|
|
MTAZAMO WA KISHERIA
KUHUSU MASUALA TAFAUTI YA UKIMWI
(MISCELLANEOUS RELIGIOUS VIEWS ON AIDS) |
ÈöÓúãö Çááåö ÇáÑøóÍúãäö ÇáÑøóÍöíúãö
ZANZIBAR
CHILDREN’S FUND
ZCF
äóÏúæóÉ ÃóÆöãøóÉö ÇáãóÓóÇÌöÏö æóãõÏóÑøöÓöíú ÇáßóÊóÇÊöíúÈö
ÇáÞõÑúÂäöíøóÉö ãöäú ßóÇÝøóÉö ãõÍóÇÝóÙóÇÊö ÇáÌóÒöíúÑóÉö ÇáÎóÖúÑóÇÁö Ýöíú
ãõßóÇÝóÍóÉö æóÈóÇÁö ÇáÅöíúÏúÒ ÊóÍúÊó ÅöÔúÑóÇÝö ãõäóÙøóãóÉö ÑöÚóÇíóÉö
ØõÝõæúáóÉö ÒöäúÌöÈóÜÜÇÑó
WARSHA YA MAIMAMU NA
WALIMU WA MADRASA
KUTOKA WILAYA ZA PEMBA
JUU YA
KUPAMBANA NA UKIMWI
MEI, 2005
ÇáãóäúÙõæúÑõ ÇáÔøóÑúÚöíøõ
Ýöíú ãõÎúÊóáóÝö ÇáãóÓóÇÆöáö ÇáãõÊóÚóáøöÞóÉö
ÈöãóÑóÖö ÝõÞúÏóÇäö ÇáãóäóÇÚóÉö
((ÇáÅöíúÏúÒ))
MTAZAMO WA KISHERIA
KUHUSU MASUALA TAFAUTI YA UKIMWI
(MISCELLANEOUS RELIGIOUS VIEWS ON AIDS)
IMETAYARISHWA NA SHEIKH:
KHALFAN SULEIMAN TIWANIY.
KUTOKA TAWI LA ISTIQAMA,KUSINI-PEMBA.
UTANGULIZI:
Inaeleweka fika kuwa UKIMWI ni janga
lililoikumba dunia yote;hasa ikizingatiwa kuwa maradhi haya hayana ubaguzi
wala uchaguzi,humsibu yoyote yule pasi na kujali rangi yake,jinsia yake,dini
yake,madhehebu yake,hali yake ya kiafya au ya kijamii,pia hayajali
ucha-mungu wa mtu au uachaji-mungu wake,kwa kusema hivyo imekuwa ni kama
jinamizi sugu linawarusha watu roho,kwa kutoa picha halisi si vibaya kama
tukisema kuwa maradhi haya ni kama POPO-BAWA linapoingia mtaani hurufaisha
nyoyo za watu wote,na labda ndio maana walimwengu wote waka”taharrak” katika
ngazi za kimataifa na kitaifa na kukaa pamoja kujadili njia za kuutokomeza
ugonjwa huu au kuupunguzia kasi yake ya uteketezaji na uangamizaji.
Kwa kuwa walimwengu wana imani kubwa na dini
zao,na zaidi pale wanapofikwa na masaibu,kwa hivyo imeonekana kuwa dini ina
nafasi kubwa katika kutekeleza jukumu hilo kupitia kwa viongozi wake katika
mahafali zake tafauti,hususan kwa vile kujitokeza katika jamii zao masuala
kadha yanayohitajiwa kupatiwa fatawa za kisheria.Hapa nimejaribu kukusanya
baadhi ya masuala hayo -angalia orodha mwisho -na kuyapatia ufumbuzi kwa
mtazamo wa wataalamu wa sheria.
(1)-HUKUMU
YA KUTUMIA MIPIRA (CONDOMS):
Mipira (Condoms)ni kitu kama soksi ya
plastiki nyembamba ambayo huvaliwa katika uume wa mtu, ambayo huzuia
kuanguka kwa maji ya uzazi katika ‘rahim’, condoms imekuwa ni kichochezi
kizuri cha zina,Uislamu hauhamasishi kabisa utumiaji wa mipira hiyo
((ÇáÑøöÝóÜÜÇá)) hasa ukizingatia
hadithi isemayo:
((ÇäúßöÍõæúÇ ÇáæóáõæúÏó æóÇáæóÏõæúÏó¡ÝóÅöäøöíú ãõßóÇËöÑñ Èößõãú ÇáÃõãóãó
íóæúãó ÇáÞöíóÇãóÉö)) yaani: ((Oeni
mwanamke mwenye kizazi,mwenye kupenda,kwani mimi nitajinata mbele ya uma
nyengine (kwa wingi wa uma wangu) siku ya kiama)).
