ukumbi  

Go Back   ukumbi > ukumbi Main Category > DINI na SHERIA

Reply

 

LinkBack Thread Tools
  #1 (permalink)  
Old 18-04-10,
Moderator
 
Join Date: 10-09-04
Location: Mawaleh-Shamaliya,Oman
Posts: 225
Send a message via MSN to Abu-Muslim Send a message via Yahoo to Abu-Muslim
Default Hivi ndivyo tulivyo

Bismillahi Rahmani Rahim.
Asalaam alaikum warahmatullahi wabarakatuh.
Ndugu Waislamu nimefikiria fikra moja ambayo kwa mawazo yangu nahisi itasaidia kufikia katika njia moja wapo ya kuamrishana mema na kukatazana maovu.Fikra yenyewe ni hiii ya kuanzisha mada " HIVI NDIVYO TULIVYO ". Lengo ni kwamba kila mtu aweze kueleza kile anachokiona katika jamii yake anayoishi iwe kizuri au kibaya ili watu wapate kuacha kama ni maovu au kupata faida ya kushajiishwa kama ni kizuri.Lakini kuwe na sharti kwamba kusitajwe majina ya watu,wadhifa au kitambulisho chochote kitachoweza kumtambua mtu.Na vile vile kusitajwe majina ya mitaa au mahala pa kazi.Tunaweza kutaja majina ya nchi kama Oman.Zanzibar,Ulaya,Marekani nk.Kusudio ni kwamba kuelimishana na kuongozana kwenye njia ya Allah(S.W.T) na sio kubishana na kutoleana aibu.Nimekuwa na fikra hii kwasababu kuna makosa ambayo tunayafanya katika maisha yetu ya kila siku na watu tunaoneana haya kukatazana au kuoneana vibaya.Kwa kutumia njia nahisi itakuwa ni fursa kwa kila mtu kuelezea anachokiona kama kinafanywa kimakosa na watu pia wakakiona anachofanya yeye ni makosa.Na natija ya maelemisho ikapatikana.
Tunaomba ushiriki wenu katika kuchangia mada au kutoa nasaha nyengine.
__________________
Sema: Enyi watu! Haki imekwisha kukujieni kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi anaye ongoka anaongoka kwa faida ya nafsi yake, na anaye potea anapotea kwa khasara ya nafsi yake. Na mimi si mwakilishi juu yenu. - Suratil Yunus :108


Wabillahi at tawfiq,

Akhuukum,

Abu-Muslim.

Last edited by Abu-Muslim; 10-05-10 at .
Reply With Quote
  #2 (permalink)  
Old 10-05-10,
Moderator
 
Join Date: 10-09-04
Location: Mawaleh-Shamaliya,Oman
Posts: 225
Send a message via MSN to Abu-Muslim Send a message via Yahoo to Abu-Muslim
Default Kufuga Mbwa majumbani

Asalam alaikum
Mtume s.a.w amekataza ufugaji wa mbwa kwa Muislamu ila kuwe kwasababu mbili zifuatazo:-
1. Kwa ajili ya kuwindia.
2. Kwa ajili ya ulinzi.
Bila ya sababu mbili hizi haimjuzii Muislamu kufuga mbwa ndani ya nyumba yake.
Hivi karibuni kumeingia mtindo ( fashion ) kwa vijana wa kiislamu kufuga mbwa ndani ya majumba yao, kwa vile tu wanaiga tabia za watu ambao sio waislamu.
Kwao wanaona ni ustaarabu na maendeleo ya kizungu kufuga mbwa.Na wanaona fakhari kufanya matembezi nje pamoja na mbwa wao.Huu si ustaarabu bali ni kwenda kinyume na maamrisho aliyokuja nayo Rasuul s.a.w.

Tunamuomba Allah atuhifadhi
__________________
Sema: Enyi watu! Haki imekwisha kukujieni kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi anaye ongoka anaongoka kwa faida ya nafsi yake, na anaye potea anapotea kwa khasara ya nafsi yake. Na mimi si mwakilishi juu yenu. - Suratil Yunus :108


Wabillahi at tawfiq,

Akhuukum,

Abu-Muslim.
Reply With Quote
  #3 (permalink)  
Old 10-05-10,
Moderator
 
Join Date: 10-09-04
Location: Mawaleh-Shamaliya,Oman
Posts: 225
Send a message via MSN to Abu-Muslim Send a message via Yahoo to Abu-Muslim
Default Azza - Matanga

