáúÌóäøóÉö ÈõßúÑóÉð æóÚóÔöíøðÇ’’ Maana yake, “Mashahidi (watakuwa) kwenye mto wa Baariq katika mlango wa Pepo, katika mnara wa kijani, inatoka riziki zao kutoka Peponi asubuhi na jioni.” Makala haya yametolewa kutoka katika kitabu changu, "Neema za Peponi." |
![]() |
| Bookmarks |
Currently Active Users Viewing This Thread: 1 (0 members and 1 guests) |
|
| Thread Tools | |
|
|