(MUKHTASAR) KATIKA MATENDO YA SALA
|
ÞÇá Çááå ÊÚÇáì: "ÃÞã ÇáÕáÇÉ áÏáæß ÇáÔãÓ Åáì ÛÓÞ Çááíá æÞÑÂä ÇáÝÌÑ Åä ÞÑÂä ÇáÝÌÑ ßÇä ãÔåæÏÇ" ÇáÅÓÑÇÁ 78 Anasema Mwenyezi Mungu aliyetukuka: “Shika Sala jua linapo pinduka mpaka giza la usiku, na Qur'ani ya al fajiri. Hakika Qur'ani ya alfajiri inashuhudiwa daima”Israa 78 æÞÇá: "ÍÇÝÙæÇ Úáì ÇáÕáæÇÊ æÇáÕáÇÉ ÇáæÓØì æÞæãæÇ ááå ÞÇäÊíä" ÇáÈÞÑÉ238 Na akasema: “Zilindeni Sala, na khasa Sala ya katikati, na simameni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu nanyi ni wenye kunyenyekea” Al-Baqara 238. Amesema Mtume (SAW): “Funguo za pepo ni sala, na funguo za sala ni tahara” Na akasema pia: “Hakika malaika wanamuombea mmoja wenu dua akiwepo juu ya msala aliosalia ikiwa hajatengua udhu.Ewe Mola mghafirilie madhambi yake, ewe Mola mrehemu” Yanagawanyika matendo ya sala katika vipengele viwili navyo ni: (A) Matendo ya Nyoyo (Moyo). (B) Matendo ya viungo vyote vya mwili. |
|
| (A) Matendo ya Nyoyo (Moyo): | |
|
1. NIA: Na pahali pake ni moyoni, nako ni kutia nia moyoni (Kuhakikisha kwa moyo), kuwa unatekeleza faridha ya sala , kwa kumtii Mwenyezi Mungu. Amesema Mtume (SAW): “Hakika matendo ni nia, na kila tendo ni lile ulilolitilia nia”. 2. IKHLAS (Mtakaso): Nako ni yule mwenye kusali kufanya ikhlas (kumtakasa Mola) juu ya matendo yake yote, na maneno yake yote anayo yanena (anayo yasema), juu ya Mwenyezi Mungu. Na sala bila ya ikhlas inakuwa ni kumdanganya Mwenyezi Mungu. íÞæá Çááå ÊÚÇáì: "æ ãÇ ÃãÑæÇ ÅáÇ áíÚÈ쾂 Çááå ãÎáÕíä áå ÇáÏíä" ÇáÈíäÉ 5 “Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini" Al-Bayyina 5. 3. UNYENYEKEVU: Ndio roho ya sala, na sala bila ya unyenyekevu ni sala yenye udanganyifu juu ya Mwenyezi Mungu. Unyenyekevu ndio nguzo ya sala.Amesema Mtume (SAW): “Kila kitu kina nguzo, na nguzo ya dini ya kiislamu ni sala, na nguzo ya sala ni unyenyekevu”. Na njia ambazo zinasaidia kuwa na unyenyekevu: Ni kutakasa maneno, kutukuza ufalme wa Mola, na kuwa na yakini ya ukamilifu, na kukusanya hima juu ya ibada. |
|
| (B) Matendo ya viungo vyote vya mwili: | |
|
1. KUSIMAMA: Nako ni kusimama sawasawa bila ya kuelemea upande mmoja au kulega lega. Na yawe macho yameelekea pahali unaposujudu au baina ya pahali unaposujudu na sehemu za miguu. 2. TAWJIYH: Sifa yake ni mwenye kusali aseme: (SUBHAANAKA LLAHUMA, WABIHAMDIKA, TABAARAKA S’MUKA, WATAALA JADUKA, WALA ILAHA GHAIRUKA. INNI WAJJAHTU WAJHIYA LILLADHI FATTARA SAMAAWAATI WAL ARDHA HANIIFAN WAMAA ANAA MINA L’MUSHRIKIIN). 3. TAKBIRAT AL-IHRAAM (Takbira ya kuingia kwenye sala): Nayo ni nguzo katika nguzo za sala. Na sala haitimii bila ya hiyo Takbira. Sifa yake ni yule mwenye kusali kusema: (ALLAHU AKBAR). 4. ISTIADHA ( Kujikinga na Shetani) : Nako ni kumuomba Mwenyezi Mungu akulinde na shetani, na inakuwa baada ya TAKBIRAT AL-IHRAAM na kabla ya kuisoma Surat Al-Fatiha (Al-Hamdu) katika rakaa ya mwanzo peke yake. Na sifa yake ni kusema (AUDHU BILLAHI MINA SHAYTANI RRAJIYM). 5. KUSOMA SURAT AL-FATIHA : Nayo ni nguzo katika nguzo za sala, na inamuajibikia mtu kuisoma katika rakaa zote za sala, ikiwa anasali peke yake au anasali sala ya jamaa (maamuma). Na sala haitimii bila ya kusoma sura hii, dalili ni hadithi ya Mtume (SAW): Hakuna sala ila kwa kifunguzi cha kitabu (Surat Al-Fatiha). 