Hata hivyo itajuzu kutumia mipira hiyo
katika hali za dharura zinazokubalika
kisheria,
kama vile mpango wa uzazi wa majira,
au kwa kuhofia kuambukizana maradhi iwapo mmoja kati ya mume au mke kasibiwa
na moja ya maradhi yanayoambukiza,na Allah ndie anayejua zaidi.
(2)-HUKUMU
YA KUBEBA MIMBA KWA ALIYESIBIWA:
Dini ya Kiislamu inachunga kupatikana kizazi
imara na inausia kufanya hivyo pindi ikiwezekana,amesema Mtume (s.a.w):
((ÇáãõÄúãöäõ
ÇáÞóæöíøõ ÎóíúÑñ¡æóÃóÍóÈøõ Åöáóì Çááåö ãöäó ÇáãõÄúãöäö ÇáÖøóÚöíúÝö¡æóÝöíú
ßõáøò ÎóíúÑñ))
yaani:((Muumini mwenye nguvu ni m-bora na anapendwa zaidi na Allah kuliko
Muumini dhaifu,na wote wana kheri)).
Sasa
ikithibiti kuwa kuna uwezakano mkubwa kwa Mama muathirika kuweza kubeba
mimba salama basi itakua hakuna ubaya,kinyume cha hivyo itakatazwa
kuchukua mimba,na Allah anajua zaidi.
(3)-HUKUMU
YA KUHARIBU MIMBA KWA ALIYESIBIWA:
Kuharibu au kutoa mimba
((ÇáÅöÌúåóÜÇÖ))
kwa kuhofia kuwa mtoto alietumboni ataathirika kimaumbile kwa vile mama yake
ni muhanga wa Aids ni kitu kisichokubalika, Allah S.W amepiga marufuku
kuua,na mtoto akishapuliziwa roho,huwa ni nafsi iliyoharamika kuihiliki.Na
kwa kuwa Allah ameshamleta basi hatuna njia ya kumuangamiza. Na mtu hana
jukumu juu ya kile kilichoko tumboni na kinachotokea ndani yake kwani viumbe
vyote vinasibiwa na mabalaa. Mtu huwajibika na hubeba jukumu pale
anapokusudia uadui. Hivyo kuitoa mimba ni kufanya uadui,kwa hivyo atakayetoa
mimba atawajibika kwa kitendo hicho mbele ya Allah.
(4)-HUKUMU YA MAINGILIANO YA KAWAIDA NA-ALIYESIBIWA:
Mtu aliesibiwa na maradhi ya Ukimwi ni kama
mtu mwengine yoyote yule,ingawa Aids ni miongoni mwa maradhi yenye
kuambukiza (Contagious deseases),lakini kwa vile njia za kuambukizana
hazitokani na maingiliano ya kawaida (Casual contact) kwa hivyo itakuwa
hakuna ubaya kushirikiana nae kimasomo, kibiashara na katika nyanja nyengine
za kimaisha,na kama Mgonjwa kaathirika sana akawa anavuja kila pahala kiasi
cha kutishia amani kwa wengine hapo atapaswa mgonjwa huyo kujitenga na watu
ili asiwaambukize wengine,kasema Mtume (s.a.w): ((áÇó
ÖóÑóÑó¡æóáÇó ÖöÑóÇÑó))
yaani:((Hakuna kujidhuru wala
kudhuriana)),na Allah anajua zaidi.
(5)-HUKUMU
YA MWENYE KUAMBUKIZA WENZAKE UGONJWA WA AIDS KWA MAKUSUDI:
Kitendo cha kumuambukiza kwa makusudi
binaadamu mwenzako maradhi ya aina yoyote ni kitendo cha kinyama na cha
kishenzi seuze uambukizaji wa Ukimwi, hili likitokea itaangaliwa,ikiwa
kitendo hicho kitapelekea kifo kwa upande wa pili basi hukumu ya kulipa
kisasi itatumika na ikiwa si hivyo basi Hakimu ndio ataangalia adhabu gani
inafaa kutiwa Mtendaji huyo, kwani hii itaingia katika hukmu ya
((ÇáÊøóÜÚúÜÒöíÜúÑ))
na Allah ni mjuzi wa yote.
