Waalaykum Salam warahmatu-LLahi wabarakaatuh
Jawabu:
Akiwa hataraji kupona maradhi yake akaweza kufunga baadae, anapaswa badala ya kufunga atoe fidia ya kulisha masikini mmoja kwa kila siku ya Ramadhani iliyopita na kadhalika itakapofika Ramadhani ijayo. Maskini apewe milo miwili kwa kila siku ya Ramadhani au nusu pishi ya mchele (= kilo moja na gramu 25). Akichukua rukhsa ya kutoa thamani aongeze kidogo kwa ajili ya usalama zaidi; mfano akitoa riali moja na nusu ya Omani inatosha kwa sasa. Maskini mmoja anatosha kupewa kwa siku zote.
Akiwa hana uhakika kama baadae ataweza au hataweza kufunga, ni bora akatoa fidia kwa mwaka uliopita madamu Ramadhani ya pili imeshafika naye bado hajaweza kufunga na ni mtu mzima, kisha akiweza baadae atalipa.
La kuzingatia ni kuwa fidia inapomlazimu humlazimu katika mali yake mwenyewe; akiwa hana mali anasameheka wala haiwalazimu wanawe ila wakipenda kumtolea kama sadaka.
Wa'LLahu A'lam.
Abukhalil.
|