SALA YA TARAWEEH

1) HUKUMU YAKE:

Sala ya Taraweeh ambayo pia huitwa sala ya kisimamo cha Ramadhan (Salat L’Qiyam) ni katika Sunna amabazo inatakiwa Muislamu azitilie umuhimu na kutozipuuza. Mtume wetu Muhammad (S.A.W)alisali sala hii ya Taraweeh na masahaba zake sala ya jamaa baaadhi ya siku za Ramadhani, kasha hakuendelea baada ya hapo kuisali jamaa alikhofia isije ikafaridhioshwa. Na sala hii ni Sunna sio kama wanavyosema baadhi ya watu kuwa ni faridha ila anae acha kuisali anahesabiwa yuko duni katika daraja.

2) WAKATI WAKE:

Husaliwa baada ya sala ya Ishaa katika siku za mwezi mtukufu wa Ramadhani. Wakati  wake huanzia baada ya sala ya Ishaa mpaka kabla ya adhana ya Al-fajiri. Na utaratibu wa kusali sala hii ni kwanza kusali sala ya Ishaa rakaa nne, kisha Sunna ya Isha rakaa mbili.

3) IDADI YA RAKAA KATIKA SALA YA TARAWEEH:

Mtume (S.A.W) alisali sala hii rakaa nane. Abubakar (Allah awe radhi juu yake) wakati wa ukhalifa wake aliongeza rakaa nane nyingine zakawa rakaa 16, na Omar bin Alkhattab (Allah awe radhi juu yake) wakati wa ukhalifa wake pia aliongeza rakaa nane nyingine zikawa rakka 24. Na hizi rakaa walizoengeza ni ziada kutoka kwa Makhalifa hawa wawili; Abubakar na Omar (Allah awe radhi juu yao). Hii ni dalili ya kuwa sala ya Taraweeh upo uwezekano wa kuongeza idadi ya rakaa isipokuwa ni bora zaidi kumfuata Mtume Muhammad(S.A.W) amabe aliisali sala hii rakaa nane.

Kisimamo (Qiyam) kimoja katika sala ya Taraweeh ni rakaa nne. Na unaweza ukasali sala hii kwa kisimamo (Qiyam) kimoja au viwili au vitatu inategemea uwezo wako. Na baina ya visimamo (Qiyam) viwili (baada ya rakaa nne), unamdhukuru Allah na kuomba Duaa. Na ndio maana sala hii ikaitwa “QIYAM RAMADHAN”. Katika wakati huo unaweza kumdhukuru Allah kama ifuatavyo:

SUBHAANA LLAH, WAL HAMDU LILAH, WALA ILAHA ILLA LLAH, WALLAHU AKBAR, WALILAHI LHAMD. ADADA KHALQIHI WAZINAT ARSHIHI WAMIDAADA KALIMATIH WARIDHAA NAFSIHI WAKAMA YANBAGHI LAHU WAKAMA HUWA LAHU AHL LA YANQATIU WALA YANFADU MIN AZALI L’AZAL ILA ABAD L’ABAD. WA SALA LLAGHU WASALAM ALAA SAYYIDNA MUHAMMAD WA ALAA ALIHI WASAHBIHI AJMAIIN.

4) VIPI HUSALIWA:

I) RAKAA YA KWANZA

Fanya yafuatayo:

a) Soma Tawjeeh (SUBHAANAKA LLAHUMA, WABIHAMDIKA, TABAARAKA S’MUKA, WATAALA JADUKA, WALA ILAHA GHAIRUKA. INNI WAJJAHTU WAJHIYA LILLADHI FATTARA SAMAAWAATI WAL ARDHA HANIIFAN WAMAA ANAA MINA L’MUSHRIKIIN).

b) Piga Takbiratul Ihraam (Allahu Akbar)

c) Soma Istiadha kutokana na shetani (audhubillahi mina shaytani rajeem)

d) Soma Suratil Faatiha na kisha soma sura yeyote katika Quran, na inapendekezwa kusoma sura ndefu.

e) Rukuu kisha sujudi.

II) RAKAA YA PILI

Fanya yafuatayo:

a) Soma Al Fatiha na surah

b) Rukuu na sujudi

c) Kaa Tashahhud (kukaa tahiyyat), soma tahiyyat (Attahiyyaatu lillahi wassalawaatu wattayyibaatu. As’salamu alayka ayyuha nnabiyyu warahmatu llahi wabarakaatuh. As’salamu alayna wa alaa ibadi llahi ssaalihin. Ash’hadu an’laa Ilaaha illa llah wa ash’hadu anna Muhammadan abduhu warasuluh.

d) ToaTaslim (kutoa salaam)

III) RAKAA YA TATU

Inuka rakaa ya tatu bila takbira, Katika hii rakaa fanya kama ulivyofanya katika rakaa ya kwanza.  Soma tawjeeh(SUBHAANAKA LLAHUMA, WABIHAMDIKA, TABAARAKA S’MUKA, WATAALA JADUKA, WALA ILAHA GHAIRUKA, takbiratul ihraam, istiadha, soma suratil Faatiha na sura nyingine.