(6)-HUKUMU
YA TOBA YA ALIEATHIRIKA:
Allah anapokea toba ya mja wake madhali
haijafika wakati wa kutaka kukata roho na ndiyo akasema:
{Þõáú íóÇ ÚöÈóÇÏöíó ÇáøóÐöíäó ÃóÓúÑóÝõæÇ Úóáóì ÃóäÝõÓöåöãú áóÇ ÊóÞúäóØõæÇ
ãöä ÑøóÍúãóÉö Çááøóåö Åöäøó Çááøóåó íóÛúÝöÑõ ÇáÐøõäõæÈó ÌóãöíÚÇð Åöäøóåõ
åõæó ÇáúÛóÝõæÑõ ÇáÑøóÍöíãõ }ÇáÒãÑ53
yaani:((Waambie waja wangu waliofanya dhambi
msikate tamaa na rehma ya Allah. Hakika Allah anasamehe dhambi zote kwani
yeye ni mwingi wa kutoa misamaha na mwenye kurehemia)).
Pia imekuja katika hadithi kuwa:((Hakika
Allah ananyoosha mkono
wake usiku ili kupokea toba kutoka kwa waliofanya madhambi wakati huo pia
hunyoosha mchana kwa ajili ya watakaotenda dhambi kwa mchana huo)). na
kunyoosha hapa imekusudiwa kukubali.. na Allah anajua zaidi.
(7)-HUKUMU
YA KUMUUA ALIEATHIRIKA KWA HIARI YAKE KWA NIA YA KUMPUMZISHA!!:
Inaeleweka tosha kuwa Aids inatesa vibaya
kiasi cha kuyatamani mauti,na katika miaka ya karibuni tu katika nchi za
Ulaya ulitokezea mripuko wa baadhi ya madaktari kuwauwa magonjwa
wanaosumbuliwa na maumivu makali kwa kuwatoga sindano za vifo kwa nia ya
kuwapumzisha!
Maulamaa walilijadili suala hili kwa kina na
wakaona kuwa ni haramu kuiua nafsi ya mtu pasi na haki, hata ikiwa ni kwa
ridhaa yake,kasema Allah:
{..æóáÇó ÊóÞúÊõáõæÇú ÃóäÝõÓóßõãú Åöäøó Çááøåó ßóÇäó Èößõãú ÑóÍöíãÇð }ÇáäÓÇÁ29
yaani: ((Wala msiziuwe nafsi zenu
hakika Allah kwenu ni mwenye rehema).
Na
Mtume (s.a.w) amesema:
{æóãóäú
ÊóÍóÓøóì ÓõãøðÇ ÝóÞóÊóáó äóÝúÓóåõ¡ÝóÓõãøõåõ Ýöíú íóÏöåö íóÊóÍóÓøóÇåõ Ýöíú
äóÇÑö Ìóåóäøóãó ÎóÇáöÏðÇ ãõÎóáøóÏðÇ ÝöíúåóÇ ÃóÈóÏðÇ}
yaani: ((..na atakaye kunywa sumu
akajiua,sumu yake atakuwa nayo mkonono mwake anaichubua katika moto wa
Jahannam milele na daima)).
Hivyo inapaswa mgonjwa wa Aids amche Allah
na avumilie kwani kujiua kutampeleka katika adhabu kuu zaidi.
Pia waliosalimika wamvumilie mgonjwa
aliyefikwa na mtihani huo, kwani Allah huwaonja kwa dhiki na shida na
wengine kwa raha na neema.
N.B:Kwa
maana hiyo Daktari akimtoga sindano ya kifo mgonjwa kwa makusudi itakuwa
kauwa,na hivyo hivyo ikiwa atamtilia dawa ili ajiue..na Allah anajua zaidi.