6. KUSOMA SURA(baada ya surat Al-Fatiha): Nayo ni Sunna, na unasoma sura katika sala ya faridha, isipokuwa rakaa kumi na moja za sala ya faridha. Nazo ni: Rakaa nne za sala ya faridha ya Adhuhuri. Rakaa nne za sala ya faridha ya Al-Asr. Rakaa ya mwisho ya sala ya Maghrib. Rakaa mbili za mwisho za sala ya Ishaa ya mwisho. Sala zote za Sunna na za Nafila unasoma sura katika rakaa zote za sala. 7. RUKUU: Sifa yake ni mwenye kusali kupinda(kuinamisha) mgongo wake, kwa kutamka Takbira (ALLAHU AKBAR), kuweka mikono yake juu ya magoti yake hali ya kuwa vidole vyake vimetengana, aweke mgongo wake sawasawa, na huku anasema (SUBHANA RABIYA L’ADHYM X 3). Idadi ndogo ya tasbih anayoisema mwenye kusali katika rukuu ni mara tatu. Kisha anainuka (anasimama) kutoka kwenye rukuu mpaka viungo vyote vya mwili virejee mahali pake, huku anasema (SAMIA LLAHU LIMAN HAMIDAH) ikiwa ni Imam au mwenye kusali peke yake. Akisha simama sawasawa anasema (RABBANAA WALAKA L’HAMD). Na ikiwa mwenye kusali ni maamuma hasemi (SAMIA LLAHU LIMAN HAMIDAH), bali anamfuata imamu kwa kusema (RABBANAA WALAKA L’HAMD). 8. SIJDA: Sifa yake ni kwenda mwenye kusali kwenye sijda (kuinamisha kichwa chini mpaka kiguse ardhi) huku anasema (ALLAHU AKBAR), wakati anatanguliza magoti yake, kisha mikono yake, kisha anakutanisha (kuambatanisha) pamoja vidole vyake vya mikono, huku vinaelekea Qibla. Na aweke mikono yake baina ya magoti na masikio, na ncha za vidole ziwe katika masikio. Kisha anaweka kipaji cha uso na pua yake kwenye ardhi, na aweke miguu yake sawa sawa mpaka tumbo za vidole vyake vya miguu viguse ardhi, hali ya kuwa anategemea nguvu za vipaji vyake vya mikono yake kwenye sijda yake. Na mwenye kusali anasema katika sijda yake (SUBHANA RABBIYA L’AALA X 3). Idadi ndogo ya tasbih anayoisema mwenye kusali katika sijda ni mara tatu. 9. KUKAA KITAKO: Nako ni mwenye kusali kukaa kitako sawa sawa na kuunyoosha mgongo sawa sawa, huku amekalia mguu wake wa kushoto na kunyoosha mguu wa kulia huku tumbo za vidole vyake vinagusa ardhi. Na viganja vya mkono wa kulia vinakaa juu ya goti la kulia na viganja vya mkono wa kushoto vinakaa juu ya goti la kushoto. 10. TASHAHHUD (TAHIYAT) YA KWANZA: Nayo ni sunna katika sunna za sala. Sifa yake ni yule mwenye kusali kusema: Attahiyyaatu lillahi wassalawaatu wattayyibaatu. As’salamu alayka ayyuha nnabiyyu warahmatu llahi wabarakaatuh. As’salamu alayna wa alaa ibadi llahi ssaalihin. Ash’hadu an’laa Ilaaha illa llah wa ash’hadu anna Muhammadan abduhu warasuluh. 