NAMNA ZA KUHIJI

 

Kuhiji kuna namna tatu, nazo:

1-     Tamat-tuu: Nayo ni kuhirimia umra peke yake katika miezi ya hija, akimaliza atatokana na ihramu ya ibada hiyo, kisha atahirimia hija siku ya Tarwiya (8 Dhul-hija) au kabla yake. Tamat-tuu ndio namna bora ya kuhiji, na inashurutiziwa iwe umra na hija katika mwaka mmoja na safari moja na asirejee nchini kwake au mfano wake kwa umbali baina ya ibada mbili hizo.

Mfanya-tamat-tuu humwajibikia kichinjo cha Tamat-tuu.

2-     Qiraanu: Nayo ni kuhirimia hija pamoja na umra katika miezi ya hija kisha kubaki na ihramu mpaka atakapotokana na ihramu ya ibada mbili hizo kwa pamoja siku ya kuchinja (10 Dhul-hija).

Mfanya-Qiraanu huwajibika pia kuchinja. Yeye inamtosheleza Tawafu moja na Sai moja kwa hija na umra yake, kutokana na kauli yake - rehema za Allah na amani zimshukie: “Mwenye kuhirimia hija pamoja na umra itamtosha Tawafu moja na Sai moja kwa zote mbili mpaka ajihalalishe nazo pamoja.” Ameipokea Tirmidhi na Ibnu Maajah. Na kuna kauli kuwa lazima kuwe na Tawafu mbili na Sai mbili.

Lakini huyu aingiapo Maka atatufu Tawafu ya Quduum (kufika Maka), na anaweza kufanya Sai kabisa akitaka, halafu atakaporejea siku ya  kufanya Tawafu ya Ifadha akatoshelezeka kwa Tawafu tu; kwasababu ameshafanya Sai hapo kabla kwa uoni wa baadhi ya wanazuoni. Na kuna kauli aakhirishe Sai apate kuifanya pamoja na Tawafu ya Ifadha.

3-     Ifraadu: Nayo ni kuhirimia hija peke yake na kubaki na ihramu yake mpaka atakapolirushia vijiwe Jamratul-Aqaba siku ya kuchinja (10 Dhul-hija).

 

?      Mfanya-Ifraadu haimlazimu umra anapofanya hija pekee. Akitaka kufanya umra ni baada ya siku za Tashriiq (ambazo ni 11 – 13 Dhul-hija).

?      Inajuzu kuhirimia hija pekee hata kwa ambaye hakufanya umra hapo kabla.

Mfanya-Ifraadu inamjuzia kutufu Tawafu ya Quduum bila kufanya Sai

 

Copyright ©2004  Uislam.net