(8)-HUKUMU
YA KULEA MAYATIMA WA UKIMWI:
Uyatima ni kitu cha kisikitisha sana,hususan
kwa jinsi jamii zinavyomtizama Yatima kama ni kiumbe kilichopungukiwa na
mtunzaji,kwa hivyo mara nyingi Mtoto yatima huonewa na kudhulumiwa,Sheria ya
Kiislaamu imelipa suala la mayatima kipa umbele sana,Mtume (s.a.w) amesema:
((ÃóäóÇ æóßóÇÝöáõ ÇáíóÊöíúãö Ýöíú ÇáÌóäøóÉ ö ßóåóÇÊóíúäö)) æóÃóÔóÇÑó
ÈöÃõÕúÈõÚóíúåö:ÇáÓøóÈóÇÈÉ óö æóÇáæõÓúØóì))
yaani:(Mimi na Mtunzaji wa Yatima tutakuwa
katika Pepo kama vidole hivi viwili, anasema hayo huku akiambatanisha kidole
chake cha shahada na kile cha kati pamoja,pia Allah kawasimanga wale
wanaowasuta mayatima kwa kusema:
{ÃóÑóÃóíúÊó ÇáøóÐö í íõßóÐøöÈõ ÈöÇáÏøöíúäöó ÝóÐóáößó ÇáøóÐöí íóÏõÚøõ
ÇáúíóÊöíãó }ÇáãÇÚæä2
((Jee,umemuona yule anayekadhibisha
dini,huyo ni yule anayemsuta Yatima..)).
Kwa ujumla suala la kuwatunza Mayatima
katika dini lina umuhumi bayana,Yatima huyo awe wa karibu au wa mbali,huyo
ni Yatima wa kawaida wachilia mbali Yatima wa Ukimwi ambaye anahitaji
matunzaji zaidi.. na Allah anajua zaidi.
(b):JEE
INAFAA KULEA YATIMA WA UKIMWI WA ZINA?:
Kuna tetesi katika ndimi za
watu kuwa mtoto wa zina ni muovu na hafai kuoa wala kuolewa na hatakasiki na
uharamu wake mpaka kizazi chake cha saba (seventh generation),tetesi hizo
zinaenezwa kwa
kutegemea hadithi inayomsifu mtoto wa zina
kuwa:
((åõæó
ÔóÑøõ ÇáËøóáÇóËóÉö)).
yaani:(Yeye ni mbaya wa watatu)),ikimaanisha
baina ya Mzinifu,Mama na Mtoto mwenyewe,na katika riwaya nyengine imekuja:
((æóáóÏõ ÇáÒøöäóÇ áÇó íóÏúÎõáõ ÇáÌóäøóÉó))
yaani: ((Mtoto wa zina haingii Peponi))...Lakini Watalamu wa Hadithi
wamezidhoofisha hadithi hizi,kwani zinapingana na Aya za Qur-ani,kama ile
aya isemayo:
{æóáÇó ÊóÒöÑõ æóÇÒöÑóÉñ æöÒúÑó ÃõÎúÑóì}
((Haitobeba nafsi madhambi ya nafsi
nyengine)),na pia hadithi hizi zinapingana na akili,kwani kama ni makosa
basi ni ya Wale wawili waliokubaliana kufanya ‘fahishatu-zinaa’ na sio ya
Yule Mtoto aliyekuja bila ya khiari.
Kwa hivyo hakuna ubaya bali ni fadhila
kubwa sana
kumtunza mtoto wa aina hiyo,bali kuna malipo na Allah anajua zaidi.
(9)-HUKUMU
YA NDOA YA WALIOSIBIWA:
Kisheria hakuna ubaya kwa waliosibiwa
kuoana,hasa tukizingatia kuwa ndoa ina malengo mengi,kati ya hayo ni:
(a):Kujenga familia.
(b):Kukata shahwa.
(c):Kupata heshima katika jamii,n.k.
Na kwa vile ndoa ya wasibiwa itawakidhia
haja zao,basi pia itachangia kwa kiasi kikubwa kutoenea kwa maradhi hayo
mabaya kwa kupitia milango ya nyuma (unlawful sexual intercourse),kwa ajili
hiyo hakuna kipingamizi cha sheria kuhusiana na ndoa hiyo.
(10)-HUKUMU
YA KUDAI TALAKA KUTOKA KWA MUATHIRIKA:
Kama mwanamke atabaini kuwa mumewe kasibiwa
na Aids mapema kabla ya yeye kuambukizwa,basi Wanavyuoni wameonelea kuwa ni
haki ya mwanamke huyo kudai talaka yake,na kama mume atagoma kutoa
talaka basi Mahkama itamuachisha kwa nguvu,kwani hii itaingia katika milango
ya kifiqhi ya dosari zinazopelekea mke na mume kufarikiana..Laa
kama mwanamke ataridhia kuendelea na mumewe hivyo-hivyo ili kulea watoto wao
pamoja basi pia inakubalika kisheria..na Allah anajua zaidi.
