NASAHA ZA RAMADHAN

1- Jitahidi kuufanya mwezi huu mtukufu uwe mwezi wa kuihisabu amali zako na kutubia na kutengeneza makosa yako.

2- Jitahidi  kusali sala ya jamaa na tarawehe; kwani Mtume (SAW) kasema: “ Atakae Sali na Imam mpaka akamaliza, basi ataandikwa kuwa miongoni mwa wale waliosali usiku”

3-  Jikinge na israfu ya mali na nyegineo; kwani israfu imeharamishwa na inakupunguzia nafasi ya kutoa sadaka na thawabu zake.

4-   Weka juhudi kuendelea na mambo mema ambayo umejizowesha kuyafanya katika mwezi huu mtukufu.

5-   Hakika mwezi huu ni mwezi wa ibada, sio mwezi wa uvivu na kulala.

6-  Uzoweshe ulimi wako kwa kuudumisha na kumdhukuru Allah, na wala usiwe miongoni mwa wale walio kuwa hawamdhukuru Allah isipokuwa kidogo.

7-  Unapohisia njaa kumbuka kuwa wewe ni dhaifu na wala huwezi kuvumilia kukosa neema za Allah (chakula, maji…..nk).

8-  Usiwache nafasi ya mwezi huu mtukufu kwa kujizuwia kwa mabaya ambayo hayakupi manufaa yoyote bali yanakuletea madhara.

9- Juwa kuwa kazi ni amana, basi jihisabu nafsi yako kwa kujiuliza : Je nimeifanya kama inavyotakikana.

10- Kimbilia kuomaba msamaha kwa yule uliyomdhulumu kabla ya kukuchukulia thawabu zako (kesho Akhera).

11- Jitahidi kulisha aliefunga ili upate ujira (malipo) kama yake.

12- Jua kuwa Allah ni mwingi wa kukirimu na mwingi wa kurehemu na anakubali toba ya wenye kutubia na kuwa Allah ndiye mwenye kuadhibu adhabu kali, anatoa nafasi ya kutubia na wala hapuuzi waja wake.

13- Kama ulifanya ovu na Allah (SWT) akakusitiri, basi jua kuwa hilo ni onyo kwako wewe ili utubie, basi kimbilia kuomba msamaha na azimia kutorudia kutenda ovu hilo.

14- Juwa kuwa Allah ametuhalalishia kuzifurahisha nyoyo zetu mbali na haramu, lakini usijiendekeze kwa kuutumia wakati wote kwa kujifurahisha nafsi yako na ukapitisha nafasi ya kufanya mambo ya kheri.

15- Juwa kuwa kutafuta ilimu ni ibada, basi jitahidi na kusoma tafsiri za Qur’an,  hadithi za Mtume (SAW) na mwendo wake pamoja na elimu ya dini.

16- Jitenge na marafiki wabaya na jitahidi kukaa na marafiki wazuri (wema).

17- Kwa hakika kujizowesha kwenda msikitini mapema ni dalili ya imani na kuwa na hamu ya kufanya ibada.

18- Jitahidi kuwaongoza waliokuwa chini ya uwongozo wako kwa mambo yanayowafaa na dini yao, kwani wao wanakusikiliza zaidi kuliko wengineo.

19- Usifanye/usipike namna nyingi za vyakula kwani itakushughulisha kutopata nafasi ya kusoma Qur’an na kufanya ibada.

20- Punguza kwenda sokoni au madukani katika siku za Ramadhani na hasa siku za mwisho wa Ramadhani ili usije ukapitwa na hizo siku thamini.

21- Kumbuka kuwa mwezi huu mtukufu ni mgeni wa kupita njia basi jitahidi na kuupokea (kumkirimu mgeni huyo) kwa vizuri.  Kwani ni haraka kumkumbuka akiondoka.

22- Jitahidi na kuamka usiku kusali katika kumi la mwisho la Ramadhani kwani hizo siku zinafadhila kubwa sana, na ndani yake kuna usiku mmoja ambao bora kuliko miezi elfu moja.

23- Kaa ukijua kuwa siku ya Idi ni siku ya kumshukuru Mola basi usiifanye kuwa siku ya kuanza kuyarudia yale maovu ambayo ulikuwa umejizuia katika mwezi wa Ramadhani.

24- Tahadhari na kula mchana wa ramadhani bila ya dharura ya kukubalika, kwani atakae fanya hivyo hatoweza kuikidhi siku hiyo hata akifunga milele.

25- Jitahidi kufanya itikafu japo kidogo (hasa katika kumi la mwisho).

26- Inapendeza kupiga Takbir kwa sauti kuanzia usiku wa Idi na asubuhi yake mpaka ifike wakati wa sala ya Idi.

27- Jihisabu/jipime nafsi yako katika mambo yako yote kama:

Kuhifadhi sala ya jamaa-zakaa-kutembelea jamaa zako-kuwafanyia wema wazi wako (mama na baba)-kutembelea jirani-kutofanya israfu-kuwapa malezi mazuri waliokuwa chini ya uongozi wako-kujishughulishe na mambo yanayowahusu ndugu zako wa kiislamu- kutahadhari na kujionesha-kumpendea ndugu yako muisilamu jambo unalolipendea nafsi yako-kutowasema (nyuma yao) ndugu zako wa kiisilamu-kuisoma qur’ani na kuzingatia maana yake-kuwa na utulivu unapoisikia.

æÇáÜÜÓÜÜáÇã ÚÜáÜíÜßÜã æÑÍÜãÜÉ Çááøå æÈÜÑßÜÜÇÊÜÜå