Asalaam alaikum,

Binadamu sote ni wakoseaji, hapana budi kukosoana.Kuna kijana amehadithia kwamba kabla ya miaka miwili ilopita alifiwa na shangazi yake.Baada ya kumaliza taratibu zote za kuzika na wakati wa Azza kumalizika ilipofika magharibi wakasali.Walipomaliza kusali wale wafiwa walikusanyika kwenda kwao kwa ajili ya kunywa chai na kupumzika. Mashaallahu wafiwa hawakupata taabu ya kuhangaika kwa kupika chai.Vyakula vyote vilitoka kwa jamaa na majirani ambao wamefanya jambo la kheri kuwapunguzia mzigo walofiwa kwa kuwasaidia kuwaletea vyakula.Ni mfano mzuri na unapasa kuigwa kwa waislamu wote.Lakini penye zuri hapakosi kasoro. Kasoro ilojitokeza hapo ni kwamba kulikusanyika watu ambao hawakuhitaji kuwepo kwao pale.Huo ulikuwa ni msiba kwa wafiwa na haikuwa karamu au hafla maalum. Na juu ya hayo pakawa na mazungumzo, mahadithi na vicheko katika chai hio, hata wafiwa wakawa wanajiuliza hivi kweli tunamsiba wa kuondokewa na mzee wetu au tuna karamu ya hafla ya kuondoka kwake?
Linalopasa kwetu ni kupeana msaada wakati wa kufiwa ili kupunguziwa mzigo na sio kuzidishiwa mzigo.Watu wanaostahiki kuwepo ni wenyewe wafiwa pamoja na ndugu na jamaa ambao wamesafiri kutoka mbali kuja kwenye kilio na hawawezi kurudi siku ile ile kwa umbali wa safari,na sio akina sisi tuko jirani ya mfiwa tukamkalie atulishe asubuhi,.mchana na usiku. Huo ni kwa upande wa wanaume.
Na kwa upande wa wanawake ni mambo makubwa zaidi kwani wao huwacha nyumba zao,waume zao,watoto wao na shughuli zao zote kwenda kumkalia mtu alofiwa ndani ya nyumba yake akawa hana hata wakati wa kupumzika kwa msongamano wa watu ulojaa ndani.Siku tatu za kupikiwa,kupakuliwa,kuandaliwa watu wasiokuwa na kazi ila kula,kulala na kusemana.Yakisha hayo yanayoitwa Matanga tena kazi kwa mwenye nyumba kuisafisha nyumba iloyopinduliwa juu chini.Kuna baadhi ya mambo hayahitaji mjuzi wa elimu kuyatambua kwamba hili baya hili zuri,akili inatosha kufikiri na kutambua kwamba hili silo,hili ndilo.Kwasababu sisi ni binadamu tumepewa akili ili tuitumie.

Hivi ndivo tulivyo!!!!

Tujirekebishe ndugu zanguniiii!!!!
__________________
Sema: Enyi watu! Haki imekwisha kukujieni kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi anaye ongoka anaongoka kwa faida ya nafsi yake, na anaye potea anapotea kwa khasara ya nafsi yake. Na mimi si mwakilishi juu yenu. - Suratil Yunus :108


Wabillahi at tawfiq,

Akhuukum,

Abu-Muslim.
Reply With Quote
  #4 (permalink)  
Old 14-05-10,
Moderator
 
Join Date: 10-09-04
Location: Mawaleh-Shamaliya,Oman
Posts: 225
Send a message via MSN to Abu-Muslim Send a message via Yahoo to Abu-Muslim
Default Kombe la dunia v/s kombe la akhera

Bismillahi rahmani rahim.

KOMBE LA DUNIA V/S KOMBE LA AKHERA


Asalaam alaikum,
Watu wamo mbioni kwa matayarisho ya Kombe la Dunia huku wakisahau Kombe la Akhera ambalo ndilo lenye thamani kubwa na ya kudumu.Habari na mazungumzo mitaani ni hayo.Huo ni wakati wa sala kutupwa,kusahauliwa au kusaliwa bila khushuu.Fikra zote ziko kwenye kombe la dunia.Watu kukesha mpaka usiku mkubwa mpaka kusali alfajiri kunawapita.Tujihadhari waislamu na kusahau kombe la akhera.Huko ni kufuzu milele.Wakati wetu tuutumie vizuri kwani suala la wakati litakuwemo kwenye karatasi ya mtihani wa kombe la akhera.Jee tunajua jawabu lake???
Tujiandae kujibu vipi tumeutumia wakati wetu.
__________________
Sema: Enyi watu! Haki imekwisha kukujieni kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi anaye ongoka anaongoka kwa faida ya nafsi yake, na anaye potea anapotea kwa khasara ya nafsi yake. Na mimi si mwakilishi juu yenu. - Suratil Yunus :108


Wabillahi at tawfiq,

Akhuukum,

Abu-Muslim.
Reply With Quote
  #5 (permalink)  
Old 29-07-10,
Moderator
 
Join Date: 10-09-04
Location: Mawaleh-Shamaliya,Oman
Posts: 225
Send a message via MSN to Abu-Muslim Send a message via Yahoo to Abu-Muslim
Default Malezi ya vijana wetu