(11)-HUKUMU
YA MAMA MUATHIRIKA KUMNYONYESHA MWANAWE:
Hapo nyuma ziliwahi kutoka fatwa kuwa hakuna
ubaya kwa Mama muathirika kumnyonyesha mwanawe,kwa kutegemea Kanuni ya
Kifiqhi isemayo:
((ÇÓúÊöÕúÍóÇÈ ÍóÇáóÉö ÇáÃóÕúáö)),yaani:
((Kwenda sambamba na hali ya asili)),lakini baada ya Sayansi ya Tiba
kuthibitisha kuwa mama anamuambukiza mwanawe kwa njia ya kunyonyesha,kwa
hiyo italazimika kutafuta njia nyengine kama vile kukodi Mnyonyeshaji
au kutumia maziwa ya ng’ombe,mbuzi n.k. au maziwa ya makopo..na Allah ndie
anaejua zaidi.
(12)-JEE
UKIMWI UNA DAWA KWA MTAZAMO WA KISHERIA?:
Ukimwi ni maradhi, na kisheria inaaminika
kikamilifu kuwa una dawa,imebakia kuwa haijajuilikana tu,hii ni kutokana na
hadithi isemayo:
((ãóÇ
ÃóäúÒóáó Çááåõ ÏóÇÁð ÅöáÇøó æóÃóäúÒóáó ãóÚóåõ ÏóæóÇÁð))
Yaani:((Allah hakuleta maradhi ispokuwa
kaleta na dawa yake)),na katika baadhi ya riwaya imekuja:
((Úóáöãóåõ
ãóäú Úóáöãóåõ¡æóÌóåöáóåõ ãóäú Ìóåöáóåõ))
((Ameijua alieijua,na hakuitambua
aliekuwa-hakuitambua)),pia imekuja kwa lafdhi ya:
((áößõáøö ÏóÇÁò ÏóæóÇÁñ¡ÝóÅöÐóÇ ÃõÕöíúÈó ÏóæóÇÁõ ÇáÏøóÇÁö ÔõÝöíó ÈöÅöÐúäö
Çááåö))
yaani: ((Kila maradhi yana dawa,na
ikipatikana dawa ya maradhi,hupoa kwa idhini ya Allah)).
(13)-
KUSHIRIKIANA NA WASIOKUWA WAISLAMU KATIKA
KUPAMBANA NA JANGA HILI:
Ni jambo linaloeleweka tosha kuwa Uislamu ni
dini iliyokamilika,na ina hukumu zake na hikma zake za kiiungu zisizoweza
kubadilishwa,sasa vipi leo waislamu washirikiane na wasiokuwa waislamu
katika kupambana na janga hili?
Hili ni suala nyeti ambalo hukanganya sana
vichwa vya baadhi wa Waislamu..
Kwa ufupi suala hili itakuwa halina ubaya
pindi ikiwa lengo ni kupambana na “adui fulani wa pamoja”
((ãõßóÇÝóÍóÉ ÇáÚóÏõæøö ÇáãõÔúÊóÑóßö)),vigezo
vya jambo hili vinapatikana katika kitendo cha Mtume (s.a.w)alipoweka
mkataba na Mayahudi kuilinda Madina kutokana na adui wa nje,pia pale
alipomkodi Mushriki mmoja wa Makka kumpeleka Madina kupitia njia za
kienyeji,na pia pale alipokuwa Madina mara nyengine alikuwa akiwaandikia
barua baadhi wa Washrikina wa Makka wamzawadie Maji ya Zamzam,na Allah ndie
ajuaye zaidi.
(14)-SUALA
LA KUPIMA KABLA YA NDOA:
Hapana shaka njia moja itakayopelekea
kupunguza uzagaaji wa maradhi ya Aids kwa wingi ni suala la kupima kabla ya
kufunga ndoa,na kwa vile suala la afya lina nafasi kubwa katika dini,kwa
nini isiwe kupima ni sheria ya lazima kabla ya ndoa? Wengine hudadisi.
