|
Chuo cha Istiqaama
cha Masomo ya Dini ya Kiislamu – Zanzibar ni taasisi ya taaluma ya
mafunzo ya dini iliyo chini ya Jumuiya ya Kiislamu ya Istiqama ya
Tanzania.
HISTORIA
FUPI YA CHUO CHA ISTIQAMA:
Chuo cha Istiqama kimeasisiwa chini ya usimamizi wa Sk. Muhammed bin
Salim
Al Busaidi na Sk. Zahir bin Khalifa Al Alawi mwaka 1415H / 1995AD,
kikafunguliwa awali katika Msikiti wa Istiqama wa Zanzibar, kikiwa na
wanafunzi 32 kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania, walimu 3 na afisa
utawala 1.
Mwaka 1418H / 1998AD Chuo kilihamia kwa muda katika jengo la Madrasat
Lemki ya watoto wa kike, na mwaka 1421H / 2001AD kikahamia katika
makao yake ya kudumu iliyoko Tunguu kiasi kilomita 16 kutoka mjini
Zanzibar, katika ardhi ambayo Tawi la Jumuiya ya Istiqama la Zanzibar
lilijitolea kuinunua mahususi kwa ajili ya mradi wa Chuo cha Istiqama.
Chuo kilipohamia huko Tunguu, majengo yake hayakuwa zaidi ya msikiti,
madarasa, dakhalia (makaazi ya wanafunzi) na nyumba mbili za wageni/walimu.
Baadae ujenzi uliendelea likapatikana jengo la utawala na ofisi za
walimu, jengo la maktaba, jengo la ukumbi wa kulia/mikutano/sherehe,
nyumba za wapisi, na uwanja wa riadha.
AL - ISTIQAAMA AL -
KHAIRIYA
A/C. NO : 03 -
513397 - 02
Oman International
Bank (SAOG)
Mina Al- Fahal (MNF)
- SULTANATE OF OMAN |