Sheikh Said bin Mabrook Al-Qanoobi ni mmoja katika wanavyuoni wakubwa, khasa katika utafiti wa Hadith na elimu zake, na Elimu za usuul na Fiqh. Sheikh Said ana fatwa nyingi katika mambo mbali mbali ya Kisheria. Sheikh kaandika vitabu vinavyofaida kubwa pamoja na kuwa na fatwa nyingi ambazo hazijachapishwa.

Sheikh wetu huwa ni mgeni katika kipindi cha (Sual Ahli Dhikr) kinachotolewa na Television ya Oman kila siku katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kujibu masuala tofauti.

Inshallah hivi karibuni tutajitahidi kuwawekea wasomaji baadhi ya masuala aliyoyajibu sheikh Said katika kipindi hiki.

 

 

FADHILAT SHEIK SAID BIN MABROOK AL-QANOOBI