Jawabu ni kuwa ndoa ina sharti zake maalumu
za kusihi kwake,na suala la kupima halimo katika sharti hizo,lakini Kiongozi
wa nchi akiona kuna maslaha ya kulipa suala hili uzito basi nafasi hiyo iko
wazi katika dini hasa tukizingatia zile kawaida (laws)za kifikhi zisemazo:
((ãóÇ áÇó íóÊöãøõ ÇáæóÇÌöÈõ ÅöáÇøó Èöåö¡Ýóåõæó æóÇÌöÈñ ãöËúáõåõ))
yaani: ((Wajibu isioweza kutimia ispokuwa kwa kupatikana kitu Fulani,basi
kitu hicho pia itakuwa kuna uwajibu kupatikana)),kwa maana ikiwa hatutowezo
kuokoa maisha ya wanaotaka-kuoana ispokuwa kwa kuwapima basi itabidi
kuwapima,na kaida nyengine ni ile isemayo:
((ÇáÖøóÑõæúÑóÇÊõ ÊõÞóÏøóÑõ ÈöÞóÏóÑöåóÇ)),yaani:
((Dharura zinaangaliwa vile zilivyo)),kwa maana ikiwa itakuwa ni mtindo wa
watu kuambukizana maradhi wakati wa ndoa basi sheria inaweza kuchukua hatua
zinazofaa kuhusiana na upimaji kabla ya ndoa.
(15)-MWENYE
AIDS ATIZAMWE KWA JICHO GANI?:
Awali hatuna budi tufahamu kuwa Aids ni
maradhi yanayoweza kumsibu mtu yoyote na kwa wakati wowote,huwapata wengine
kama ni adhabu,amesema Allah:
((æóãóÇ ÃóÕóÇÈóßõãú ãöäú ãõÕöíúÈóÉò¡ÝóÈöãóÇ ßóÓóÈóÊú ÃóíúÏöíúßõãú)),yaani:
((Msiba wowote utakaokupateni ni kwa yale yaliyochumwa na mikono yenu)),na
kwa ile hadithi isemayo:
((ãóÇ
ÙóåóÑó Ýöíú Þóæúãò ÇáÒøöäóÇ Ãóæú ÇáÑøöÈóÇ ÅöáÇøó ÃóÍóáøõæúÇ ÈöÃóäúÝõÓöåöãú
ÚóÐóÇÈó Çááåö)),yaani: ((Haitodhiri
katika jamii zina au riba ela hujisababishia adhabu ya Allah)).
Na wengine hupatwa na maradhi haya kama ni
mtihani ili Allah awalipe kheri pindi wakifanikiwa,kasema Bwana Mtume
(s.a.w.):
((ãóäú
ÃóÑóÇÏó Çááåõ Èöåö ÎóíúÑðÇ íõÕöÈú ãöäúåõ))
yaani: ((Anaemtakia Allah kheri basi
humuonja kwa mitihani)).
Kwa hivyo si busara kumtazama aliesibiwa
kama ni mzinifu,na hata kama itathibiti hivyo haina maana ya kuacha kumpa
nasaha na kumuwaidhi na kumuombea hidaya,tukiangalia sira ya Mtume Muhammad
(s.a.w) utakuta alikuwa akiwafanyia ihsani wale waliokuwa wakimkera,na hata
Qur-ani imewaekea wale watu waliokuwa na imani dhaifu fungu la zaka ili
kuimarisha imani zao,wao walijuilikanwa kwa jina la
((ÇáãõÄóáøóÝóÉõ ÞõáõæúÈõåõã))
,na imekuja katika athari kwamba
Mtume (s.a.w.)alikua akiomba dua kwa kusema:
((Çááøóåõãøó
ÃóÚöÒøó ÇáÅöÓúáÇóãó ÈöÃóÍóÏö ÚõãóÑóíúäö)),yaani:
((Yaa-Rabbi,Upe nguvu uislamu kwa mmoja kati ya Omar wawili)),akimaanisha
Omar ibnul-Khatt’aab au Amruu ibnu Hishaam (Abu jahli),dua ikajibiwa
akasilimu Omar bin Khatt’aab.
Siasa hii ndio iliyopelekea leo Uislamu kuwa
na mamilioni ya wafuasi la si-hivyo dini hii ingalipotea..Tabaan,Mzinifu
akidhihirisha inadi na uadui basi hadithi ziko nyingi zinazofahamisha namna
ya kumtendea.Inatosha kutaja hadithi moja katika mnasaba huu,ni ile
inayosema:
((ãóäú
ÑóÃóì ãöäúßõãú ãõäúßóÑðÇ ÝóáúíõÛóíøöÑúåõ ÈöíóÏöåö¡ÝóÅöäú áóãú íóÓúÊóØöÚú
ÝóÈöáöÓóÇäöåö¡ÝóÅöäú áóãú íóÓúÊóØöÚú ÝóÈöÞóáúÈöåö¡ æóÐóáößó ÃóÖúÚóÝõ
ÇáÅöíúãóÇäö)) yaani: ((Yoyote
atakayeona ubaya basi na auondoshe kwa mkono wake,ikiwa hakuweza augeuze kwa
ulimi wake na kama hakuweza basi kwa moyo wake,na huo ni udhaifu wa
Imani))..na kuna aya nyingi za Qur-ani zinazoweza kutumika katika mnasaba
kama huu..Wallahu A’alam.