Asalaam alaikum warahmatullahi wabarakatuh.
BISMILLAHI RAHMANI RAHIM.
Tunachukua fursa hii tena kukumbushana.
Malezi ya vijana wetu kwa mtizamo wa nyakati za kulala na kuamka katika nyumba zetu.Bila ya kuchunguza wala kudadisi suala hili utaona kwamba asilimia kubwa au unaweza kusema inakaribia yote ya vijana wetu wanautumia wakati wa usiku kuzunguruka mabarabarani,madukani,mikahawani (kuvuta mashisha), kukaa mabarazani,kuangalia TV kukesha mpaka karibu ya alfajiri.Na inapoadhiniwa sala ya alfajiri wao huwa washapanda vitandani kwa kulala.Mchana kutwa huwa wamelala.Malezi tuliyolelewa sisi ilikuwa ikifika magharibi, watoto wote huwa ndani au misikitini.Na ikimaliza sala ya Isha na kunywa chai,moja kwa moja kwenda kulala.Hivi ndivyo tulivyolelewa sisi,lakini leo cha ajabu ni kwamba wazee sisi tuliolelewa tukaleleka katika malezi mazuri imekuwa kinyume tunavyowalea watoto wetu.Unapokwenda katika nyumba zetu wakati wa asubuhi au mchana utaona vibaya hata kuuliza watoto wako wapi, huku ukimuona mzee anapohangaika kufungua mlango kukukaribisha na kukuwekea kahawa.Na utapo uliza utajibiwa kuwa wamelala bado kwasababu usiku wamechelewa kulala.Ni kweli malezi haya yatatujengea jamii nzuri ya kiislamu?Ikiwa vijana wetu wa kiume wao ndio msingi wa jamii na tegemeo la taifa linalokuja wanaachiwa kuranda usiku na kulala mchana kutwa,nini tunategema maisha yao ya baadae?
Huu sio mwendo alokuja mtume wetu (s.a.w).Muislamu anatakiwa kulala mapema usiku na kuamka mapema alfajiri na ikiwezekana kuamka kabla ya alfajiri kwa kisimamo cha usiku.Na Allah (s.w.t) amesema katika Qur-aan suratil Furqaan aya 47 na Suratil Nabaa aya : 10




47. Naye ndiye aliye kufanyieni usiku kuwa ni vazi, na usingizi kuwa mapumziko, na akakufanyieni mchana ni kufufuka



10. Na tukaufanya usiku ni nguo?



Sadaqallahu l-adhiym.

Haya ni maneno ya muumba wetu alotupa muongozo huu wa Qur-aan ili tuufuwate.Lakini binadamu ni wakaidi wakupinga maamrisho ya Mola wao.Kila alichotuamrisha Allah tukifuate kina faida na kila alichotukataza kina madhara yake.Hivi karibuni tu wanasayansi wamegundua kuwa jua la asubuhi lina faida kubwa kwa mwanadamu na manufaa makubwa kwa ukuwaji wa watoto wadogo na linasaidia wanawake kupata calsium yakujenga mifupa.Na pia wamesema hewa ya oxygen safi inapatikana asubuhi mapema.Mbali na kwamba kuamka mapema kunasaidia akili kuwa nzuri zaidi na fikra za binadamu kupanuka.Na kiwiliwili kuchangamka.Neema kubwa sana kuamka mapema.Rasuul s.w.a alikuwa halali baada ya kusali alfajiri ila hubaki msikiti mpaka asali sala ya shuruq.Na akasema kufanya hivyo ujira wake ni sawa sawa na kwenda umra kamili,kamili kamili.Kwa ufupi ni kwamba maumbile ya binadamu yanakubaliana na maumbile ya dunia na maamrisho ya Qur-aan na Sunna.Kwenda kinyume chake ni kupingana na maamrisho ya Allah na sunna za Rasuul s.a.w.

Allah atujaalie wenye kufuata maamrisho yake na kuwacha makatazo yake, AMIN
__________________
Sema: Enyi watu! Haki imekwisha kukujieni kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi anaye ongoka anaongoka kwa faida ya nafsi yake, na anaye potea anapotea kwa khasara ya nafsi yake. Na mimi si mwakilishi juu yenu. - Suratil Yunus :108


Wabillahi at tawfiq,

Akhuukum,

Abu-Muslim.
Reply With Quote
Reply

Bookmarks


Currently Active Users Viewing This Thread: 1 (0 members and 1 guests)

 
Thread Tools

Posting Rules
You may not post new threads
You may not post replies
You may not post attachments
You may not edit your posts

BB code is On
Smilies are On
[IMG] code is On
HTML code is Off
Trackbacks are On
Pingbacks are On
Refbacks are On



All times are GMT +5. The time now is .


Powered by vBulletin Version 3.8.3
Copyright ©2000 - 2010, Jelsoft Enterprises Ltd - Upgraded by SurCity.net.