|
|
NASAHA ZA MWANAMKE WA KIISLAMU |
ÈöÓúãö Çááøóåö ٱáÑøóÍúãóÜٰäö ٱáÑøóÍöíãö
1.
MWANAMKE WA KIISLAMU
ni mwenye kuamini Allah mtukufu
kuwa ndie Mola wake wa
haki, na kuwa Muhammad (s.a.w) ni Mtume wake, na kuwa Uislamu ndio
Dini yake, basi anakuwa ni mwenye kutokeza kwake athari za Imani yake kwa
Maneno, Matendo na Itikadi, anakuwa ni mwenye hadhari kubwa yasije
yakamchukuwa Makasiriko ya Allah mtukufu, ni mwenye kuogopa Maumivu ya
Adhabu yake na Ubaya wa kwenda kinyume na Amri zake, amesema Mtume Muhammad
(s.a.w): ((Sio Imani kwa kutamani, lakini Imani ni ile
aliyotulizana katika Moyo na ikasadikishwa na Matendo)).
2.
MWANAMKE WA KIISLAMU
anahifadhi Sala tano kwa Udhu wake katika wakati wake, wala
hashughulishwi na chochote akawacha Sala, wala hababaishwi na Mila yoyote
akawacha Ibada, basi idhihirike kwake athari ya Sala, kwani hakika ya Sala
ni yenye kukataza machafu na maovu, basi hii ndio hifadhi kubwa ya kumlinda
na Maasi, amesema Mtume Muhammad (s.a.w): ((Munaona vipi,, ikiwa mbele ya
mlango wa mmoja wenu pana mto wa maji, na akawa anakoga ndani yake kila siku
mara tano hivi kitabakia kitu katika uchafu wake?)) Wakasema:
Hakibakii kitu katika Uchafu wake. Akasema (s.a.w): ((Basi huo ndio
Mfano wa hizi Sala tano)).
3.
MWANAMKE WA KIISLAMU
anahifadhi Hijabu yake na anajitukuza kwa kujishika nayo vizuri, basi yeye
hatoki nje isipokuwa amejihifadhi kwa heshima za Dini yake, akitaka hifadhi
ya Mola wake kwa kumkirimu na kumlinda yeye kwa pambo la Hijabu, na akataka
kumtakasa kwa tabia bora, amesema Allah mtukufu ((Ewe Nabii,, Waambie
Wake zako na Watoto wako wa kike, na Wanawake wa Waumini, wajishike vizuri
kwa kujilazimisha juu yao Majil-babu (Nguo mzito zinazoficha mapambo yote ya
maumbile ya mwanamke) hilo ndio ukaribu zaidi wa kujulikana wasije
wakafanyiwa maudhi na amekuwa Allah ni mwingi wa kusamehe mwingi wa kurehemu))
[Ah-zaab 59]
4.
MWANAMKE
WA KIISLAMU anajitahidi katika kumtii Mume wake, basi anakuwa ni
mwepesi katika kutimiza haki zake, anamrehemu na kumuita kunako mambo ya
kheri na anamnasihi na kutaka nasaha kwake, anafanya kwa Mume wake yale
yanampendezesha, na wala hanyanyui sauti yake juu ya Mume wake na hazungumzi
na yeye kwa ukali, amesema Mtume Muhammad (s.a.w): ((Atakaposali Mwanamke
Sala zake tano, na akafunga mwezi wake, na akamtii Mume wake ataingia katiia
Pepo ya Mola wake kwa mlango atakaotaka)).
5.
MWANAMKE WA KIISLAMU
anawalea Watoto wake malezi mema ya kumtii Allah mtukufu na Mtume wake
Muhammad (s.a.w), anawanyonyesha Itikadi sahihi ya Uislamu, anaotesha katika
mioyo yao Mapenzi ya Allah mtukufu na Mtume wake Mkarimu Muhammad (s.a.w),
na anafanya kila juhudi ya kuwaepusha na kuwahadharisha kunako Maasi na
Tabia mbaya, amesema Allah mtukufu: ((Enyi ambao mumeamini,, Okoweni
Nafsi zenu na watu wenu kunako Moto, kuni zake ni watu na mawe, uwewekewa
Malaika wasio kuwa na huruma walio wakali hawamuasi Allah kwa aliyowaamrisha
na wanafanya yote waliyoamrishwa)) [Tahriim 6].
6.
MWANAMKE WA KIISLAMU
hakubali kuwa pamoja na Mwanamme wa kando()
peke yao, amesema Mtume Muhammad (s.a.w): ((Hawatokaa Mwanamme na
Mwanamke peke
yao isipokuwa Shetani atakuwa ni wa tatu wao)).
Basi yeye hatosafiri isipokuwa na Maharimu wake au Mume wake na wala havamii
masoko na sehemu za makusanyiko ya watu isipokuwa kwa dharura inayokubalika
kisheria, tena akiwa ni mwenye Hijabu yake na heshima zake amejisitiri kwa
pambo la Uchamungu.
7.
