![]() |
|
|||
|
Asalaam alaykum
Naomba kuuliza kama kuna mtu anayefahamu dawa ya mba (dandruf ) wa kichwani.Nimejaribu kutumia shampoo za kila aina lakini sijapata nafuu yoyote na hali inazidi kuwa mbaya siku hadi siku mpaka nywele zinaanza kutoka kwasababu ya mba. Naomba msaada wenu. Wabillahi at tawfiq Akhuukum, Abu-Muslim. |
|
|||
|
Quote:
Inshallah nitajitahid kidogo kutoa dawa ninayoijua ya mbaa, mbaa jutokana na ngozi iliyokufa katika kichwa yaani dead cell. dawa zilizopo ni : Ndimu au limau: Kabla kwenda kukoga jisugue limau ndani ya kichwa na baadae yale maganda ya limau yatie katika maji ya kukoga yaani yawe dafi dafi halafu ukoshe kwa maji yale kwanza na baadae utumie maji yaliyo safi. Fenugreek hizi sina uhakika kwa kiswahili lakini zimekaa kama rai hivi ila hizi rangi yake ni ya brown vimekaa km jiwejiwe vidogodogo kama kuna mtu anajua kwa ksiwahili naomba atusaidie. Hii unachukua vijiko 2 vya chai vya fenugreek unazirowesha katika maji usiku mzima ili zipate kulainika, halafu unazipoda ponda na baadae unapakaa ndani ya kichwa na uwache kwa muda wa saa moja na baadae kuzikosha ikiwa utafanya hivi siku zote mbaa wataondoka Inshallah bila tabu yoyote. WABILLAHI TAWFEEQ
__________________
Tunamhimidi Allah naye pekee ndie mwenye kuruzuku Afya, Ponyo, na Nguvu. diira |
|
|||
|
Asalaam alaykum.
Nakushukuru sana ndugu yangu kwa msaada wako,Mola akupe elimu yenye kheri na barka zaidi ili uzidi kutuelimisha ndugu zako. Kuna neno sikulifahamu naomba unifafanulie "dafi dafi " lina maana gani. Na pia niliwahi kusikia watu wakisema kitunguu thomu kinatibu mba.Unakisaga na kupakaa kichwani..umepata kusikia hii ? mimi sikuwahi kujaribu. Bila kusahau nitajaribu inshaallah kutumia ushauri wako,ahsante sana. Wabillahi at tawfiq, Akhuukum, Abu-Muslim. |
|
|||
|
Quote:
WABILLAHI TAWFEEQ
__________________
Tunamhimidi Allah naye pekee ndie mwenye kuruzuku Afya, Ponyo, na Nguvu. diira |
|
|||
|
Asalaam alaykum
Hata mimi nimesita kutumia hicho kitunguu kwasababu hio ya harufu ndio nikaona kwanza kuuliza uhakika wake kama kinatibu basi itakuwa hapana budi kukitumia,ahsante sana.Umetupa msaada mzuri,hapa tuna kazi ya ku print maelezo yako tu na kuchukua nyumbani.Tunasubiri maana ya neno fenugreek. ALLAH akuepushe na akuondoshee kila maradhi kwa jitihada yako ya kutaka kuwapa nduguzo shifaa. Wabillahi at tawfiq, Akhuukum, Abu-Muslim. |
|
|||
|
Quote:
Inshallah dawa hiyo itakusaidia. Ama baada kuwauliza watu wawili watatu kuhusu Fenugreek wamenipatia jina jipya kabisa , lakini nimeona uzuri niliandike huenda ndio likawa jina lake wanasema inaitwa "Methi"(Meti) naona hili jina la kihindi kuna jina lengine ambalo nalijua ila hili litakuwa gumu kidogo hata hivo huenda mtu akalifahamu kwa jina hilo "Trigonella graecum" alofahamu katika hayo majina 2 tunaomba kama lipo la kiswahili atuandikie. WABILLAHI TAWFEEQ
__________________
Tunamhimidi Allah naye pekee ndie mwenye kuruzuku Afya, Ponyo, na Nguvu. diira |
|
|||
|
Assalam alaykoum!