IV) RAKAA YA NNE

Fanya kama ulivyofanya katika rakaa ya pili lakini atahiyyat unaimaliza mpka mwisho (Attahiyyaatu lillahi wassalawaatu wattayyibaatu. As’salamu alayka ayyuha nnabiyyu warahmatu llahi wabarakaatuh. As’salamu alayna wa alaa ibadi llahi ssaalihin. Ash’hadu an’laa Ilaaha illa llah wa ash’hadu anna Muhammadan abduhu warasuluh. Allahuma Sali alaa Muhammad wa alaa aali Muhammad kama sallayta alaa Ibrahim wa alaa aali Ibrahim, wabaarik alaa Muhammad wa alaa aali Muhammad kama baarakta alaa ibrahim wa alaa aali Ibrahim fil aalamina innaka hamiidun majiid. Na baada ya salaam unakaa kumdhukuru Allah na kuomba dua. Hapa inakuwa tayari umemaliza kisimamo (Qiyam) cha kwanza.

Hukumu ya Duaa Baada Ya Kila Rakaa Nne (baada ya kila Qiyam):-

Dua zinazoombwa baada ya taraweeh si lazima wala si moja katika yanayotakikana kufanywa katika salaa. Lakini inapendekezwa kumuomba Allaha baada kila salaa.  Kama alivyosema allah Taala:

(ÝóÅöÐóÇ ÝóÑóÛúÊó ÝóÇäÕóÈú æóÅöáóì ÑóÈøößó ÝóÇÑúÛóÈú) BASI UKISHAMALIZA (KULINGANIA) SHUGHULIKA (KWA IBADA) NA JIPENDEKEZE KWA MOLA WAKO (94: 7-8)

Watu husoma dua baada ya kila rakaa nne katika taraweeh kwa kusoma albaqiyatul swalihat SUBHAANA LLAH, WAL HAMDU LILAH, WALA ILAHA ILLA LLAH, WALLAHU AKBAR, WALILAHI LHAMD. ADADA KHALQIHI WAZINAT ARSHIHI WAMIDAADA KALIMATIH WARIDHAA NAFSIHI WAKAMA YANBAGHI LAHU WAKAMA HUWA LAHU AHL LA YANQATIU WALA YANFADU MIN AZALI L’AZAL ILA ABAD L’ABAD. WA SALA LLAGHU WASALAM ALAA SAYYIDNA MUHAMMAD WA ALAA ALIHI WASAHBIHI AJMAIIN. Na kufanya hivyo si lazima lakini inapendekezwa.

5) KUMBUSHO (Tanbih)

A) Mwezi mtukufu wa Ramadhani ni fursa kubwa ya kuongeza kwa wingi thawabu zako kwani thawabu zake ni kubwa kuliko miezi mingine.  Tumia fursa hii wala usiiharibu au kuipoteza kwa mambo yasiyokuwa na faida kwako.

B) Allah wa RamadhanI ndiye huyo wa Shaaban na miezi mingine.  Jitihada yako ya ibada isiwe katika Ramadhani tu bali iwe ni jitihada ya kuendelea katika miezi yote ya mwaka.

C) Inajuzu mwanamke muislamu kusali taraweeh jamaa nyuma ya imamu kwa sharti; asali mistari ya nyuma, avae mavazi ya kusitiri  mwili wake wote bila ya kuonyesha viungo na asipake mafuta mazuri ya kunukia.  Siku hizi zipo sehemu misikitini za kusalia wanawake. Mwanamke akisali nyumbani kwake ni bora lakini akitaka kusali Taraweeh jama na imam msikitini basi hakatazwi.

D) Usitie mkazo na bidii kusali nawafil na sunna kama vile Taraweeh halafu ukapuuza sala za faridha na pia kuchelewa kwenda kusali sala ya alfajiri jamaa.

E) Baadhi ya watu hudhania kuwa rakaa za sala ya Taraweeh zimeungana na zinaendelea.  Wanaosali husimama baada ya rakaa ya pili kuingia ya tatu kwa kutoa takbira na huiacha takbiratl ihraam katika rakaa ya tatu pamoja na kuwa wametoa salaam baada ya rakaa ya pili na hili ni kosa.  Na iliyokuwa sawa ni baada ya kutoa salaam katika rakaa ya pili unasimama kuingia rakaa ya tatu bila ya takbir.  Halafu unasoma tawjeeh kisha unatoa takbiratul ihraam.

F) Baadhi ya watu husali sala ya taraweeh mbio mbio ili wakamilishe rakaa ishirini. Ni bora kusali rakaa nane kwa utulivu kuliko kusali rakaa ishirini mbio mbio.  Kwa sababu kusali kwa utulivu inakutia utulivu (khushuu) katika sala yako.  Na utulivu ndio roho ya salaa.

G) Ikiwa muislamu atachanganya sala (ikiwa amesafiri), ya maghrib na ishaa kwa kuzisali zote wakati wa magharibi (jamaa taqdiim), inafaa kusali salatil taraweeh baada ya sala ya magharibi na ishaa.  Na pia ikiwa atachanganya sala ya magharibi na ishaa kwa kuzisali zote wakati wa sala ya ishaa (jamaa taakhir), inafaa kusali sala ya taraweeh baada ya kusali magharibi na ishaa.

H) Na mwisho, ndugu yangu muislamu, kumi la mwisho katika mwezi mtukufu wa ramadhani uko usiku ambao ni bora kuliko miezi elfu moja.  Usiku huo ni Laylatul qadr.  Kazania sana kufanya ibada na kumdhukuru Allah katika siku hizo kumi.  Kumi la mwisho si wakati wakushughulika na kujitayarisha na siku kuu ya Eid.  Utakuwa umeipoteza fursa kubwa sana ikiwa kama hutoshughulika na ibada.