(16)-
UMUHIMU WA HABARI KATIKA UISLAMU:
Yoyote anayefahamu yaliyomo katika Qur-ani
japo kidogo atajua umuhimu wa habari katika Uislamu,inatosha kukumbuka kisa
cha Nabii Suleiman na Ndege wake “Hud-hud”, pia Qur-ani yote ni visa vya
Mitume waliotangulia ambavyo kutokana na umuhimu wake Allah alimsimulia
Mtume wake,akamwambia:
((äóÍúäõ
äóÞõÕøõ Úóáóíúßó ÃÍúÓóäó ÇáÞóÕóÕó ÈöãóÇ ÃóæúÍóíúäóÇ Åöáóíúßó åóÐóÇ
ÇáÞõÑúÂäó¡æóÅöäú ßõäúÊó ãöäú ÞóÈúáöåö áöãöäó ÇáÛóÇÝöáöíúäó)).
Kwa hivyo hapana budi Waislamu hasa Mashekhe
na Walimu wa vyuo watumie nafasi zao kuelimisha jamii madhara ya majanga
tafauti yanayotokea Ulimwenguni likiwamo suala la UKIMWI.
Êóãøó ÈöÍóãúÏöÇááåö
.....ÃóÚóÏøóåõ áóßõãú ÎóáúÝóÇä Èúä ÓõáóíúãóÇä ÇáØøöÜÜíúÜÜæóÇäöÜÜíú
18/ÑÈíÚ ÇáËÇäí/1426åÜ ÜÜÜÜ 27/ãÇíæ/2005ã
MASUALA YA KUJIPIMA
(1)-Kwa
nafasi yako kama Imamu au Mwalimu,Jee unahisi kuna haja ya kuweka sheria ya
lazima ya kupima Aids kabla ya ndoa,kama jawabu ndio au siyo,orodheza sababu
zako.
(2)-
Taja njia ambazo Maimamu na Walimu hutumia katika kulielezea suala la
Ukimwi,na kwa kiwango gani hufanikiwa na yepi matatizo yanayowakumba katika
kufanikisha suala hilo?
(3)-
Kwa mtazamo wako,kwa kiwango gani Uislamu umechangia kupunguza janga la
Ukimwi? Eleza kwa kifupi kwa njia ya madondoo.
ü
YALIYOMO
(1)-HUKUMU
YA KUTUMIA MIPIRA (CONDOMS).
(2):HUKUMU
YA KUBEBA MIMBA KWA ALIYESIBIWA.
(3):HUKUMU
YA KUHARIBU MIMBA KWA ALIYESIBIWA.
(4):HUKUMU
YA MAINGILIANO YA KAWAIDA NA ALIYESIBIWA.
(5):HUKUMU
YA MWENYE KUAMBUKIZA WENZAKE KWA MAKUSUDI.
(6):HUKUMU
YA TOBA YA ALIEATHIRIKA.
(7):HUKUMU
YA KUMUUA ALIEATHIRIKA KWA HIARI YAKE NIA YA KUMPUMZISHA!!
(8):HUKUMU
YA KULEA MAYATIMA WA UKIMWI.
(9):HUKUMU
YA NDOA YA WALIOSIBIWA.
(10):HUKUMU YA KUDAI TALAKA KUTOKA KWA MUATHIRIKA
(11):HUKUMU YA MAMA MUATHIRIKA KUMNYONYESHA MWANAWE.
(12):JEE
UKIMWI UNA DAWA KWA MTAZAMO WA KISHERIA?
(13)-KUSHIRIKIANA NA
WASIOKUWA WAISLAMU KATIKA KUPAMBANA NA JANGA HILI
(14)-SUALA LA KUPIMA KABLA
YA NDOA
(15)-MWENYE AIDS ATIZAMWE
KWA JICHO GANI?
