HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA JUMUIYA

 

1. Kufungua Madarasa ya kufundisha Qur - an tukufu.

2. Kufundisha lugha ya kiarabu na nahau yake pamoja na kusoma na kuandika kiarabu.

3. Kuzifanyia matengenezo misikiti mikongwe.

4. Kujenga miskiti mipya .

5. Kununua mabomba ya adhana na mashine zake.

6. Uchimbaji visima kwa ajili ya misikiti na maeneo ya karibu.

7. Ujenzi wa shule ya kiislamu.

8. Kutoa misahafu na vitabu vya hadithi za Mtume (S W A).

9. Kukusanya zakaa na kuzipeleka kwa wale wanaostahiki (nao ni wengi).

10. Kutoa vitabu vya shule na nyenzo nyenginezo.

11. Upatikanaji wa huduma za afya.

12. Kuanzisha mafunzo ya ushoni.

13. Kushiriki katika ujenzi wa nyumba kwa familia maskini.

14. Kuozesha vijana wasiokuwa na uwezo wa gharama za mahari na mahitaji yake.

15. Kuftarisha kwa wanaofunga mwezi wa Ramadhani.

16. Kutoa mavazi kwa wanaohitaji wakati wa sikukuu za iddi.

17. Kuwashughulikia watu wenye ulemavu.

18. Kutoa misaada na kutatua mahitaji ya hali zote ya mayatima.

19. Kunyanyua na kuboresha hali ya maisha ya familia maskini kwa kuanzisha miradi inayozalisha.

20. Kulipa madeni ya baadhi ya familiya maskini.

21. Ununuzi wa magari kwa ajili ya kueneza uislamu na kuwapatia wanafunzi usafiri wa kwenda na kurudi skuli n.k.

Jumuiya ya kiislamu ya kimataifa ya Istiqaama inakukaribisha kwa njia zozote zinazowezekana kuunga mkono juhudi zake kifedha au kimawazo kwa ajili ya kutimiza malengo yake thabiti katika kueneza elimu na kuwasaidia waislamu duniani.

 

Copyright ©2004  Uislam.net