SALA YA ISTIKHARA

ÈöÓúãö Çááøóåö ٱáÑøóÍúãóÜٰäö ٱáÑøóÍöíãö

Unapofikwa na jambo au kuliazimia ni vizuri kutawadha kisha ukamuelekea Mola wako mtukufu kwa kusali rakaa mbili kwa nia ya kumtaka ya kheri kwako katika jambo hilo na kupata taufiki yake katika anayoyaridhia, na baada ya kutoa salamu unamuelekea Mola wako Allah mtukufu kwa dua hii.

 

(Çóááøóåõãøó Åöäøöíú ÃóÓúÊóÎöíúÑõßó ÈöÚöáúãößó æóÃóÓúÊóÞúÏöÑõßó ÈöÞõÏúÑóÊößó æóÃóÓúÃóáõßó ãöäú ÝóÖúáößó ÇáúÚóÙöíúãö¡ ÝóÅöäøóßó ÊóÚúáóãõ æóáÇó ÃóÚúáóãõ¡ æóÊóÞúÏöÑõ æóáÇó ÃóÞúÏöÑõ¡ æóÃóäúÊó ÚóáÇøóãõ ÇáúÛõíõæúÈö.Çóááøóåõãøó Åöäú ßõäúÊó ÊóÚúáóãõ Ãóäøó åóÐóÇ ÇúáÃóãúÑó ÎóíúÑñ áöíú Ýöíú Ïöíúäöíú æóãóÚóÇÔöíú æóÚóÇÞöÈóÉö ÃóãúÑöíú ÝóíóÓøöÑúåõ áöíú æóÈóÇÑößú áöíú Ýöíúåö¡ æóÅöäú ßõäúÊó ÊóÚúáóãõ Ãóäøó åóÐóÇ ÇúáÃóãúÑó ÔóÑøñ áöíú Ýöíú Ïöíúäöíú æóãóÚóÇÔöíú æóÚóÇÞöÈóÉö ÃóãúÑöíú ÝóÇÕúÑöÝúåõ Úóäøöíú æóÇÕúÑöÝúäöíú Úóäúåõ æóÇÞúÏõÑú áöíó ÇáúÎóíúÑó ÍóíúËõ ßóÇäó Ëõãøó ÈóÇÑößú áöíú Ýöíúåö æóÑóÖøöäöíú Èöåö)

 

((Allwahumma inniy as-takhiiruka biil-mika, wa astaq-diruka biqud-ratika, wa as-aluka min fadh-lika l-adhiim, fainnaka taalamu wala aalamu, wataq-diru wala aq-diru, wa anta allaamu l-ghuyuub. Allwahumma in kunta taalamu anna hadha l-amra khayrun liy fii diiniy wa maashiy wa aaqibati amriy fayassir-hu liy wabaarik liy fiihi, wain kunta taalamu anna hadha l-amra sharrun liy fii diiniy wa maashiy wa aaqibati amriy fas-rif-hu anniy was-rif-nniy an-hu waqaddir liya l-khaira haithu kaana, thumma baarik liy fiihi wa radhdhiniy bihi))

TAFSIRI YA DUA

((Ewe Mola wangu hakika mimi ninakutaka ya kheri kwa elimu yako, na ninakutaka uwezo kwa uwezo wako, na ninakuomba katika fadhila zako kuu, kwa hakika wewe unajuwa wala mimi sijui, na wewe unaweza wala mimi siwezi, na hakika wewe ni mwenye kujuwa yaliyofichika. Ewe Mola wangu ikiwa unajuwa kuwa jambo hili ni kheri kwangu katika dini yangu na maisha yangu na mwisho wangu basi lifanyie wepesi kwangu na ulibarikie kwangu, na ikiwa unajuwa kuwa jambo hili ni shari kwangu katika dini yangu na maisha yangu na mwisho wangu basi liepushe kwangu na uniepushe nalo na unikadirie la kheri popote pale lilipo kisha unibarikie ndani yake na uniridhie kwalo))

Wabillahi tawfiq

Ndugu yenu:Hafidh. H. Seif Sawafiy.

 

Copyright ©2006 Uislam.net