Sayansi ya tiba mpaka sasa inaona kuwa mama muathirika hawezi
kumuambukiza mwanawe kwa njia ya kumnyonyesha,kwa mintarafu hii itakuwa
hakuna haja kisheria kumzuia mama kumnyonyesha mwanawe, hii inaingia katika
sheria
((ÇÓúÊöÕúÍóÇÈö ÍóÇáóÉö ÇáÃóÕúáö)) ispokuwa pale tu Daktari
atakaposhauri kutofanya hivyo kwa kuchunga mambo fulani-fulani,au kwa kuja
tafiti mpya.. na Allah anajua zaidi.
(16)-NJIA GANI AMBAZO UISlAMU UMEZITOA KAMA
NI SULUHISHO KATIKA KUTOKOMEZA AU KUPUNGUZA JANGA LA AIDS?
Kujihadhari na UKIMWI
Endapo atapata vurusi vya ukimwi mmoja kati
ya mume au mke bila kumjulisha mwenzake kuhusu ugonjwa
ni njia ipi ya kufanya ili kuunusuru upande
mwingine uliosalimika au kwa maana nyingine je, inafaa kukutana kimwili
baina yao?
Jawabu: Bismillah Rrahmani Rrahiim. Kwa
kweli katika Uislamu kinga ni jambo litakikanalo na ndio maana ya kuwekwa
sheria kuchukua hadhari na kujikinga na njia zote zinazosababisha magonjwa
na maangamizi. Imekuja katika hadithi amri ya kumkimbia (kumuepuka) mwenye
ukoma kama namna umkimbiavyo simba na ziko hadithi nyingi zinazoelezea
kuchukua hadhari ya ugonjwa wa kuambukiza. Hivyo anapaswa watu wote
kujikinga na maradhikama haya.
Amesema Jabir bin Abdi-llah:
((ßõäøóÇ äóÚúÒöáõ Úóáóì ÚóåúÏö ÑóÓõæúáö Çááåö Õóáøóì Çááåõ Úóáóíúåö æóÂáöåö
æóÓóáøóãó æóÇáÞõÑúÂäõ íóäúÒöáõ¡æóáóæú ßóÇäó ÔóíúÆðÇ íõäúåóì Úóäúåõ áóäóåóì
Úóäúåõ ÇáÞõÑúÂäõ)).
yaani: ((Tulikuwa tukimwaga nje wakati wa
Mtume (s.a.w) na Qur-ani inateremka,na ingalikuwa ni jambo la kukatazwa
ingalilikataza Qur-ani)),maneno haya yanatoa mwanga
kuhusiana na matumizi ya
- N.B:Gazeti moja maarufu la Misri lilitawanya Fatwa ya
Mufti Mkuu wa Nchi hiyo Sh.Nasr Farid Wassel inayosema kuwa Sigara ni
katika madhambi makuu,na kutokana na madhara yake kuwa ni mabaya na
yenye kudhuru wengine ameoneleo kuwa ni haki kwa mke kudai talaka kutoka
kwa mumewe mvutaji,alikaririwa akisema: ((Madhara yatakayosababishwa na
Talaka hayawezi kuzidi bali hata kufikia nusu ya madhara
yanayosababishwa na Sigara)),Sh.Farid aliwahi kutunukiwa zawadi na WHO
((ãõäóÙøóãóÉõ ÇáÕøöÍóÉö ÇáÚóÇáóãöíøóÉö))
kwa jitihada zake za kupambana na Sigara.
Fatwa hiyo imezua
kivumbi nchini Misri baina ya wanaoikubali na wanayoipinga,lakini ukweli
utabaki ni ukweli kuwa sigara ina madhara makubwa.
Nchi nyingi za Kiarabu
ni lazima katika kila pakti ya sigara kuwe na ibara ifuatayo:
((ÊóÍúÐöíúÑñ Íõßõæúãöíøñ:Åöäøó ÇáÏøõÎóÇäó ÓóÈóÈñ ÑóÆöíúÓöíøñ
áöÃóãúÑóÇÖö ÇáÑøöÆóÉö æóÇáÓøóÑóØóÇäö æóÇáÔøóÑóÇíöíúäö æóÃóãúÑóÇÖö
ÇáÞóáúÈö))
yaani: ((Tangazo la
Serikali:Sigara ni sababu kuu ya maradhi ya mapafu,kensa, kuziba mishipa
ya damu,na maradhi ya moyo)).
Matangazo yanayofanana
na hayo yameanza kuonekana katika mabango ya njiani katika Jiji la
Dares-Salaam.
|