Waalaykum Salam warahmatu-LLahi wabarakaatuh
Jawabu:
Sikuona katika wenye ilmu aliyeainisha umri huo kwa miaka, lakini wanasema siyo kusita kupata hedhi tu, bali na kufikia hali ya kuto kutamani kuolewa na kuto kutamaniwa na waume kwa utuuzima.
Hao ndio walioruhusiwa, katika surat A'Nuur aya 60, kupunguza nguo wanazovaa kwa stara ya nje; yaani wanaweza kuacha kuvaa abaya (baibui) wakatosheka na kanzu zao na mtandio bila kujipamba na kuonesha mapambo yao. Hata hivo wameambiwa wakijitakasa kwa kuto kuacha stara kamili ni bora kwao. Kutokana na rukhsa hiyo ndiyo kumekuwa na kauli inayoruhusu kupewa mikono lakini pia kuacha ni bora. Wa'LLahu A'lam.
Abukhalil.
|