11. TASHAHHUD (TAHIYAT) YA MWISHO: Anazidisha baada ya maneno ya Tashahud ya mwazo maneno yafuatayo: Allahuma Sali alaa Muhammad wa alaa aali Muhammad kama sallayta alaa Ibrahim wa alaa aali Ibrahim, wabaarik alaa Muhammad wa alaa aali Muhammad kama baarakta alaa ibrahim wa alaa aali Ibrahim fil aalamina innaka hamiidun majiid. Baada ya Tashahud ya mwisho na kabla ya kutoa salaam: Zimekuja riwaya za dua juu ya Mtume Muhammad (SAW), inatakikana mwenye kusali aziombe kabla ya kutoa salaamu (kumaliza sala). Nazo ni: Allahuma inni audhubika min adhaabi l-qabri, wa audhubika min adhabi jahannam wa audhubika min fitnati l’masihi ddajjal, wa audhubika min fitnat l’mahya wal mamaat, wa audhubika mina l’ma’atham wal’maghram. Allahuma innii dhalamtu nafsii dhulman kathiyra, walaa yaghfiru dhunuuba illaa anta, faghfir liy maghfiratan min indik. warhamnii innaka anta l’ghafuru rrahiym. Allahuma ighfir lii maa qadamtu wama akkhartu wa maa asrartu wa maa aalantu wa maa asraftu wa maa anta aalamu bihi minni anta l’muqadimu wa anta l’muakhir, la ilaaha illaa ant. Allahuma innii as’aluka l’jannata wa audhubika mina nnaar. 12. TASLIIM (KUTOA SALAAM): baada ya kumaliza hizi dua, anatoa salaam mwenye kusali akisema (ASSALAMU ALAYKUM) huku anaelekeza uso wake upande wa kulia, kisha anasema (WARAHMATU LLAHI) huku anaelekeza uso wake upande wa kushoto. Pia kuna kauli kuwa kutoa salamu mbili inafaa. Anasema mwenye kusali akitoa salamu: (Assalamu Alaykum Wa Rahmatullah), huku anaelekeza uso wake upande wa kulia. kisha anasema (Assalamu Alaykum Wa Rahmatullah), huku anaelekeza uso wake upande wa kushoto.
|
|
| (C) DUA na ADHKAAR: | |
|
Dua (adhkaar) zilizothibiti kusomwa (kuombwa) baada ya kutoa salaam: Inatakikana mwenye kusali baada ya kutoa salaam (akimaliza kusali) aelekee kwa Mwenyezi Mungu kwa kuomba dua. Zifuatazo ni baadhi ya dua zilizothibiti juu ya jambo hili: ● Kusoma AYATU L’KURSI. ● kusoma SURATI L-FALAQ na SURATI NAAS. ● Subhaana llah (mara 33), Al-hamdulillah (mara 33), AllahuAkbar (mara33 au mara34). Unasema baada ya kukamilisha. La Ilaaha illa llahu wahdahu laa shariyka lah, lahu l’mulku wa lahu l’hamdu wa huwa alaa kuli shay’in qadiyr (mara 100). ● Astaghfiru llahu l’adhiym wa atuubu ilayhi (mara 3). ● Allahuma anta ssalaam wa minka ssalaam tabarakta yadha l’jalaal wal’ikram. ● La Ilaaha illa llaahu wahdahu laa shariyka lah, lahu l’mulku wa lahu l’hamdu wa huwa alaa kulli shay’in qadiyr. Allahuma la maani’a lima aatayta wala mu’uttiy limaa mana’ata, wala raadda limaa qadhayta walaa yamnau dha l’jiddi minka l’jadd. ● Allahuma ghfir lii maa qadamtu wamaa akhartu wamaa asrartu wamaa aalantu wamaa asraftu wamaa anta aalamu bihi minni, anta l’muqadimu wa anta l’muakhiru laa Ilaaha illaa anta. ● La Ilaaha illa llahu wahdahu laa shariyka lah, lahu l’mulku wa lahu l’hamdu wa huwa alaa kuli shay’in qadiyr. Walaa hawla walaa quwata illaa billaah, wala na’abudu illaa iyyah, lahu niimatu walahu l’fadhlu walahu thanau l’husna la ilaha illa huw, mukhlisiyna lahu ddiin walaw kariha l’kaafiruun. ● Allahuma ainniy alaa dhikrika wa shukrika wa husni ibaadatik (mara 3). ● Rabii qinnii adhaabak yawma tab’ath ibaadik. ● Allahuma innii audhubika mina l’jubni wa audhubika min ardhali l’umr wa audhubika min fitnati dduniya, wa audhubika min adhaabu l’qabr. ● Allahuma ajirni mina nnaar (mara 7 baada ya Al-Fajr na Al-Maghrib) ● Allahuma inni as’aluka I’lman naafia, wa amalan mutaqabala warizqan tayyiba (mara 3 baada ya Al-Fajr) |
|
|
Imetayarishwa na: www.uislamu.net |
|
|
|
|
Copyright ©2005 Uislamu.net |