Jumuiya ya Istiqaama ya Kiislam ya Kimataifa

 

Ni Jumuiya isiokuwa ya kiserikali wala ya kibashara ambayo malengo yake ni kuendeleza utamaduni, uchumi, elimu na afya kwa jamii chini ya maadili ya Kiislam.

Nchi mbali mbali imeona iko haja kuwepo taasisi na Jumuiya binafsi ambazo malengo yake kutoa huduma bora kwa jamii.

Hivyo serikali za nchi hizo zinatathmini sana pamoja na kuzitambua huduma zitolewazo na Jumuiya za kibinafsi zenye malengo ya kuinua hali ya jamii na kujenga Taifa kwa jumla.

Chochote katika wema unachokifanya kwa ajili ya nafsi yako, basi ujira (thawabu) wake mkubwa na zaidi utaukuta mbele ya Mwenyezi Mungu.

 Udugu wa kweli sio ududgu wa damu, bali ni udugu wa kiislam, udugu wa dini. Mtume wa Mwenyezi Mungu (S A W) alisema:

 "Muislamu katika mapenzi yao na kuhurumiana ni kama mwili, sehemu yoyote au kiungo chochote kikiumwa, mwili mzima unapata maumivu"

 Mtume (S A W) amepigania Uislamu kwa hali na mali. Masahaba wake pia wamefuata nyayo zake wametupa vyote vilivyomo katika milki yao (mali) ili kuuhami uislamu kwa kuwa utufikie sisi tukiwa katika hali ya kutochafuliwa (safi na nadhifu ).

 Baadaye wakaja wafuasi (Taabiy) na wapiganaji wa kiislamu (Mujahidiin) ambao walitumia mali na kutoa muhanga maisha yao kwa ajili ya kuutangaza na kulingania Uislamu na neno (KALIMAH)(kushuhudia kuwa hapana mola anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu) la Mwenyezi Mungu (ALLAH) walipata heshima na ushindi katika dunia na malipo yao akhera ni pepo.

Enyi ndugu wa kiislamu (wake kwa waume) tumewaita ili muwe pamoja na watu hao wema.

 "… pamoja hao Mwenyezi Mungu amewaweka miongoni mwa Mitume

,wachaMungu , mashahidi, waaminifu na hao ndio marafiki wema".

 Ikiwa kweli unataka kuwa miongoni mwao na kutafuta njia itakayokuongoza kufikia huko, basi sisi Jumuiya ya Kiislamu ya Istiqaama ya kimataifa tunakualika ujiunge nasi kwa kusaidia chochote ambacho Mwenyezi Mungu (S W T) amekukirimu (amekupa) na uchangie katika miradi ifuatayo:- Kama kutoa elimu, kuhifadhi Qur - an tukufu, malezi ya watoto kulingana na tabia, maadili , misingi na silka za kiislamu.

 Mtume (S A W) alisema:

" Yule anayetumia katika njia ya kiislamu analipwa mara mia saba:

"Utajiri haupungui kwa sababu ya kutumia katika njia ya sadaka.

 

Copyright ©2004  Uislam.net