MWANAMKE WA KIISLAMU
hajifananizi na Wanaume katika yanayowahusu, wala haunganisi nywele zake,
wala hanyowi wala kupara nyusi zake, wala hachongi meno yake, wala haweki
chapa katika mwili wake, wala hajifananishi na Wanawake Makafiri katika
yanayowahusu kwa nguo zao na sehemu zao na namna zao, amesema Mtume Muhammad
(s.a.w): ((Amelaaniwa na Allah mwenye kuchonga nyusi zake na mwenye
kuifanya kazi hiyo, na mwenye kuunganisha nywele zake na mwenye kifanya kazi
hiyo, na mwenye kujipiga chapa katika mwili wake na mwenye kuifanya kazi
hiyo, mwenye kuchonga meno kwa kutaka uzuri wa mwanya , kama alivyowalaani
wanawake wenye kujifananisha na Wanaume, na wanaume wenye kujifananisha na
Wanawake)), na amesema: ((Mwenye kujifananisha na watu fulani basi
huyo atafufuliwa pamoja na wao)).
8.
MWANAMKE WA KIISLAMU
ni mwenye kuita Wanawake wenzake katika Kumtii Allah mtukufu na Mtume wake
Muhammad (s.a.w) kwa maneno mazuri na vitendo vyema, na kwa kuwatembelea
majirani zake, jamaa zake, ndugu zake na kuwazawadia zawadi za kuwaongoza
katika njia anayoiridhia Allah mtukufu. Na hali yeye mwenywewe ni mwenye
kufanya kwa yale anayoyasema na kuyahimiza ili kuiokowa nafsi yake na
wenzake kunako Laana na Makasiriko na Adhabu ya Allah mtukufu. Amesema Mtume
wa Allah (s.a.w): ((Kwa hakika kumuongoa Allah mja yoyote kwa sababu yako
ni bora kwako kuliko ngamia wekundu)).
9.
MWANAMKE WA KIISLAMU
anahifadhi Moyo wake kunako yenye kubabaisha na yenye matamanio, pia
anahifadhi jicho lake kuona mambo ya haramu, na sikio
lake kusikiliza ya haramu
kama muziki, upuuzi, na machafu
ya kuteta na fitina na matusi…. Na anahifadhi viungo vyake vyote kunako
kufanya maasi na huku anajuwa kuwa huo ndio Uchamungu, amesema Mtume
Muhammad (s.a.w): ((Oneni haya kwa Allah mtukufu, na mwenye kumuonea haya
Allah mtukufu haki ya kumuonea haya hakika atahifadhi kichwa chake na
yanayokifika, na atahifadhi tumbo
lake na yanayoingia, na atakayekumbuka mifupa
ya kaburini hatodanganywa na mapambo ya Duniani)).
10.
MWANAMKE WA KIISLAMU
anahifadhi wakati wake usipotee bure, na mchana wake na usiku wake usije
ukachanika ovyo, basi yeye ni mwenye kujitenga na kusengenya (kuteta), Ulimi
mrefu, sauti refu, matusi, dharau, kujisahau ovyo, kupumbazika na mavutio ya
kinafsi, amesema Allah mtukufu: ((Na waache wale ambao wamefanya Dini yao
kuwa ni Michezo na Mapumbazo ya kinafsi, na yakawadanganya maisha ya kidunia,
na wewe kumbusha kwa hilo, isije ikaangamizwa nafsi kwa yale iliyochuma,
nayo haina asiyekuwa Allah kipenzi wala muombezi, na hata ikitolewa kila
fidia haitokubaliwa kwake, hao ndio walioangamizwa kwa sababu ya yale
waliyochuma, watapata wao kinywaji cha maji yenye kuchemka mno na adhabu
yenye kuumiza kwa walivyokuwa wakikifuru)) [An-aam 70] na amesema Allah
mtukufu kwa kuwazungumzia wale waliopoteza Maisha yao ya kuwa watajuta huku
wakisema ((Ee,, OLE wetu kwa tulivyopuuza! Na wao watabeba mizigo yao juu
ya migongo yao, Ee,, ifahamike kuwa ni maovu mno hayo wanayoyabeba))
[An-aam 31].
NDUGU YANGU WA KIKE HEBU KUWA NGUVU YA HAKI
KATIKA JAMII KWA YALE ANAYOIRIDHIA ALLAH MTUKUFU AMBAYE AMEKUUMBA WEWE NA
KILA KITU, NA USIWE NGUVU YA BATILI YA NAFSI NA SHETANI WA KIJINI NA WATU
UTAANGAMIA NA KUANGAMIZA JAMII YAKO.
EWE MOLA
MUONGOZE MWAMKE WA KIISLAMU KWA YALE UNAYOYAPENDA NA UKAYARIDHIA NA UUPE
MOYO WAKE NURU YA IMANI YA KWELI (AMIN).
Alisema Mtume wa Allah (s.a.w): ((Makundi
mawili ya walio wa motoni sijayaona bado, wanaume katika mikono yao kuna
bakora kama mikia ya n`gombe wanapiga watu ovyo, na wanawake wamevaa lakini
wako uchi wanatembea kimaringo vichwa vyao kama nundu za ngamia ziliyoinama,
hawatoingia peponi wanawake hao, wala hawatapata hata harufu yake, na hakika
harufu yake inapatikana masafa kadha wa kadha)).
NA AMANI KWA ATAKYEFUATA UONGOFU
Assante sana
Imetayarishwa na Imamu wa Msikiti wa Ibadhi -
Buja.
Hafidh. H. Seif Sawafiy.
Tel. 991787
|