Itakuwa Jambo la busara saana kama nitaomba Rukhsa Kuchangia Juu ya Dawa ya mba Kichwani!.. Na inshallah Pasi na Khiyana najua nitakuwa nimeruhusiwa. Mimi Ni mmoja wapo kati ya wale waliowahi kupata shida saana juu ya mba! na nilihangaika na kubahatika kupata Tiba Mbali mbali na zikiwemo hizo Alizozitaja Dada Yetu katika Uislamu-DIIRA. na Wengi wamefanikiwa kwa kutumia dawa hizo. Ila Mimi Dawa ilonisaidia ni Habbat Souda na Mafuta ya Nazi. Kinachotakiwa Kufanya ni kuwa Wakati ukienda Kuoga Kichwani Yakupasa Uoshe nywele kwa maji Ya Dafi Dafi( au uvugu vugu) kisha Ukifute kichwa Uzuri sana kiasi Kisibakiwe na Maji maji mengi, Ila nywele ziw zimelainika tu!.. Kisha Unachukua Mafuta ya Nazi (coconut oil) then unaichanganya na Habbat souda( Habbat souda iwe ya Mafuta) yaani ile habbat souda Liquid. kisha unajipakaa kichwani mafuta ya kutosha . Asubuhi na usiku. Inshallah Kwa dawa hiyo ndio itakusaidia pia ikiwa umejaribu dawa zingine hazikukufaa. Kwani mimi navyokwambia hivi nimetumia dawa hiyo na imenisaidia sana. Kuna wengine wanatilia mkazo mafuta ya nazi uyatengeze mwenyewe! uchukue nazi ilokaushwa ukaipika na kuchuja yale mafuta utayoyapata bila kuyazimua na kingine. Al-muradi kila mtu anasema yake, lakini muhimu ni mafuta ya nazi tu. Ahsanteni. Wabillahi Tawfeeq Kama nimekosea naomba kukosolewa. M.A.Alhinai
__________________
Alhamdu lillahi, sifa zake subhana, Mola asiye shabihi, na wapili hana, Ametukuka Ilahi, Hana mke hana mwana |
|
|||
|
Quote:
Shukraan sana kaka yetu!
__________________
Tunamhimidi Allah naye pekee ndie mwenye kuruzuku Afya, Ponyo, na Nguvu. diira |
|
|||
|
Asalaam alaykum
Napenda kutoa shukurani zangu kwa ndugu zangu waliochangia katika mada hii Dada yetu Dira na Kaka yetu M.A Alhinai.Dawa alonielekeza Dada yetu DIRA kwa maradhi haya ya mba imefanya kazi kwani hivi sasa alhamdulillah ninaendelea vizuri kwani siooni ishara yoyote ya mba kichwani mpaka sasa.Nimetumia ndimu kama nilivyoelezwa na nimepata mafaninikio makubwa sana.Na hii ya mafuta ya nazi na haba asauda imo njiani kufanyiwa majaribio kwa mtu mwengine,baada ya muda tutatowa natija yake pia.Kwa hakika shukurani zangu sijui nishukuru vipi na mara ngapi ila kila nikikumbuka hushukuru Mungu.Alhamdulillah,alhamdulillah,alhamdulillah... ...... Mola akupeni jazaa njema duniani na akhera. Kwa hakika tumepata faida kubwa sana tangu kuanzishwa kwa website yetu hii,Mola awape jazaa njema wote waloshiriki katika uanzilishi huu. Wabillahi at tawfiq Akhuukum, Abu-Muslim. |
![]() |
| Bookmarks |
Currently Active Users Viewing This Thread: 1 (0 members and 1 guests) |
|
| Thread Tools | |
|
|
|
||||
| Thread | Thread Starter | Forum | Replies | Last Post |
| Naomba mnijulishe dawa ya kifua. | abdulwaheed | UKUMBI WA AFYA na TIBA | 2 | 17-05-05 |
| naomba dawa ya mafua | lutfy | UKUMBI WA AFYA na TIBA | 13 | 02-03-05 |
| Naomba dawa | yubi | UKUMBI WA AFYA na TIBA | 3 | 15-02-05 |
| naomba dawa au dua!! | slutunga | UKUMBI WA AFYA na TIBA | 4 | 30-01-05 |
| Naomba Dawa | Uislam | UKUMBI WA AFYA na TIBA | 6 | 17-12-04 |