|
|
A'Salaam Alaykum Warahmatullah Wabarakatuhu
Napenda kukuarifu ya kwamba niko njiani ninakuja na nitakuwa mgeni wako hapo
nyumbani kwa kipindi cha mwezi mmoja, natumai umejiandaa vizuri sana
kunipokea kama mgeni wako mtukufu kabisa kuliko wageni wako wote wanaokuja
hapo nyumbani, ikiwa utabahatika kukutana na mimi na kuwa mgeni wako tena
mwaka huu huna budi kumshukuru Allah (SW) kwa kupata fursa nyengine tena ya
Ninakushukuru sana kwa mapokezi yako ya kila mwaka na juhudi yako ya
kunitumia ili niweze kukufaa siku ya hesabu, nitafurahi zaidi ikiwa
umejiandaa vizuri zaidi na utanitumia kwa juhudi zako zote mwaka huu kuliko
mwaka jana, ninatambua kwamba mwaka huu sitokuwa nao baadhi ya wenzako ambao
niliwakuta mwaka jana leo hii wako mbele ya haki, fursa hii adhimu umeipata
natumai kwa juhudi zako zote japo kuwa zimebaki siku chache tu na lolote
linaweza likatokea katika kipindi hiki kifupi.

UKUMBI WA UISLAMU.NET
|
|